Hata kama Rais Samia haumkubali, si sahihi kumpuuza na kumwandikia jumbe zisizo na staha

Gesi ya mtwara haijauzwa huo ni uongo wa hali ya juu sana,pia wantukane ama wasimtukane samia ni mtu makini sana anaiendesha nchi kwa kufuata misingi ya utawala bora

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Hata mbowe ni baba na ana watoto na kiongozi wa chama kikuu cha upinzani kumpa tuuma za kubumba cio sawa
 
😍
 
Na Mbowe ana watoto na família kiujumla inamhitaji yeye sio aonewe kwasababu ya mitazamo tofauti na watawala.

Huyo Samia atakachokipanda ndicho atakachovuna na atakejeliwa bila ya kuangalia sura yake.
Hivi sura yake inaweza kumfanya mkosoaji aghairi kukosoa eeh!?
 
Uzi wako unalenga kumtweza mama. Unajifanya unakemea maovu.
 
Mie naona sawa tu.Wewe hujui au huoni bei ya gesi au wewe kwako ipo tu inamwagika kama maji ya chemchemi kwa kutumia kodi zetu.Wengi wanaotumia kodi zetu wako kama wewe kwa sababu wanaagiza tu, peleka haraka gesi nyumbani sasa hivi na hiyo invoice mpelekee mhasibu alipe.Nakwaambieni nchi hii kuna watu wanateseka sana.
Mtoa mada hyo 'nb' yako si matusi kwa utawala mzima..au wewe unaona iko sawa?
 
Kwani wewe mmachinga!? Maumivu yetu huyajui, usiropoke.
 
Wazalendo wanapaswa kuangalia maslahi ya nchi na sio mapenzi kwa watu binafsi.
 
Pamoja na yote, nadhani watu wanao mzunguka Rais SSH nao ni wachumia tumbo tu! Hawamshauri vizuri Rais wetu, wanayashauri vizuri matumbo yao tu!
 
Wazalendo wanapaswa kuangalia maslahi ya nchi na sio mapenzi kwa watu binafsi.
Sawa kabisa lakini mapenzi yao yawe binafsi kweli kweli wasiingilie maslahi ya nchi yetu! Sasa yule Rais aliyetuingiza kwenye janga kubwa la ufisadi anafanya nini ikulu yetu!?
 
Rais ni wa Jamuhuri ya Tanzania, ukiona mtu anashindwa kuwa na staha, huyo hafai kwa jua wala kwa mwezi...Mtu yeyote anayejitambua lazima aheshimu mamlaka iliyo juu yake kwakua mamlaka zote zinatoka kwa Mungu, haina maana uwe passive, but unatoa maoni yako kwa staha na utulivu.

Kutoa maoni ni haki ya kikatiba kama ilivyo kuheshimu viongozi wote wanaotambuliwa na hiyo katiba.
 
Matatizo yote ya nchi umsifie kiongozi utakuwa zuzu
Kumstahi na kumpa heshima yake kunahusiana vipi na kueleza tatizo liko wapi? Au unaona ukieleza tatizo pasipo kumkosea heshima hatasikia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…