Hawa Feminist walipofikia ni pabaya sasa

Hawa Feminist walipofikia ni pabaya sasa

Nani achanganyikiwe...labda kama ubongo wa mtu anaejisikia kuchanganyikiwa ni empty set. Hivi hili ni jambo la kudebate kweli? Ukute huyo Shamira hafanyi haya anayoyasema katika jamii. Wanaune wakipinga mahari, wanawake tunasema ni mila na tamaduni za kiAfrica, saivi tunazikataa tena mila zetu. I guess she is chasing clout au ndo donors wa organization yake wamempa hizi terms kwamba awe feminist wa mchongo..it actually doesnt suit her [emoji849][emoji849].

Haya mambo ya gender nyee..gender nyaa yanatuharibu kwa speed ya 5G. Mbaya zaidi kuna gen Z wakikutana na such content, wanaicopy na kwenda kuipaste kwenye familia zao zijazo. Misingi ya kiAfrica iheshimiwe maana inapass on value kubwa sana kwetu. Binti asomeshwe sawa. Lakini hata akipata kazi, ajue primary purpose yake hapa duniani ni kulea familia na kurithisha mema kwa kizazi chake.

Sipendelei kushindana na wanaume kufanya kazi mpaka saa mbili usiku ndo nitoke kazini, ili nisecure promotion..mwisho wa siku watoto ninaowapambania wanakuja kunifurahisha..show show..afu nakimbilia kwa Mwamposa kubeba mafuta ili mapepo yawatoke..hata shetani atasema dada nikome..umeyachuma mwenyewe. Family (incase umepata hii nafasi) inatakiwa ibebe 70% of your time, Career 30%. Naona hii ni balance moja nzuri, unless otherwise.. alijisemeaga The Boss, unaishia kuwa corporate slut..raha iko wapi kwenye ubatili huu??
Safi Sana dada inabidi ujengewe Sanamu pale uwanja wa Taifa alimaarufu kwa Mkapa na pale uwanja wa ndege JNIA na Makumbusho zote za Taifa maana Ni wanawake wachache waliobaki na Busara Kama zako hebu chukua[emoji259][emoji255][emoji1651][emoji257][emoji253]yako.
 
"Moja ya ukatili ambao wanawake wanafanyiwa ni kufanyishwa kazi majumbani bila kulipwa, kiuhalisia mwanamke anapofanya kazi za nyumbani lazima alipwe, kwasababu hujamuoa awe house girl wako, yule ni mke wako ambaye umemuoa kwa malengo maalumu na siyo ya kufanya kazi za nyumbani."

"Sisi kama wanaharakati tupo kwenye mchakato kuhakikisha ule muda ambao mwanamke anautumia kufanya kazi za nyumbani uwe na manufaa kwake, alipwe na mume wake."- Shamira Mshangama, Mwanaharakati.

Wamefikia stage mbaya sana aloo.
[emoji174][emoji23][emoji23]View attachment 2713479
Kwani walio kwenye mahusiano wanasemaje?
 
Mbona kuna watu wanawalipa mshahara wake zao hasa wale waliowaachisha kazi au walikataa wasipate ajira wakae nyumbani kutunza familia,

Nakubaliana na huyo Mwanaharakati wake za watu wanaoshinda tu nyumbani walipwe mshahara na waume zao, wanafujika bure na kushindwa hata kusaidia kwao.
 
Anaetoa ushauri unakuta ni single maza hajaolewa. Wewe na ndoa yako unachukua ushauri kichwa kichwa shauri yenu.

By the way kama ulitaka kulipwa bas sema mapema kabla ya ndoa mhusika ajue mpo kibiashara, na kanisani kiapo kibadilishwe so unaingia ndani unataka kulipwa.

Pia kama unataka kulipwa basi make sure unajitegemea kila kitu, sio unalala kwangu, nakulisha, nakuvalisha, nalipia ada za watoto, etc

Nikikulipa basi na wewe unanilipa rent nyumbani kwangu, unalipia umeme unaotumia, maji, ada watoto unatoa nusu, gari yangu unakodi etc

Housegirl yupo anafanya kazi zote, wewe unataka kulipwa? Shubamiti
 
Mbona kuna watu wanawalipa mshahara wake zao hasa wale waliowaachisha kazi au walikataa wasipate ajira wakae nyumbani kutunza familia,

Nakubaliana na huyo Mwanaharakati wake za watu wanaoshinda tu nyumbani walipwe mshahara na waume zao, wanafujika bure na kushindwa hata kusaidia kwao.
Tangu kuumbwa kwa ulimwengu kazi ya mwanamke ni KUZAA na KULEA TU. Majukumu sahihi ya mwanamke ni nyumbani na kuwajibika kwa mumewe PEKEE. hayo majukumu mengine mnayojivisha ndio chanzo cha migogoro na shida nyingi za kifamilia duniani na ndio matokeo ya familia za ovyo na vizazi vya ajabu ajabu.

