Hatari ya kuwalazimisha watoto wa Watu kwenda JKT!

Hatari ya kuwalazimisha watoto wa Watu kwenda JKT!

Leo nimeona mkeka wa wahitimu wa kidato cha sita wapatao 60,000 ambao wamelazimishwa kwenda JKT kwa lazima kw
... HAKUNA KIJANA ANALAZIMISHWA KWENDA JKT BALI JKT INATOA FURSA KWA VIJANA KUHUDUMIA KWA MUDA MFUPI UNAOTOLEWA!
... MTOTO WAKO AKIWA ANAJITAMBUA NA KUJISIMAMIA HAKUNA ATAKAYEMTENDEA KINYUME NA SHERIA!
 
Dangote kaleta Cement nyingi sana na ukiangalia tuna uhaba wa Tofali ....warete warete wajomba....Mng'ao huo maamae.

Shambani nako naona si haba..... Jembe zipo za kumwaga
Mnawachelewesha BBT shati inapepea mwendo mkali mnoo.
 
tooooooookaaaa kuliaaaaaaaaaaaaa
mistareeeeeeeee fungua
up

mastareeeeee mbele nyosha, kati na mwisho

tuliaaaaaaaa tuliaaaaaaa tuliaaaaaa

macho mbeleeeeee up

afande mgeni rasmi waliopo mbele ni vijana 60, service man na service gelo nipo tyr kwa ukaguzi afande mgeni rasmi.
 
tooooooookaaaa kuliaaaaaaaaaaaaa
mistareeeeeeeee fungua
up

mastareeeeee mbele nyosha, kati na mwisho

tuliaaaaaaaa tuliaaaaaaa tuliaaaaaa

macho mbeleeeeee up

afande mgeni rasmi waliopo mbele ni vijana 60, service man na service gelo nipo tyr kwa ukaguzi afande mgeni rasmi.
Hivi wewe 🤣🤣
 
Leo nimeona mkeka wa wahitimu wa kidato cha sita wapatao 60,000 ambao wamelazimishwa kwenda JKT kwa lazima kwenye makambi mbalimbali waliyopangiwa kuripoti kuanzia tarehe 01.07.2026. Huyu mtu aliyelazimisha kutungwa sheria ya wanafunzi wa kidato cha sita kwenda JKT kwa lazima ni mwendawazimu. Hivi anafahamu kweli matatizo ambayo wanafunzi hawa wanapitia wawapo huko kwenye makambi ya mateso?

Ingependeza kama wanasiasa wanaolazimisha watoto wa makabwela kwenda kuteseka kwenye makambi ya jasho na damu nao watoto wao wangepelekwa huko wakateseke. Hawa wapuuzi watoto wao wapo Oysterbay, Msasani na Masaki wanakula bata huku watoto wa wenzao wanateseka kwenye makambi ya mateso. Inauma na inasikitisha sana. Hivi ni lini hawa wachumiatumbo wataacha kuwatesa watoto wa walalahoi? Kuwalazimisha watoto wa maskini kwenda JKT sio tu kunasababisha mateso kwa watoto bali pia kunaongeza gharama zisizokuwa za lazima kwa wazazi maskini ambao wamejikamua hadi senti ya mwisho kuwasomesha watoto wao.

Kibaya zaidi, yapo malalamiko kwamba baadhi ya makambi haya yamekuwa yakihusishwa na vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto wa kike. Wapo wazazi wanaohofia usalama wa watoto wao kutokana na madai ya mimba na maambukizi ya HIV magonjwa yanayoripotiwa kutokea kwa baadhi ya wahusika waliopita kwenye mazingira hayo

Kuna wakati Tunasingizia maprofesa wa vyuo vikuu kuwajaza mimba na UKIMWI watoto wa kike na kuwapa digrii bure bilashi. Lakini kuna madai Watoto hawa huathirika pindi wanapokuwa kwenye makambi y. Natoa wito kwa wazazi kuwazuia watoto wao wasiende kutwezwa kwenye haya makambi ya kijanjaweed na yasiyokuwa na adabu hata kidogo. Mzazi chukua hatua; mlinde mwanao dhidi ya utwezwaji!

