Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Unaambiwa harmonize alimpigia simu mpaka mwakyembe ambaye kwa wakati huo ndio waziri wa sanaa, lakini yule mnyakyusa naye alikuwa chawa hakutaka kumsikiliza harmonize
Si mchezo.
 
Muimbaji Harmonize amedai kuwa mabosi wa WCB walimtuhumu baba yake kwa kumroga Diamond.

Harmonize alikuwa akizungumzia sababu za kujiondoa kwenye record label ya WCB kwenye kiwanda kidogo nchini Tanzania baada ya kuwasili kutoka katika ziara yake ya hivi karibuni nchini Marekani.

Katika video aliyoitoa Simulizina Sauti kwenye Instagram, Harmonize alisema baba yake alitendewa vibaya kwa uchaguzi wake wa mavazi, kitu ambacho hawezi kubadilisha;

"Siwezi kumbadilisha baba yangu, ana haki ya kunitembelea wakati wowote, alipokuwa akinitembelea nyumbani walikuwa wakidai kuwa amekuja kumroga Diamond, niliwauliza kwa hiyo baba yangu asitembelee? baba ni mtu wa dini hatakiwi kuja nyumbani kwangu?' Je, ina maana?"

Alisema hawezi kumzuia babake kuvaa vazi lake la Kiislamu na kuongeza kuwa hiyo ni njia mojawapo waliyotumia kumtoa nje kwa nguvu.

"Yeye ndiye sababu ya mimi kuwa Harmonize leo. Walikuwa wanatafuta sababu zote za kwanini niache lebo."

Harmonize pia alifichua kuagizwa kulipa faini ya KSh 560k kwa kufanya kolabo na Benki ya Reekado ya Nigeria.

1637336895961.jpg
 
Diamond anatakiwa ayatolee ufafanuz haya malalamiko , Harmonize anamtuhumu Diamond kwamba kuna watu anawatuma wamchafue notable Baba levo na Juma lokole , ili kumharibu kimziki yes yawezekana ni kweli , Ila harmonize haangalii Kwa upande wake kuwa na yeye ana chawa akina mwijaku , carlmastory, hbaba , jaymaudaku na wengine weng na wao kazi Yao ni kumwandama diamond , lakini pia Wasafi wakiandaa event yeye harmonize na yeye anaandaa ili kudivert attention ... Means na yeye anaishi na kuamini humo humo kwenye Fitina na figisu , anamponda mond kwa madhaifu yake hata hvyo bado anamtegemea mond indirect ili awin, ...... Tatizo linakuja hafikii peak Ile anayotaka sababu mwenzake kaenda mile nyingi mbele na ana nguvu nyingi zaidi ndo chanzo cha malalamiko hayo yote.

Turudi Kwa Maghufuli , mtoa mada kuna kitu umekiruka au umekificha Kwa maksudi ili
ujumbe wako wenye utata na kisiasa ufike , mpak kusema Jiwe alimbembeleza Diamond kitu ambacho Kwa Maelezo ya harmonize sio kweli ...

Harmonize anadai alifanya kila njia kuwaomba watu wenye nguvu ya kimaamuz ili wamsaidie azma yake ya kuvunja mkataba , kwani by that time kwake ilikuwa ni ngumu hata kumfikia Diamond Kwa jinsi mambo yalivyokuwa yana-turn around...

Aliwafikia watu kama kusaga ( sababu ya status yake na ushkaji na mond ), alimfikia mama dangote (nguvu ya mama) alimfikia mwenyekiti sjui ndo katibu wa Basata, na alimfikia mwakiyembe ( by that time Wazir wa Sanaa ) , Kwa Maelezo yake anadai wote hawakuonyesha kumsaidia na inaonekana hawakuwa tayar , huku akiandamwa na pressure toka Kwa wadhamini wake CRDB na Sayona , Kondeboy aliona kete Yake ya mwisho ni Raisi John Pombe Joseph Maghufuli....

