Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi siteseki namkubali sana huyu rais nyie mnaoteseka poleni
| 9) Wakatabahu khadimu, Mimi kijitu fakiri. | (9) This was written by a servant, I’m an unimportant, poor person |
| Jina langu mwalimu, Mbaraka bin Shomari. | My name is Mwalimu, Mbaraka bin Shomari. |
| Nimesifu mwazzimu, Mfalme akhiyari | I’ve praised the Great, the beloved Kaiser — |
| Hapana tena hapana, wewe ndio Kaizari! | There is nobody else. You are the Kaiser! |
| (1) Leo siku ya tatu katika mwezi wa Juni | (1) Today is the third day in the month of June |
| Kazaliwa Bwana wetu King George Sultani | When was born our lord and sultan King George |
| Jamii ya wote shime andameni Mkongeni | Everyone hurry up and proceed to Mkongeni |
| Tukatazame heshima ya maulana King George. | So we see respect paid to His Highness King George |
| (2) King George ni mwana wa King Edward | (2) King George is the son of King Edward |
| Amezaliwa Ulaya nchi ya upande wa kaskazi | He was born in Europe in a country to the north |
| Kama tujuavyo yeye ni pekee asadi17 | As we know he is a special lion |
| Tukatazame heshima ya maulana King George. | So we see respect paid to His Highness King George |
| (3) Watakutana mabwana wakubwa na wadogo | (3) The noble and the lowly will participate |
| Hapazuiwi kijana akuambiaye ni mrongo | No youth will not be denied; whoever tells you otherwise is a liar |
| Wala fujo hapatakuwa ya mafimbo na magongo | Nor will there be disturbances with sticks or clubs |
| Tukatazame heshima ya maulana King George. | So we see respect paid to His Highness King George |
| (4) Siku hiyo ni siku ya furija na anasa18 | (4) This day is a day of celebration and entertainment |
| Atakayejaliwa kwenda furaha hatakosa | Whoever attends will certainly be happy |
| Kwani ni siku ya idi bashasha yatupasa | For it is a holiday and we are expected to be joyful |
| Tukatazame heshima ya maulana King George. | So we see respect paid to His Highness King George |
| (5) Atahudhuria Gavana bwana wa Tanganyika | (5) His Lord the Governor of Tanganyika will attend |
| Siku hiyo mwenye nishani itampasa kupachika | On this day whoever has medals should wear them |
| Asiyekuwa na mwana hata jiwe ataeleka19 | The one without children should carry a stone |
| Tukatazame heshima ya maulana King George. | So we see respect paid to His Highness King George |
| (6) Akina Bwana Askari hupanda wao farasi | (6) The soldiers will mount their horses |
| Mwendo wao taratibu kama mwendo wa papasi | They will pass slowly by, at the speed of a tick |
| Kuwaonyesha raia mambo yasiyo kiasi | To show the citizens extraordinary things |
| Tukatazame heshima ya maulana King George. | So we see respect paid to His Highness King George |
| (7) Tazameni ibura ya Mfalme kuwa Ulaya | (7) Look at this extraordinary celebration for a king who is in Europe |
| Huko mambo mbayana kama amehudhuria20 | There [at Mkongomeni] things will be celebrated as though he were attending |
| Jamaa ukaidi wani mbona mtaangamia21 | What’s the point of being stubborn lest you be destroyed?22 |
| Tukatazame heshima ya maulana King George. | So we see respect paid to His Highness King George |
| (8) Kuna wingi wa Polisi wazuiao hatari | (8) There are many police to prevent danger |
| Wapitisha kwa kiasi zote pia motakari | They only allow selected motorcars to pass |
| Hiyo ndiyo dunia wala nyingine haiwi | That is indeed how the world is. It cannot be otherwise |
| Tukatazame heshima ya maulana King George. | So we see respect paid to His Highness King George |
| (9) Mfalme King George wote mnamjua | (9) Sovereign King George all of you know him |
| Kwa alama za mataji mara utamjua | By the symbol of his crowns you’ll immediately recognize him |
| Na utakapo ya zaidi soma utajua | And if you want to know more, read about him |
| Tukatazame heshima ya maulana King George. | So we see respect paid to His Highness King George |
| (10) King George ana sifa kupenda wake raia | (10) King George is known for liking his subjects |
| Walio bora na hafifu wote twamfurahia | The upper and lower classes we all are happy for him |
| Tumwombee Rabuka huruma amzidishie | Let us pray to God will show more mercy to him |
| Tukatazame heshima ya maulana King George. | So we see respect paid to His Highness King George |
| (11) Sifa hapa zimekoma mwaka huu najaribu | (11) The praises end here, this year I am trying |
