mkorinto
JF-Expert Member
- Jun 11, 2014
- 31,415
- 38,761
Mambo ya Nyakati wa 2, 18:18-21, inasema
18 Mikaya akasema, Sikieni basi neno la Bwana; Nalimwona Bwana ameketi katika kiti chake cha enzi na jeshi lote la mbinguni wamesimama mkono wake wa kuume na wa kushoto.
19 Bwana akasema, Ni nani atakayemdanganya Ahabu mfalme wa Israeli, ili akwee Ramoth-gileadi akaanguke? Basi huyu akasema hivi; na huyu hivi.
20 Akatoka pepo, akasimama mbele za Bwana, akasema, Mimi nitamdanganya. Bwana akamwambia, Jinsi gani?
21 Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo wa uongo vinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na kudiriki pia; ondoka, ukafanye hivyo.
Hawa waliokuwa na Bwana wako nai walikua dini gani?
Ni wazi hapa mikaya anamfafanulia mfalme juu ya tabiri zote za uongo kutoka kwa manabii 4000,kwamba zinatoka kinywani mwa manabii ambao wamejazwa uongo na pepo,isipokuwa anachomwambia yeye ndio uhalisia wenyewe.
Biblia ni kitabu kizuri sana ila soma kwa utulivu usiresite(kariri)kama kasuku,utauona ukuu wa yaliyomo humo.