Harusi ya Majizzo, Millard Ayo: Vijana matajiri hawapendi kuchezea pesa zao wala kusumbua watu na michango

Tatizo lenu mnaishi kwa kuwaza au kuogopa eti "Watu watanionaje"

Mtu anaingia gharama kisa kuogopa kusemwa na watu! Huwezi kuwaridhisha binadamu,vijana mna kazi sana,

Live the life u love,love the life u live.
Mstari wa mwisho uwekewe lamination.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka had machozi, khaaah
 
Wengi mnaongea tu hapa kufurahisha genGe ila mkiwa wenyewe huko hela zinawatoka mnachanga sana tu mnakuja kutolea machungu huku
Kabisaaa yaan [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Harusi zina kamati...ndo zinachangisha...wanaoana unaweza kuta hawana hata mbwembwe
Nipo added kwenye group la mchango wa harusi na aliyeniadd ni bwana harusi. Na huyo huyo ndio mshereheshaji na mshawishi mkuu kwenye hilo group watu watoe michango.

Nilichofanya kwavile namuheshimu jamaa nikaamua ku-mute group waendelee na harambee zao wenyewe.
 
Hivi Millard ni kweli alioa, mbna ilisemekana ni tangazo lile? Duuh bas hongera zake.

Kuoa ni swala binafsi na watu wake wa karibu,, familia yake na familia ya bibi harusi.

Kwa record za msajili wa ndoa Tanzania rita Millard ayo ana mke halali kabisa aliyefunga nae ndoa ya kikatoliki kanisani

Mambo ya tangazo ama sio Tangazo hayo siyajui
 
Mimi nilitaka kufanyiwa tena na mama zangu wadogo baki ,ila niligoma zote form four ambayo niikuwa na ndugu yangu nasoma nae darasa moja siku ya graduation sisi tulikuwa kweny tuition tunafanya practical.

Zote form six mpaka chuo niligomea na niliwachenga mpaka trh ya graduation ..
 
Bas sawaa.
 
Nikiona mwanaume anashoboka na mambo ya sherehe sijui naonaje ..
Mambo mengine kuleta wasiwasi mtu mpaka sherehe ipite kakonda kwa kuwazia shughuli itaendaje?

Kistaarabu kanisani au msikitini pale tena fasta na wala viongozi wa dini hawachukui pesa nyingi kama mna pesa andaeni hata karamu kwa watoto yatima au kutoa msaada ...Sasa mnaanza kupiga kelele kwa miziki baadae kuna vitu vinapotea mnalipa , mara walevi wamepigana ..Mambo kibao ya hovyo.

Millardayo ,Majizzo hata Mengi sio kwamba ni matajiri hawa watu ni wastaarabu ndio maan hawapendi vurugu..
 
Ni vijana matajiri na maarufu nchi nzima wanajulikana. Ndio maana wametolewa mfano.

Unaweza ukawa wewe ni kijana tajiri ila sio maarufu. Hivyo jina lako likitumika kwwnye mfano watu wanashindwa kuelewa...maana hawakujui kwa chochote
Kama utajiri ni kumiliki radiostation and online tv; basi mimi ni bilionea
 
Pole mkuu. Mi waliniunga group la harusi simjui ata member mmoja wala bwana harusi.

Nikaahidi nitatoa laki 5 hafu nikaleft. Nilitafutwa aisee ova sio SMS sio kupigiwa. Akijitambulisha tu anakula block.
Haha safi . Hii ilinitokea wakati ndo nimemliza shule za juu juu , jamaa etu anajua kabisa sisi bado apeche alolo katuweka kwenye kamati eti tuanze kuahidi nyie mnaita kupledge sijui mi nikawambia Mr Emmanuel andikeni laki nne .. yule jamaa angu akanifata inbox et kua serious mwanangu. Nikamwambia serious uanze kuwa wewe , Katibu wa ile kamati alikua ni mdada mmama majibu niliyokuwa nampa aliona bora aachane na mimi tu na kejeli nyingi kwamba unaahidi halafu kumbe masikini tu. Nikamjibu masikini baba ako
 
Nashkuru Mungu
Huu ujinga wa michango ya hovyo ilishakataliwa kwny ukoo wetu tangu nakua Hadi hivi sasa

Harusi ya mwanafamilia yeyote itagharamiwa full na Wana ukoo wote kwa kushangishana sisi kwa sisi, sio Watu wa nje.

Labda wale wa hiari yao
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mtoa post upo sahihi sanaaaa.kuna jamaa yangu alifungaaa ndoa ya milion 35+ chaa ajabu week mojaa anasema oyaaa nikopeshe ten thousand...hivi hizi n akil au ufalaaa ..hapaaa nina kadi 3 za 30k single nachanga mojaa tuu...
 
safi sana , ndoa ni muunganiko wa kiroho baina ya nafsi mbili. Haya mengine kanisani , Msikitini ni mbwembwe tu, hakuna kwenye bible kasisi kafungisha ndoa

Watu walikuwa wanapatana tu na mzazi au wenyewe , tayari ndoa

Ila kufanya sherehe sio mbaya ,lakini usikele watu kwa michango
 
Akili za KIMASIKINI huwa ni KUKARIRI yasiyo ya maana ,kubweteka na kufurahisha jamii.....

#Jiamini Mwenyewe

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…