| Labda nitapata yangu huwa bahati nasibu | Perhaps I will have my luck |
| Sikukaa nasimama nangoja yangu matulubu23 | I am not sitting, I stand, waiting to get what I expect |
| Tukatazame heshima ya maulana King George. | So we see respect paid to His Highness King George |
| (1) Wenzangu nawahubiri, sikukuu imefika! | (1) My fellows, I’m preaching to you: the birthday is here! |
| Sote tukae tayari, tuadhimishe ushirika! | We should all be ready to celebrate together |
| Wala siyo kukasiri, raia tumefurahika, | And we shouldn’t be angry. We citizens are happy |
| King George mtajika, Mfalme tunayemkiri! | The renowned King George is the king we accept! |
| (2) Tunamtakia heri nyingi, na baraka, | (2) We wish him best wishes and blessings |
| Mfalme mashuhuri, ambaye twamtaka | The famous king, whom we want |
| Atutawale dhahiri, na milele apendeke! | May he rule us well and be forever loved |
| King George mpendeka, mwema mwenye siri! | The beloved King George, good and secretive! |
| (3) Pasiwe na ghururi, Mungu amemsimika, | (3) Let there be no deceit, God has installed him |
| Awali na aheri, hakika ni sikukuu, | From start to finish, truly it is a holiday |
| Leo hakuna shauri, afisi zimefungwa, | Today there’ll be no government work, the offices have closed26 |
| King George hakika ana wengi matajiri! | Truly King George has many rich people! |
| (4) Ni furaha ya fahari, Mfalme anatukuzika! | (4) It is a great joy that the king is praiseworthy |
| Raia na askari, wamejishika pamoja, | The citizens and armed forces are united |
| Tajiri na maskini, huungwa na mamlaka, | The wealthy and the poor are joined by the authority |
| King George amefika, hali ya ujasiri. | King George has reached a state of bravery… |
| (7) Kwa yakini nasadiki, ugonjwa ulivyoshika, | (7) With certainty I believe illness attacked him |
| Mfalme kwa dhahiri, maradhi yalimshika, | The king apparently was overtaken by disease |
| Katibiwa na madaktari, na ugonjwa ukatibika! | He was treated by doctors and his ailment cured |
| King George amevuka, maradhi yaliyokuwa hatari. | King George overcame the dangerous disease. |
| (8) Alipatwa na hatari, sasa ameokoka, | (8) He faced danger but now has been saved |
| Nasi sote kadiri, himaya ilimofika, | And we all are able to accept the extent of his rule |
| Siku zote twamkiri, Mfalme wa mamlaka, | We always accept him as a king with authority |
| King George Afrika, kaitawala dhahiri. | King George has transparently ruled Afrika. |
| (22) Salaam nyingi tayari, nafasi zinapunguka, | (22) Many greetings already. Space is running out |
| Mambo Leo mashuhuri, pokea chakula shika, | Famous Mambo Leo, take the food27 |
| Gazeti letu zuri, busara hukutanika; | Our newspaper is good, wisdom collects here |
| Maulana ajuika, King George dhihiri. | His Highness is famous. King George appear to us! |
| (23) Mtengenezaji habari, Mungu akupe baraka, | (23) News editor, may God bless you |
| Umetutoa kiburi, gizani pia tumetoka; | You removed our arrogance and we came out of the darkness |
| Twakusalimu dhahiri, na wengine kadhalika; | We greet you openly and the others as well |
| Maulana hakika, King George kadiri. | Truly His Highness King George is the able one.28 |
| (24) Kaditamati shairi, kalamu ninaiweka, | (24) I bring the poem to a close and set down my pen |
| Nawaambia kwa dhamiri, Inshalla nikifika, | I’m telling you that my intention, God willing, is to |
| Hoja kuwa na umri, kutunga na kuandika, | continue To compose [poems] and to write as long as I live |
| Kwa heri nasimika, King George wa fahari. | I bid you farewell, King George the Proud. |
MIEHE, Gudrun, Katrin BROMBER, Said KHAMIS, and Ralf GROSSERHODE. Kala Shairi: German East Africa in Swahili Poems. Archiv afrikanistischer Manuskripte, Vol. 6. Köln: Rüdiger Köppe Verlag, 2002.
MIEHE, Gudrun, and Abdilatif ABDALLA. Poems Attributed to Fumo Liyongo. Archivafrikanistischer Manuskripte, Vol. 7. Köln: Rüdiger Köppe Verlag, 2004.
Heri ya kuzaliwa Mheshimiwa Rais na Mama yetu mpendwa. Tunakupenda na tunakutakia maisha marefu yenye furaha, afya tele and hofu ya Mungu ndani yako.Mnamo tarehe 27 Januari 1960 Rais wa Awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Ndg. Samia Suluhu Hassan alizaliwa huko Makundichi Zanzibar.
Leo anatimiza umri wa miaka 62. Ni Rais wa kwanza mwanamke nchini kwetu na mfano wa kuigwa kwa wasichana, wanawake na watu wa rika na jinsia mbalimbali kwa namna moja ama nyingine.
