Hatimaye ndoa yangu imevunjika

Hatimaye ndoa yangu imevunjika

Ndo maana kuna comment flan nilisema
"Wanawake wa kipindi hiki ni ngumi jiwe, Ukimpiga ya bega yeye anakupasua ya JICHO"

maumivu yake utasimulia mpaka vitukuu
Wengine hatupendagi ligi. Tukichoka tunasepa tu. As long as hudaiwi cha mtu baasi... maisha yanasonga..

Nachofurahigi ni wanaume kulalamika kupata wake wema ila wakipata wanawanyanya wanaenda kwa slay queens na makalio makubwaaa... siye tupoooo endeleeni kutuita wasimbe eh[emoji23][emoji23] lakini cha moto munakiona huko
 
Haha mkuu kilichokuuma Zaid Ni mwanamke kujinyeregesha mwenyewe ...!
Aisee inauma sana mkuu, lazima kama kidume ukae ujiulize uanaume wako uko wapi kama mkeo unaelala nae kitanda kimoja kajiunga CHAPUTA, vikao vyote anahudhuria na hisa zote anapanda.
 
Exactly,
Ndo mana michepuko hawanaga jema.

Anaweza kukuonesha kukupenda sana unapokua unamkeo.

Ila ukiachana na mkeo, afu kiabya zaidi kiuchumi uyumbe.
Na yeye anakata maguu unakufa na Depreession yako kifuani
Si tumeona kwa vigogo wengi tu? Yanawakutaga na wanaacha funzo ila wengine kimyaaaa... hamujifunzi...
 
Asalaam,

Ndoa yangu ilikua nzuri saana kwasababu tulianza tukiwa vijana wadogo maskini, kutokana na hivyo tuli inspire vijana wengi na ndoa nyingi kusimamia.

Tuka barikiwa watoto wazuri. Mungu alitubariki na unafuu wa maisha wa kupata tunachokita kwa level ya maisha ya kawaida. Basi ghafla maisha yakabadilika nikaanza kupitia magumu kiuchumi hata jero mtihani kupata.

Balaa lilianza hapo kudharaulika, kununiwa, Visa vya kila aina mpaka hatimaye Mimi ndiye nikawa "mama wa nyumbani" na yeye akawa anarudi nyumbani ka guest house ni kulala tuu bila kujali hata watoto wanna hali gani.

Biashara nimemfungulia mwenyewe, na hata kodi nimekua nikimsaidia kulipa. Pamoja sasa Sina shughuli maalumu lakini Mungu ananisaidia kumudu kutimiza mahitaji muhimu ya familia yangu.

Sasa amepata mwanaume mwingine na amenidhibitishia na nilipohitaji aende kwao akapumzika akaniambia hawezi atabaki Dar aendeleze maisha yake kwakua anashida saana ya hela. Kumbe nia yake ni kuendelea kuishi na huyu mwanaume.

Leo nimedhibitisha. Ndoa yangu haitakuwepo tena baada ya kukamilisha taratibu za kisheria.

Roho inauma kwakua sikutegemea kama wanangu wataishi na mzazi mmoja.

Wanaume tutafute hela, ndo thamani yetu!

#Mwanamkemkwelinimamayakotuu

Speaking from experience... Wanasema love is blind

Dharau huwa zinaonekana mapema Sana, Ila wewe Kama mume unakua wa mwisho kuziona, baadhi ya wanaokupenda huwa wanaona lakini hawawezi kukuaambia because you will react to them

Tunachotakiwa kufanya Ni kujua mapema Aina ya wake zetu ili tusiwe surprised badae

Separation na divorce siku hizi sio Cha kushangaa tena, kwasababu maisha yamekua too open and th choices are too many

Tulia, tafuta chocho, uendelee na maisha

Inshallah utapata akufaaye
 
Wanaweza kurudiana hao,
Achana kabisa na kitu inaitwa MAPENZI.

Hainaga mwenyewe
Yes. Its possible endapo jamaa huko akazingua. And obviously atazingua tu najua[emoji23][emoji23] sema sasa mke sasa hv anapata ukuni wa size XXXL itakuaje tena na raha ya gongo anaijua
 
[emoji122]safi sana binti mzuri nahahidi kuchangia matofari 100 kwa ajiri ya ujenzi wa sanamu lako[emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23] sanamu langu lijengwe kwa zege sitaki tofali.. na liwe njia panda ya HIMO na MOSHI MJINI[emoji23][emoji23]
 
Nayaona sana mtaani,

Vijana wanatia tu mbegu wanakung'uta makalio wanasepa zao.

Unakuta binti wa watu alijitoa moyo wake wote kwa mtu asiekua na mpango nae.

Sitamani kabisa ije itokee kwa mabinti zangu, Eeh mungu nisaidie
Mwenyezi Mungu akusimamie mkuu. Na ikawe kheri kwao. Awaepushe na vijana wahuni
 
Ila mkuu kabla ulete utetezi wako uliaga ukasema utajua mbivu ma mbichi nilijua exactly utaleta makaburi tu[emoji23][emoji23] watu wanajisahaugi sana.

