Hatari ya kuwalazimisha watoto wa Watu kwenda JKT!

Hatari ya kuwalazimisha watoto wa Watu kwenda JKT!

Mzee wa fisihi nimekuelewa mno.. JKT imetoa mazao mazuri sana kwenye sekta nyingi, huoni kama ni jambo jema..?

Wapo wajinga ambao wamekuwa samaki wakavu hawakunjiki tena jeshi linajitahidi kuwamwagia maji na kuwapinda hivyohivyo..

Tulipongeze jeshi letu kwa mazuri yake
Mkuu mafisadi wote wanaoutusumbua hapa nchini wamepita JKT. Ina maana wao hawakukunjika huko (kama unavyotoa mfano wa samaki) ili wawe viongozi wazalendo?
 
Mtu hajifunzi uzalendo kwa miezi mitatu.

MTU hujifunza uzalendo kutoka
a) Familia yake (wazazi na walezi)
b) Shuleni
c) jamii yake
d) Viongozi wake

Kama hiyo listi hapo juu kuna mafisadi, wachumia tumbo, wabinafsi, wenye dhulma.

Huyo mtoto hata akae huko jeshini miaka 10 hawezi kuwa mzalendo
Haswaaa
 
Gentleman,
ni vizuri zaidi vijana wote wanaohitimu masomo ya sekondari waende kupata mafunzo ya ukakamavu, utii, uzalendo, utayari na stadi za maisha katika makambi ya Jeshi la Kujenga Taifa, ili hatimae tuwe na vijana wenye moyo wa kulijenga taifa lao kwa kufanya kazi kwa bidii na kujitegemea.

hakuna haja ya upotoshaji useless hata kidogo kwenye hili. Ni vizuri kua wakweli na itapendeza zaidi 🐒
Mkuu mafisadi wote wanaotamba ktk nchi hii wamepita JKT. Mbona hawana uzalendo, utii na faida kwa taifa? Nani kakwambia JKT ni chuo cha uzalendo na kwamba mtu anaweza kuwa mzalendo kwa kuteswa kwenye makambi haya ya kishetani kwa miezi 3 tu?
 
Basi lalamikia misconduct ya military trainers!

Otherwise, JKT ni taasisi muhimu inayowapa vijana wengi exposure ya maisha halisi ya Mtanzania. If you didn’t know, kuna watoto mayai ambao bila kwenda JKT wanakuwa hawajui chochote kuhusu maisha ya Mtanzania wa kawaida. Such kind of kids take everything for granted!
Huu ni uongo mtupuu, wala hakuna ukweli wowote.
 
Mkuu mafisadi wote wanaotamba ktk nchi hii wamepita JKT. Mbona hawana uzalendo, utii na faida kwa taifa? Nani kakwambia JKT ni chuo cha uzalendo na kwamba mtu anaweza kuwa mzalendo kwa kuteswa kwenye makambi haya ya kishetani kwa miezi 3 tu?
acha upotoshaji gentleman,
mafunzo ya stadi za maisha, ukakamavu, uadilifu, uzalendo na kujitegemea sio mateso please.

uvivu wako ndio umaskini wako, acha dhana potofu na visingizio nonsense dhidi ya viongozi na watumishi wa umma nchini 🐒
 
Hayo Eleza wewe, mm nimejadili kua JKT hakuna unyanyasaji wa kijinsia kama anavyo dai mleta mada, na hakuna UKIMWI wala uharibifu kama inavyo daiwa.

Tulipita tukayaona tukayaishi, walio kuja na bk waliondoka nazo, Walio amua kutoa K walifanya kwa mapenzi yao wenyewe.
Uongoo wengi wao wanalazimishwaa.
 
JKT haina mambo mabaya kama alivyosema mwandishi. Kama unalitoto umelilea bila adabu huko linaweza fundishwa kwa kiasi chake.

Kama mtoto wako katoka 6 na unaona muda wa kusubiri kwenda chuo hana cha kufanya mruhusu aende kule.

Lakini naweza kusema JKT haina faida yeyote baada ya mtu kutoka kule,hakuna cha kujivunia na hauta apply popote.
 
JKT faida yake labda iajiri vijana
Au iweke mfumo wa kuwasaidia vijana kuwapa mifumo ya miradi huku ikiwasimamia.

Itakuwa na tija lakini tofauti na hapo NI kupotezea muda vijana, na kutumia muda wao kwa ishu Ambazo haziwasaidii

Wapo vijana wametoka JKT wengine waliahidiwa ajira za JW wapowapo huku mitaani wanambwela mbwela.

Hawana tofauti na wale ambao hawakwenda jeshini. Yaani sio kwa ujuzi wala kwa mafunzo ya kikakamavu.

Kama kweli ipo Nia ya dhati kusaidia hawa vijana maskini. Ni Bora waweke mifumo yakueleweka.
Sio vijana wapoteze muda bure. Badala ya kukaa na wazazi wao wamalizie likizo na utoto wao.

JKT ifungue scheme kubwa nyingi, scheme za kilimo, ufugaji, utengenezaji wa bidhaa au viwanda vidogo vidogo, n.k.

