Mkuu kwenye vita kuwa na Washirika ni Jambo la kawaida.
Israel kuficha watu wake kwenye mahandaki ni sehemu ya mkakati wa kulinda watu wake na kushinda vita za hapo mashariki ya kati.
Iran ipo kwenye mgogoro na tension kubwa ya kuingia vitani na mataifa ya magharibi kwa kumtumia Israel kwa kipindi kirefu. Haikuona umuhimu wa kuandaa mpango wa kulinda raia wake kwa kuchimba mahandaki?
Haikuona umuhimu wa kutafuta washirika kama China na Urusi ili kujihami na adui zake?
Kuwekewa vikwazo ni sehemu ya kumdhihirishia yeye ni mdogo na anatakiwa afuate mifumo ya wakubwa.
Kama ameamua kufurukuta na kuonyesha naye anamapembe(mkubwa) bila mipango na mikakati sio sababu ya watu kutumia kigezo cha kusema amewekewa vikwazo. Maana mtu atauliza kwa nini Iran asiwawekee vikwazo Magharibi na US akawekewa yeye. Jibu ni kuwa yeye ni mdogo.
Tukijadili kwa mrengo wa Haki, tutakubaliana anaonewa na kufanyiwa dhulma. Hiyo ni kweli.
Lakini Nature inakanuni zake, moja kubwa ni kuwa Nature is heartless, Mother nature has no Mercy.
The bigger Monster eat the little one.
Survival of fittest.
Na nature love the winner and Worship him/her.
Hizo kanuni zinatumiwa na watawala wengi duniani.
Iran mbinu inayotumia unafikiri itatoboa? Kwa upande wangu sioni mbinu anazotumia zikifanya KAZI
Zaidi naona atapigwa chini ya wakati kama ataendelea kurusha ngumi nyingi zisizo na madhara