Hamna. Mimi naonaga ni bonge la ufalasi, eti mtu kakutosa, kaenda kuoa/kuolewa kwingine huko!; afu bado unarudi kulala naye kama mchepuko. Haswa hawa ndugu zetu utawasikia tu; wewe mkomeshe tu, mpelekee moto; ngoja akuambukize na Ukimwi, utajua haujui. Wote mnakuwa hamna akili; ukiachwa songa mbele kama Injili. Hakuna heshima kwa mwanaume anayelala hovyo na wanawake in the name of kuwakomesha, haijalishi walikuumizaje. Afu inakuwa kama bado hujamsahau na una uchungu naye moyoni, ndiyo maaana unahisi ukimlala tena utakuwa umemkomoa. Bado tu unamuwaza mtu ambaye anaendelea na maisha yake. Pathetic