Tunaamini kuwa leo asubuhi 27 Januari 2022 Saa 12:00 Asubuhi - 03:00 Asubuhi kupitia mahojiano maalum katika kipindi cha Jambo Tanzania katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) utakuwa na mengi ya kutueleza yakuhusuyo wewe, maendeleo endelevu ya nchi yetu na mustakabali bora wa nchi yetu pendwa ya Tanzania.
Tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu awe nawe katika uongozi wa awamu ya sita, akujalie afya njema, furaha, maisha marefu na nguvu za kuwatumikia watanzania bila kuchoka wala kukatishwa tamaa katika kuhakikisha taifa hili linapata maendeleo.
Heri ya Kumbukumbu ya Siku ya Kuzaliwa Rais wetu na daima Kazi Iendelee.
View attachment 2096714
View attachment 2096717
Hakurupuki.Ni afadhali tuna mtu ana fanya maamuzi baada ya kutafakari
Mkuu unaishi na maumivu ya nafsi, pole sana. Kumbuka ukikubalika na wengi umekubalika kwa Mungu pia.Fisadi Bwana Chato kupewa salamu za happy birthday haihalalishi fisadi Hangaya kupewa salamu za happy birthday.Two wrongs don't make a right.
Fanya kazi toka jasho kuwa mbunifu ili pato lako liongezeke. Mabilionea wasingekuwa na ukwasi walionao kama wangekuwa na mawazo kama haya ya aliye juu mgojee chini, utagonja mpaka siku ya kwenda kaburini.Na yeye alipe kodi kutoka kwenye mshahara wake, posho zake zipunguzwe pamoja na watawala wenzake, na mishahara yao minono ipunguzwe.
Fanya kazi toka jasho kuwa mbunifu ili pato lako liongezeke. Mabilionea wasingekuwa na ukwasi walionao kama wangekuwa na mawazo kama haya ya aliye juu mgonje chini, utagonja mpaka siku ya kwenda kaburini.Na yeye alipe kodi kutoka kwenye mshahara wake, posho zake zipunguzwe pamoja na watawala wenzake, na mishahara yao minono ipunguzwe.
JPM na Samia wanaunganishwa na CCM tu lakini ni watu wawili tofauti kabisa. Naona unajaribu kujenga hoja lakini inaishia juu juu haina mashiko mazito.Huyu ndiye amekubalika na wengi?!🐒🐒🐒View attachment 2097420View attachment 2097421
Kuongozwa na mwanamke muda ulikuwa haujafika miaka yote ya nyuma na sasa umefika. US wana running mate mwanamke hivyo lolote likimpata Biden mwenye miaka 80 Kamala anakabidhiwa nchi. Kuwa mpole tu.Acha kumpa ujinga Wewe mwanaume na watoto unakubali kuongozwa na mwanamke?
Mmh yale ya kuteua mkurugenzi mpya wa tpdc na kumtumbua usiku wake, sio kukurupukaa huko?Hakurupuki.
Kukurupuka kubaya ni kumtumbua mtu 2015 halafu akaendelea kulipwa mshahara wa serikali akiwa hafanyi kazi mpaka 2020 mwishoni.Mmh yale ya kuteua mkurugenzi mpya wa tpdc na kumtumbua usiku wake, sio kukurupukaa huko?
Au Yale ya wenzake na mbowe wameshtakiwa
Unahisi nimekataa? au unafikiri sasa hivi hakuna hiyo.Kukurupuka kubaya ni kumtumbua mtu 2015 halafu akaendelea kulipwa mshahara wa serikali akiwa hafanyi kazi mpaka 2020 mwishoni.
Bado hawajakamatwa . Upinzani kuteseka imekua ni kitu cha kawaida kwasasa. Lakini nafurahi zaidi samia anavowanyoosha mbogamboga hasa kundi lile[emoji847][emoji847][emoji847]Hivi waliojaribu kumuua Tundu Lissu bado hawajakamatwa?
Nauliza tu jamani ni muda mrefu umepita lakini hakuna taarifa yoyote juu ya kukamatwa kwa wauaji. Jeshi la polisi na vyombo vya ulinzi na usalama mbona mpo kimya imeshindikana?www.jamiiforums.com
Sio mbogamboga tu, hata mwenyekiti mbowe ananyooshwa ni miezi mitano sasa yupo jela kwa kesi ya kubumba.Bado hawajakamatwa . Upinzani kuteseka imekua ni kitu cha kawaida kwasasa. Lakini nafurahi zaidi samia anavowanyoosha mbogamboga hasa kundi lile[emoji847][emoji847][emoji847]
Nina kadi ya chadema ya 2004.Tumia akili zako ulizopewa na Mungu bure kufikiria sawasawa.
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Mbowe hajaanza kukaa jela utawala huu au unajifanya hukumbuki? Hukuona kesi zilikua za kubumba? Pelekeni unafki hukoSio mbogamboga tu, hata mwenyekiti mbowe ananyooshwa ni miezi mitano sasa yupo jela kwa kesi ya kubumba.