Iwasimamie vijana, makundi makundi, vijana wapate kazi. Na soko ndni ya nchi lipo. Nje ya nchi watumie njia za kidiplomasia au zile za uvamizi
Mkuu Taikon umemaliza kila kitu. JKT haina faida yoyote kwa vijana zaidi ya kuwapotezea muda na kuwasababishia mzongo wa mawazo na pia kuwaingiza wazazi kwenye gharama zisizokuwa na tija.
 
Unalalamika kuhusu wabunge wakati kioindi wanapitisha hyo sheria wao ndo walikua wakwanza, Akina zito walienda JKT kipi kipya sasa?
Kwa hiyo hoja ikipitshwa na Zitto, hata ikiwa ya kipuuzi, lazima tuikubali tu mkuu?
 
Mtoto wangu asipoenda watamfanyia nini ?
Watamnyima nafasi ya kwenda Chuo Kikuu na kumuwekea mizengwe
Daaah umenikumbusha mbali sana Mwaka 2017 nikiwa Bulombora JKT "B" Coy.

Nilienda mzima kabisa nimetoka huko naumwa Mgongo, Nashukuru Mungu nilikujaga kupona mwaka 2022, takribani miaka 5 baadae baada ya kutoka huko.

Ilikuwa mjibu wa sheria Operation Tanzania ya Viwanda kama sijakosea.
Kaka yangu alienda JKT akaangukia kwenye kambi ya mateso inayojihusisha na kilimo cha mpunga. Kwa bahati mbaya alijikata mguu na jembe wakati anaandaa jaruba la mpunga. Hicho kidonda kiliendelea kukua na kumtesa bila kutibiwa hadi kikageuka kuwa kidonda ndugu. Alikuja kuponeshwa na daktari bingwa kwa gharama kubwa baada ya kuhitimu mateso. Hata hivyo, baada ya kidonda kukauka, kimeacha kovu kubwa sana mguuni ambalo linamtesa kwa ganzi hadi leo. JKT ni makambi ya mateso kama yalivyo makambi ya Gwantanamo na makambi mengine ya mateso.
 
Leo nimeona mkeka wa wahitimu wa kidato cha sita wapatao 60,000 ambao wamelazimishwa kwenda JKT kwa lazima kwenye makambi mbalimbali waliyopangiwa kuripoti kuanzia tarehe 01.07.2026. Huyu mtu aliyelazimisha kutungwa sheria ya wanafunzi wa kidato cha sita kwenda JKT kwa lazima ni mwendawazimu. Hivi anafahamu kweli matatizo ambayo wanafunzi hawa wanapitia wawapo huko kwenye makambi ya mateso?

Ingependeza kama wanasiasa wanaolazimisha watoto wa makabwela kwenda kuteseka kwenye makambi ya jasho na damu nao watoto wao wangepelekwa huko wakateseke. Hawa wapuuzi watoto wao wapo Oysterbay, Msasani na Masaki wanakula bata huku watoto wa wenzao wanateseka kwenye makambi ya mateso. Inauma na inasikitisha sana. Hivi ni lini hawa wachumiatumbo wataacha kuwatesa watoto wa walalahoi? Kuwalazimisha watoto wa maskini kwenda JKT sio tu kunasababisha mateso kwa watoto bali pia kunaongeza gharama zisizokuwa za lazima kwa wazazi maskini ambao wamejikamua hadi senti ya mwisho kuwasomesha watoto wao.

Kibaya zaidi, yapo malalamiko kwamba baadhi ya makambi haya yamekuwa yakihusishwa na vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto wa kike. Wapo wazazi wanaohofia usalama wa watoto wao kutokana na madai ya mimba na maambukizi ya HIV magonjwa yanayoripotiwa kutokea kwa baadhi ya wahusika waliopita kwenye mazingira hayo

Kuna wakati tunasingizia maprofesa wa vyuo vikuu kuwajaza mimba na UKIMWI watoto wa kike na kuwapa digrii bure bilashi. Lakini kuna madai Watoto hawa huathirika pindi wanapokuwa kwenye makambi haya ya mateso. Natoa wito kwa wazazi kuwazuia watoto wao wasiende kutwezwa kwenye haya makambi ya kijanjaweed na yasiyokuwa na adabu hata kidogo. Mzazi chukua hatua; mlinde mwanao dhidi ya utwezwaji!
​
Hii mimi sikubaliani nayo kabisa
 
Si bora huku ni wahitimu wa kidato cha 6 tu nchi nyingine ni kwa kila raia ni lazima kupata mafunzo ya kijeshi bila kujali na ukithubutu kukwepa jera inakuhusu.
Katika nchi yenye mamilioni ya raia, kuwachukua wahitimu wa kidato cha sita tu kunaleta manufaa au tija gani mkuu?
 
Wewe ndiye ulipaswa kutueleza mbadala wake ambao ni better, lakini uliishia katika kulalamika tu!
Mimi nimeeleza mabaya ya JKT. Sasa wewe unayeshupaa kuwa JKT kuna "faida nyingi sana", hebu tutajie walau faida mbili zenye mashiko za kuhudhuria JKT.
 
Back
Top Bottom