Uchaguzi 2020 Halima Mdee, fedha za mfuko wa jimbo umepeleka wapi?

Ndungu zangu wana jamvi habari za muda huu.

Leo nimepata wasaha wa kupitia Kitabu cha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya jimbo la kawe (2015-2020)
kilichoandikwa na aliyekuwa mbunge wetu Halima James Mdee.

Nimeshtushwa sana na nilichokiona kwenye kitabu hiki, naomba kuwashirikisha kitu ambacho kimepelekea nishtuke mimi kama mkazi wa jimbo la Kawe na mnufaika wa fedha za mfuko wa jimbo.

Kwenye kipengele kinachosomeka Taarifa ya Miradi ya Maendeleo ya Fedha za mfuko wa Jimbo.

Jina la Mradi: Kujenga Kivuko cha waenda kwa miguu Soko la Samaki Ununio

Mwaka 2017/18- (Uk.25 )

Tsh. Mil 5,000,000/= zilitengwa kwa ajili ya mradi huo wa kivuko cha waenda kwa miguu kilichopo karibu na soko la samaki la ununio.

Mwaka 2018//19- (Uk.27)

Mradi huo huo unaonekana katika ukurasa namba 27 huku ukitengewa Kiasi cha Tsh Mil 13,500,000/= lakini utekelezaji wake kama ilivyoandikwa kwenye kitabu hiki bado ulikuwa katika hatua za awali za manunuzi.

Mwaka 2019/20 - (Uk.31)

Mradi huo huo tena unaonekana kutengewa kiasi cha Tshs Mil 20,000,000/= kwenye page no 31. Huku mbunge wetu akijinadi kwenye kitabu hiki kuwa mradi huo umekamilika.

Lakini kiuhalisia kabisa ni kwamba mradi huo hadi ninavyoandika thread hii , haujakamilika na hautumiki hata na mkazi mmoja wa ununio na kata nzima ya kunduchi kwa ujumla.

Kwa hiyo mradi mmoja wa kivuko cha waenda kwa miguu soko la samaki ununio umegharimu Jumla ya kiasi cha Tshs Mil 38,500,000/= ndani ya kipindi cha miaka 2 (2018-2020) , ambazo ni fedha zinazosimamiwa na kutolewa na Ofisi ya Mbunge ambaye ni Mh.Halima Mdee.

Kwa tafsiri nyepesi kabisa inaonyesha hakukua na usimamizi mzuri wa fedha za jimbo la Kawe chini ya dada yetu Halima.

Ndugu zangu wana Jamvi nimeattach hapa picha za mradi uliotajwa kwenye taarifa kama ulivyo kwa sasa.

Ally Ramadhan Salehe

Ununio Mwisho-Kunduchi
 

Attachments

  • IMG-20201001-WA0035.jpg
    99.7 KB · Views: 2
  • IMG-20201001-WA0020.jpg
    126.9 KB · Views: 2
  • IMG-20201001-WA0024.jpg
    126.8 KB · Views: 2

Gwajima kaajiri wachumia tumbo kibao, kuna id kibao za kumpigia debe Gwajima, ila wote wanaimba single moja. Nawashauri pigeni hela za huyo boya maana hiki ni kipi cha kula hela za Mabwege, lakini mtashangaa matokeo. Mbinu pekee ya ccm kushinda hilo jimbo ni kutoka na mabox ya kura kwa uratibu wa jeshi la polisi, na tume ya uchaguzi.
 
Apelekwe mahakamani haraka.
 
Dah huyu mama kweli wanakawe wanahaki ya kumlaani yan watu tunashwa kuvuka kisa wewe
 
Huyu Dada ni kiongozi wa maneno na sio wanadharia ila tulichelewa tu kumgundua na ametumia ubabe sana ktk kutoa sera
 
Huyu bibi sauti ya zegee hafai kabsa kuwa ubunge kama miaka 10 ameshindwa kumalizia kivuko yan tunashindwa kufanya biashara Zetu kwa wakati kisa we mjinga mmoja kwendraaaaa
 
Hiiiii!! Ametekeleza lini?
Hayo yote si ya kweli, Huyu mwanamke anamatatizo kwakweli.
 
Nakuwa nafikiri halima mdee viongozi wake wa juu wa chama hawaangalii anachokifanya na safari hii chadema mkalale kwasababu mnajali manufaa yenu wenyewe
 
Id nyingine ya Jul 5, 2020 nayo inalipwa na Gwajima ili kufanya kampeni mitandaoni. Safari hii mtakojoa dagaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…