Binafsi siungi mkono hoja yako kwani
Jeshini ni mahala salama kabisa (achana na story za kijiweni mnazo danganyana)
Jeshi hasa la sasa lipo very organized na professional, uliza sisi tulioenda miaka ya hivi karibuni.
Lakini pia, kizazi hiki kimejaa wimbi kubwa la wazazi wanaolea watoto kwa tamthilia ndio sababu wahitimu wengi wanaishia kwenye kubeti na kamari na kuwa mzigo kwa wazazi kwa kwa jamii nzima.
Leo hii wapo watoto/vijana hawajui kufua, kulima, hata kujitegemea mambo madogo madogo hawawezi na wamemaliza form six....wanafikiri maishi ni kuishi kwa remote....na ndio hao wa get rich soon....kila nafasi wanayopewa wanawazia kuiba, kutotenda haki, kuchepusha ili tu watajirike; hawana uzalendo.....

Natamani muda wa jeshi uongezwe na kufikia walau mwaka kama zamani (China wao ni miaka miwili)
na hii ingewajenga watoto (vijana) wawe tayari kupambana na maisha yajayo badala ya kuwa mzigo kwa wazazi.... MTOTO YEYOTE MWENYE CHANGAMOTO YA KIAFYA, ANAKWENDA NA CHETI CHA DACTARI NA KINAZINGATIWA. Acheni kudanganyana/ acheni kuamini porojo za kijiweni!!!
VIJANA WALIOHUDHURIA JESHINI NI FAIDA KWA MZAZI, KWA JAMII NA KWA TAIFA!!!
 
Huo "uzalendo" unaousifika huko jeshini ndio huo ulioonekana October 29 na kuendelea au kuna mwingine! 🤔
Hata mimi najiuliza swali hilo hilo mkuu. Kama JKT ndiko uzalendo unakojengwa mbona mafisadi wote wanaotusumbua nchi hii wamepita huko? Huo uzalendo waliovuna huko uko wapi? JKT ni mahali pa ovyo. Usimruhusu mwanao kamwe kwenda kuteswa na kutwezwa huko kwenye makambi ya mateso.
 
JKT ina faida sana kwa hiki kizazi,hiki kizazi kina mapungufu mengi aisee
Mimba na UKIMWI ni faida mkuu? Kama hiyo ni faida basi mpeleke huko mwanao au dada yako akajazwe mimba na kuambukizwa UKIMWI. Usitulazimishe.
 
Mtu hajifunzi uzalendo kwa miezi mitatu.

MTU hujifunza uzalendo kutoka
a) Familia yake (wazazi na walezi)
b) Shuleni
c) jamii yake
d) Viongozi wake

Kama hiyo listi hapo juu kuna mafisadi, wachumia tumbo, wabinafsi, wenye dhulma.

Huyo mtoto hata akae huko jeshini miaka 10 hawezi kuwa mzalendo
Uzalendo ni kisingizio kinachotumiwa na CCM kuwatweza watoto wa walalahoi kwenye makambi yao haya ya kijanjaweed.
 
Basi lalamikia misconduct ya military trainers!

Otherwise, JKT ni taasisi muhimu inayowapa vijana wengi exposure ya maisha halisi ya Mtanzania. If you didn’t know, kuna watoto mayai ambao bila kwenda JKT wanakuwa hawajui chochote kuhusu maisha ya Mtanzania wa kawaida. Such kind of kids take everything for granted!
Una hakika kwamba hayo "mazuri" wanayoyapata huko JKT hawawezi kuyapata sehemu nyingine mkuu? Can you substantiate your claims?
 
Imagine toto umeliona linatingisha alafu wewe ni mkufunzi alafu ni binadamu unahsia utafanyaje kama ni wewe?
Ndio maana nasisitiza kwamba hii JKT ni upuuzi mtupu, haina tija yoyote kwa vijana wa taifa hili mkuu.
 
Back
Top Bottom