Mungu hakuwa mjinga kwenye ugawaji wa majukumu kwa mwanamke na mwanaume.
 
Mbona unafafanua mada na sio msemaji! how do you know?

Mbona unaweka utaratibu kulingana na fikra zako! Wakati kila familia inamifumo yake! Hata familia za watumishi zinamifumo yao yakuendesha ndoa bila shida na wala bila ayo malipo unayoyapromote hapo, year it can be impossible to you but not for all.

Mke kufanya kazi/kutokufanya kazi za ndani ni swala la maelewano watu wawili, kinachopigwa hapo ni uyo dada kuamka alipotoka na kutaka kuonesha kama vile wanawake wanateswa kwa kuwapikia wammezao na kufanya shighuli zingine za nyumbani, mbaya zaidi kaamua kabisa kuweka utaratibu kwamba iwe malipo as if ndoa sasa imekua ajira!

Hivi hujui kua kuna nyumba zingine wanaume na wanawake zao wanafanya kazi kwa kushirikiana! Leo hii akitokea mwanaharakati wakiume akasema sio sawa ela za mwanaume ndo zitumike ndani kwakua wote wanalipwa mishahara iwe sheria ela ikitoka inakatwa pasu kwa pasu kwajil ya matumizi ya nyumbani ivi unahisi wanawake wote watakubali? Je kama wataibuka wanaharakati wakiume wakasema sio sawa kutoa mahari ili kuoa maana upendo sio biashara je wanawake watakubali?

Hayo mambo hua nimaelewano ya mke na mume ndani sasa kama yeye ndo kaona ivo akakokotane na mme wake mahakani sio apangie watu wengine utaratibu wamaisha.
Well spoken my brother
Hata vigezo nowdays vitapungua kwa wanawake kuolewa
Tunakoelekea itakuwa Bora mwenye marinda tuu na tukifikia hapo basi ndugu zetu wale wa "KATAA NDOA" watapata pa kusemea
 
🤣🤣🤣kweli lakin
Kuna wake za watu wanazeeka haraka kwa majukumu ya nyumbani,ya kufua mijinsi,kupikia ukoo,kutunza mifugo kama mbuzi, kuku, bata, kuosha mijivyombo,kuteka maji, daily kupiga deki nyumba, wengine kulima kila msimu yeye na watoto,bado kuzaa double double na kulea bila hata hausigelo.
Kuzeeka hakuzuiliki hata wanaofanya makeup wafanane na shetani nao uzeeka tu
 
Hing
Shamira ni wa kupuuzwa ila kama alivyotangulia kusema mwanaJF Ironbutterfly ni kweli kuna wanawake wanazeeshwa fasta kutokana na kazi nyingi huku akizalishwa kwa kasi.

Vijijini hasa uchagani utakuta msichana mdogo kakomaa kwa kazi zilimzozidi nguvu.

Hata kama hatuwalipi tuwatafutie wasaidizi au ikiwezekana kuwasaidia sisi wenyewe pale tunapoweza. Mimi kiukweli dada zangu niliwashauri wasiolewe na maskini. Wangeteseka sana aisee.
Hongera vipi walipata matajiri
 
Ndoa sio lazima Ivo yani,maana mambo yanazidi kuwa mengi: mwanamke alipweashahara,mara ndoa ikivunjika mwanamke apewe nusu ya Mali yote iliyochumwa atakama hakushiriki kutafuta ila tu kwakuwa uliishi nae kinyumba,mara mke ni msaidizi WA mwanaume lakini hapohapo apewe mshahara,mara mke Naye harusiwe akafanye kazi huko maofisini n.k

.NDOA sio lazima bhana huitaki achana nayo waachie wanao iweza, makelele tu Kila siku ya Hawa wanaharakati uchurwa
 
Komaaa hayo ndiyo maisha
Ukishindwa kataa kuolewa sio lazima uolewe

Kula maisha subiri kufa wala usizae
Hawawezi pingana na lengo la Mungu.

Mwanamke alie-olewa, anaetunza vyema familia yake, anaetimiza vyema majukumu yake yote ya kifamilia, alierizika na hali na huduma anazopata kwa mumewe. Anafuraha na raha kuliko hao wanaojiita wapambanaji huko nje.

Nazungumzia familia zenye wanaume wanaojielewa na kujali wake na familia zao.
 
Back
Top Bottom