Hapa ni wapi? Trafiki wadakwa kwenye video wakichukua Rushwa mara kadhaa

Hapa ni wapi? Trafiki wadakwa kwenye video wakichukua Rushwa mara kadhaa

Hawa vidagaa hawana madhara kama wale wanaochukua mlungula wa kina ADANI ili watwishe Taifa katika mikataba mithili ya kina Dowans.., Yaani kama hawa ni wachawi wale wanakula kabisa nyama za watu...
 
Kwa hiyo unataka rushwa ihalalishwe!!?ati kwa kuwa maisha magumu!!,,na mtoa rushwa inamaana maisha yake si magumu??!,,watu wengine bhana!!
Yani Rushwa imefanywa sehemu ya maisha ya kibongo. Mtu huyo anasomeshea watoto na kulisha familia kwa fedha haramu. Unaoa mtto aliyesomeshwa kwa laana alafu mnakimbilia kwa mwaposa kungoa laana za mababu
 
Japo sipend rushwa ila hii sio njia sahihi sana kuwaadhibisha wahusika..
Kuna maisha baada ya hichi kitu ulicho post.

Tunahangaika na vidagaa tunawaacha mapapa serikalini waokwapua mabilioni ya hela kwenye miradi .
Tena hela ambazo zimekusanywa tayari.. Si bora huyu ni hela ambayo hata haijaingia serikalini..
Umeishia level gani ya elimu mkuu
 
Huyu mama hatumii hata akili kula rushwa.Yaani anapokea waziwazi bila kificho kabisa.Anaona kama ni haki yake kupokea rushwa
 
Wrong is wrong even if everyone is doing it,
Right is right even if no one is doing it,

Unasapoti rushwa halafu ikitokea ajali wakafa watu utamlaumu nani? au utawalaumu hao hao wanaokula rushwa ambao wewe sasa hivi unawasapoti hapa?

Hakuna rushwa ndogo wala kubwa,rushwa ni rushwa,mla rushwa na mtoa rushwa wote ni wakosaji,
Rushwa ndogo ndio hupelekea mtu kupokea rushwa kubwa.
JF kuna watu wanafiki sana. Mtu akileta thread hapa akisema kakamatwa na traffic akaombwa atoe rushwa watatoa povu kulaani huyo askari, leo anafanya hicho hicho kwa daladala watu wale wale wanaona ni kitendo sahihi.
 
Serikali ndio iangalie biashara ya usafirishaji inavyolipa hapo,foleni na za kubrashia viatu lakini bado faida inapatikana,inakuaje brt bus zao zisizotoa za kubrashia viatu na azikai foleni barabarani zinapata hasara!mradi wa brt wapewe watu binafsi
 
JF kuna watu wanafiki sana. Mtu akileta thread hapa akisema kakamatwa na traffic akaombwa atoe rushwa watatoa povu kulaani huyo askari, leo anafanya hicho hicho kwa daladala watu wale wale wanaona ni kitendo sahihi.
Au mtu anakuja kulalamika hapa kua hupati Passport bila rushwa,
Halafu hapa ana support rushwa!
 
Hapa ni wapi, hawa wanajulikana, Kamanda Mulilo, IGP Wambura hapana naona mtaharakisha kutoa press Release kama mfanyofanya kwenye matukio mengine.
Zaidi kongole kwa camera man wa kujitegemea.

View attachment 3202252
Mnashidwa kuhangaika na watu wakubwa mapapa wanaokula billions of money mnahangaika na hawa samaki wadogo ambao ni wazi ujira wao ni mdogo ma maisha yanapanda bei kila kukicha....shame on you.
 
Ukimiliki Ndinga ndio utajua traffic kupokea rushwa si dhambi bali ni msaada kutuokoa na mikononya Serkali sisi tunaojitafuta.
 
Kwa hiyo unataka rushwa ihalalishwe!!?ati kwa kuwa maisha magumu!!,,na mtoa rushwa inamaana maisha yake si magumu??!,,watu wengine bhana!!
Ni halali sio mpaka iandikwe kwenye vitabu.
Sio rushwa iite takrima, ipo kila pahala hiyo kwa hapa Tz.
 
Ajabu ni kwamba hata jamii inaona ni sawa kinachofanyika, kwamba huyu polisi wa barabarani anachofanya ni sawa tu, kumbe haya yanafanyika mahakamani, mashuleni, ofisi za umma zenye kuhitaji watu wapate haki kama tra, nssf. Watu wananyimwa haki zao ila sisi mbumbumbu tunaona it's okay, wale kwa urefu wa kamba zao. Afrika imejaa watu wajinga tu, tupo nyuma sana...
inasikitisha sana,
Nadhani watanzania wengi hata hawajui wanataka nini, inasikitisha sana!
 
Kwa utafiti wangu mdogo kwenye hii thread nimegundua sisi OLD GUARDS ndio tunaona si sawa. Hawa new gen z wanaona sawa na ndio utaratibu mzuri wa maisha.

Wengine wapo huku.
 
Back
Top Bottom