Jiwe alifanya sehemu yake Kwa kumpigia simu Wazir wa Sanaa na michezo kuhusu hlo sakata,na nafk Mwakiyembe alikuwa aware na hyo changamoto thus why alifanya maamuz ya haraka , kumzuia diamond kukwea pipa mpak amalize hlo suala ...

Kwa hyo Siyo kwamba Maghufuli alimbembeleza Diamond ...na kama ingekuwa hvyo ingechukua sku mbili au tatu ...

Zaidi ya yote Kongole Kwa Harmonize Kwa upambanaji na roho ya kiume , kuhusu Fitina hata yeye hzo Fitina anazifanya , ushindi wake sio wa haraka kama anavyofkria sababu mwenzake still bado ni ngome imara ...!!
 
Nionavyo elimu inamnyima mwanga Harmonize na sijui kwa nini management yake haimshauri.

Hivi ni kweli alichoandika Diamond kilitosha kumfanya Harmonize afikie hasira anazodai kuwa nazo?

Tukubali yote ni sawa, kulikuwa na sababu gani ya kumuingiza Rayvanny na Kusaga katika issue za Diamond?

Hivi 40% katika record label ni ndogo? Umewahi kufikiri idadi ya watu waliopo nyuma ya hiyo 60%

Ili tumumjani alipaswa athibitishe mikataba ya record label yake inatoa ngapi?

Katika vita jana ndio ametumia silaha ya mwisho wakati vita haijapamba Moto. Kilichobaki tumuombee tuu.
Umeongea ukweli dogo hajakomaa kwenye uwanja wa medani tumuombee tu kashajionesha ni mtu wa aina gani watu wataanza kumkwepa na kuwa royal fans wao hawalioni hili, nahisi hata management yake imekosa weledi.

Kuhusu uswahili wa Diamond ndio asili yetu Watanzania yeye harmonaize angekausha tu haku akimlia timing mbona angemuangusha maana tayari mtaji alikuwa nazo lakini kwa hizi mbinu mission fail
 
Sasa si mpaka wakubali kusaini sasa .
Unagoma vipi kusaini kama kipengele cha kuvunja mkataba kipo na mtu kafikia kidau husika?

Mfano mimi ninaifanyia kazi jf kimkataba, ila kuna kipengele tumeweka nikitaka niachane nao, niwalipe milioni 10, sasa nayoa 10M kisha wanagoma, wanaanzaje?

Angewaburuza mahakamani tu kama ni kweli au la basi huo mkataba ulikuwa huna higho kipengele.
 
Naomba kuweka wazi kabisa kwamba mimi si mpenzi wa Muziki wa Tanzania na wala siwapendi wanamuziki wa Tanzania , hii ni kwa vile wamekuwa mara zote wakitumika na ccm kuwapotosha
Aibusana, ilanilisikia akisema rais alimpigia cm mwakymbe iliawazuie air potrt wasisafiri mbaka wasaini kuvunja mkataba. Hapo ilitoka amri hakukua na ubembelezaji.
 
Unagoma vipi kusaini kama kipengele cha kuvunja mkataba kipo na mtu kafikia kidau husika?

Mfano mimi ninaifanyia kazi jf kimkataba, ila kuna kipengele tumeweka nikitaka niachane nao, niwalipe milioni 10, sasa nayoa 10M kisha wanagoma, wanaanzaje?

Angewaburuza mahakamani tu kama ni kweli au la basi huo mkataba ulikuwa huna higho kipengele.
walilipwa kila walichostahili kwenye mkataba wao , lakini kuna hili HUNIWEZI KISERIKALI , HUNIWEZI KIFEDHA NA HUNIWEZI KIUCHAWI
 
Naomba kuweka wazi kabisa kwamba mimi si mpenzi wa Muziki wa Tanzania na wala siwapendi wanamuziki wa Tanzania , hii ni kwa vile wamekuwa mara zote wakitumika na ccm kuwapotosha wananchi , na hasa hawa wanaoitwa Wanamuziki wa kizazi kipya
MMimi hwa sipendi hata kuyasikia takataka tupu
 
Back
Top Bottom