Hapa kuna funzo kubwa sana, Nami nitaongezea kisa kimoja nilichopata kusimuliwa na watu ninaowaamini.
Miaka ya hapa kati (2010-2015) kanisa moja la Anglican tena ni kanisa kuu la diocese lilikuwa linafanya sherehe za kutimiza karne moja tangu kuanzishwa kwa diocese hiyo, moja kati ya diocese kongwe hapa Tanzania.
Basi Siku hiyo kulikuwa na maandamano ya waumini na viongozi wa kanisa kutoka mahali ambapo ndipo palikuwa na kanisa la kwanza kabisa la dayosisi hiyo mpaka lilipo kanisa kuu la sasa ambalo nalo ni la zamani sana.
Basi maandamano yalikatiza mitaa ya katikati ya mji wakiongozwa na kiongozi wa maandamano aliyebeba MSALABA mkubwa wa mbao.
Waandamanaji walipofika maeneo ya katikati ya mji akatokea bwana mmoja aliyekuwa mchukuzi maarufu wa maeneo hayo kwa jina maarufu CHENGO, basi yule bwana CHENGO alicheka kwa kejeli na kutoa maneno ya kuudhihaki msalaba, alizidi kutoa maneno machafu kwa Waandamanaji na juu ya ule MSALABA MTAKATIFU.
Baada ya maandamano kupita na kuisha katika maeneo yale yule bwana alipata ajali ambayo mpaka leo hakuna ajuaye BWANA CHENGO aligongwa na chombo gani. Hakuna gari iliyoonekana kwa macho ikimgonga lakini ndiyo hivyo yule bwana akapoteza uhai siku ileile tena muda mfupi baada ya kuunanga MSALABA MTAKATIFU
Tuweke akiba ya maneno