Kuna mwanamke alikua analalamika juzi huku anataman kurejesha hisia kwa mumewe akasema mume anamsaliti etc. Mara makaburi ya mchepuko yakaletwa huku[emoji23] nashindwa elewa inakujae mtu anakua kbs proud kuchepuka.. japo siwez mlaumu asilan maana sijui source hasa ni nn. Japo alijitetea mumewe ndo alipelekea yeye kufika huko lkn from the scratch hakuelezea kwamba pia anachepuka unavyoleta kisa elezea ukweli kinaga ubaga kila kitu ili ushauri utakaopewa iwe tiba kwako. Dont play victims.
Binadamu tunajisahau sana,
afu tunayowatenda wenzetu na sisi tukifanyiwa POVU LINATUTOKA.

Mi mwnyw nna makaburi yangu kibao, siku yakilipuka wahuni mnakuja kunilipua.

Eeh mungu ninusuru, Niliyoyapitia yananitosha kiukweli.

Kwa sasa nimekua mume bora kwa mke wangu na baba bora kwa wangu.

THE REST IS HISTORY
 
Hamna. Mimi naonaga ni bonge la ufalasi, eti mtu kakutosa, kaenda kuoa/kuolewa kwingine huko!; afu bado unarudi kulala naye kama mchepuko. Haswa hawa ndugu zetu utawasikia tu; wewe mkomeshe tu, mpelekee moto; ngoja akuambukize na Ukimwi, utajua haujui. Wote mnakuwa hamna akili; ukiachwa songa mbele kama Injili. Hakuna heshima kwa mwanaume anayelala hovyo na wanawake in the name of kuwakomesha, haijalishi walikuumizaje. Afu inakuwa kama bado hujamsahau na una uchungu naye moyoni, ndiyo maaana unahisi ukimlala tena utakuwa umemkomoa. Bado tu unamuwaza mtu ambaye anaendelea na maisha yake. Pathetic
Apo ndio weegi tunafeli.
Binafs ukishakua ex, kila kilichochako nafuta.

No need for more communication, hata urafiki wa kawaida sitakagi.

Tuishi tu ivyo ivyo BUYU BAYA kila mtu na hamsini zake.
 
Binadamu tunajisahau sana,
afu tunayowatenda wenzetu na sisi tukifanyiwa POVU LINATUTOKA.

Mi mwnyw nna makaburi yangu kibao, siku yakilipuka wahuni mnakuja kunilipua.

Eeh mungu ninusuru, Niliyoyapitia yananitosha kiukweli.

Kwa sasa nimekua mume bora kwa mke wangu na baba bora kwa wangu.

THE REST IS HISTORY
Hahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahaa daaaahh, natamani ulete shuhuda ya matukio uliyopigwaaaa...
 
Kabla hata ya maradhi, where is your self worth? Imagine mtu alikudump, leo anajiskia kukutumia tena eti na wewe unajipeleka mbio mbio, kutoka kuwa mmiliki hadi kuwa mchepuko mweeh. Unajiweka kwenye hatari ya maradhi, unayaweka mahusiano yako mapya kwenye risk, bado ikitokea umefumaniwa mweeh.

Yes ni muhimu kujua kwa nini waliachana, kuna maumivu unaweza kuyaepuka mapema; ingawa majority hatusemagi ukweli kwamba tulizingua tukaachwa, always sisi ndiyo victims teh. Hiyo ya kujua familia/koo husika sasa mmmmh; ngoja ninyooshe miguu kwanza.

Hivi on a serious note, watu huwa hawaogopagi maradhi? Yaan jaman watu wanajitoa ufahamu. Hawaogopi hata lepe aiseee.. mwanamke amenishangaza kuingia kwenye nadhiri ila ameshataka ivunja mapema.

Nakumbuka home tulifundishwa kufatilia hasa sababu za partner wako kuachana na ex wake na kuijua familia husika kabla uingie kwenye ndoa. Kuna familia hazifai kabisa
 
[emoji23][emoji23] sanamu langu lijengwe kwa zege sitaki tofali.. na liwe njia panda ya HIMO na MOSHI MJINI[emoji23][emoji23]
Usijali kabinti mzuri nishaongea na manager wa kiwanda cha dangote cement acheck utaratibu nipate mifuko 80 ya cement😂😂😂😂
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
Bila shaka unaikumbuka hii DOUBLE FLYING KICK enzi izo[emoji2][emoji116]
images-220.jpg
images-221.jpg
 
Kabla hata ya maradhi, where is your self worth? Imagine mtu alikudump, leo anajiskia kukutumia tena eti na wewe unajipeleka mbio mbio, kutoka kuwa mmiliki hadi kuwa mchepuko mweeh. Unajiweka kwenye hatari ya maradhi, unayaweka mahusiano yako mapya kwenye risk, bado ikitokea umefumaniwa mweeh.

Yes ni muhimu kujua kwa nini waliachana, kuna maumivu unaweza kuyaepuka mapema; ingawa majority hatusemagi ukweli kwamba tulizingua tukaachwa, always sisi ndiyo victims teh. Hiyo ya kujua familia/koo husika sasa mmmmh; ngoja ninyooshe miguu kwanza.
Ex huwa ni ujinga sana. Yaan mtu amechagua maisha mapya amekudump halaf eti amekukumbuka eti. Na sababu kibaooo[emoji23][emoji706]

Siku akiwa ameshaharibu ndo ooh nilipitia changamoto nyingi sana blah blah. Kwamba ndo pumziko. Dhambj zingine za kuepuka tu. Stress zisitupelekee kufanya chaguzi zisizo sahihi asilani
 
Back
Top Bottom