Hatari ya kuwalazimisha watoto wa Watu kwenda JKT!

Leo nimeona mkeka wa wahitimu wa kidato cha sita wapatao 60,000 ambao wamelazimishwa kwenda JKT kwa lazima kw
... HAKUNA KIJANA ANALAZIMISHWA KWENDA JKT BALI JKT INATOA FURSA KWA VIJANA KUHUDUMIA KWA MUDA MFUPI UNAOTOLEWA!
... MTOTO WAKO AKIWA ANAJITAMBUA NA KUJISIMAMIA HAKUNA ATAKAYEMTENDEA KINYUME NA SHERIA!
 
Dangote kaleta Cement nyingi sana na ukiangalia tuna uhaba wa Tofali ....warete warete wajomba....Mng'ao huo maamae.

Shambani nako naona si haba..... Jembe zipo za kumwaga
Mnawachelewesha BBT shati inapepea mwendo mkali mnoo.
 
tooooooookaaaa kuliaaaaaaaaaaaaa
mistareeeeeeeee fungua
up

mastareeeeee mbele nyosha, kati na mwisho

tuliaaaaaaaa tuliaaaaaaa tuliaaaaaa

macho mbeleeeeee up

afande mgeni rasmi waliopo mbele ni vijana 60, service man na service gelo nipo tyr kwa ukaguzi afande mgeni rasmi.
 
Hivi wewe 🤣🤣
 

Binafsi siungi mkono hoja yako kwani
Jeshini ni mahala salama kabisa (achana na story za kijiweni mnazo danganyana)
Jeshi hasa la sasa lipo very organized na professional, uliza sisi tulioenda miaka ya hivi karibuni.
Lakini pia, kizazi hiki kimejaa wimbi kubwa la wazazi wanaolea watoto kwa tamthilia ndio sababu wahitimu wengi wanaishia kwenye kubeti na kamari na kuwa mzigo kwa wazazi kwa kwa jamii nzima.
Leo hii wapo watoto/vijana hawajui kufua, kulima, hata kujitegemea mambo madogo madogo hawawezi na wamemaliza form six....wanafikiri maishi ni kuishi kwa remote....na ndio hao wa get rich soon....kila nafasi wanayopewa wanawazia kuiba, kutotenda haki, kuchepusha ili tu watajirike; hawana uzalendo.....

Natamani muda wa jeshi uongezwe na kufikia walau mwaka kama zamani (China wao ni miaka miwili)
na hii ingewajenga watoto (vijana) wawe tayari kupambana na maisha yajayo badala ya kuwa mzigo kwa wazazi.... MTOTO YEYOTE MWENYE CHANGAMOTO YA KIAFYA, ANAKWENDA NA CHETI CHA DACTARI NA KINAZINGATIWA. Acheni kudanganyana/ acheni kuamini porojo za kijiweni!!!
VIJANA WALIOHUDHURIA JESHINI NI FAIDA KWA MZAZI, KWA JAMII NA KWA TAIFA!!!
 
Huo "uzalendo" unaousifika huko jeshini ndio huo ulioonekana October 29 na kuendelea au kuna mwingine! 🤔
Hata mimi najiuliza swali hilo hilo mkuu. Kama JKT ndiko uzalendo unakojengwa mbona mafisadi wote wanaotusumbua nchi hii wamepita huko? Huo uzalendo waliovuna huko uko wapi? JKT ni mahali pa ovyo. Usimruhusu mwanao kamwe kwenda kuteswa na kutwezwa huko kwenye makambi ya mateso.
 
JKT ina faida sana kwa hiki kizazi,hiki kizazi kina mapungufu mengi aisee
Mimba na UKIMWI ni faida mkuu? Kama hiyo ni faida basi mpeleke huko mwanao au dada yako akajazwe mimba na kuambukizwa UKIMWI. Usitulazimishe.
 
Uzalendo ni kisingizio kinachotumiwa na CCM kuwatweza watoto wa walalahoi kwenye makambi yao haya ya kijanjaweed.
 
Una hakika kwamba hayo "mazuri" wanayoyapata huko JKT hawawezi kuyapata sehemu nyingine mkuu? Can you substantiate your claims?
 
Imagine toto umeliona linatingisha alafu wewe ni mkufunzi alafu ni binadamu unahsia utafanyaje kama ni wewe?
Ndio maana nasisitiza kwamba hii JKT ni upuuzi mtupu, haina tija yoyote kwa vijana wa taifa hili mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…