Ila watanzania kwa unafiki hamjambo, kweli mtu anashupaza shingo unaishabikia na kuitetea rushwa? Tuna safari ndefu sana na hii Tanzania.
Rushwa haijalishi ni ndogo au ni kubwa, zote ni rushwa. Kosa ni kosa na hakuna uhalali wa kulifanya kosa hili ni zuri na hili ni baya.
Tulikemea hapa Magufuli aliposema ni ya kufutia viatu, tukaja kukemea tena Samia aliposema wa Serikalini wale urefu wa kamba zao.
Tuna viongozi wanaohamasisha rushwa na vitendo vya kifisadi. Tunaangalia nasisi tunakuwa mashabiki wao, tunatengeneza kizazi gani?
Unajua hiyo rushwa usemayo ndogo, ndiyo inapoteza maisha, kwa kutokagua vyombo vya barabarani, ajali zikitoa mnakimbilia kulaumu.
Tuihalalishe rushwa iwe kisheria kama mmeishabikia hivi, ni aibu sana.