Hawa ni watu waliomdhihaki Mungu na kupatwa na shida

Hawa ni watu waliomdhihaki Mungu na kupatwa na shida

Nadhani hoja ya mtoa mada ni kufanya kufuru kwakutokubali uwepo wa Mungu na hukumu ya haraka sana baada ya kukufuru.
Hoja sio kifo bali nikifo cha haraka sana baada ya kuona kwamba hakuna ukuu wa Mungu na mamlaka yake
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2962][emoji2962]Biololgy and laws of universe zinakupinga
 
Mungu gani?

Hutaki habari za mantiki katika Mungu wakati wewe kuniuliza swali tu kuhusu Mungu ni lazima ushatumia mantiki.

Unaelewa unachoandika? Au unaandika tu?

Kumbe huna hoja ya kuthibitisha hakuna Miungu.

Unafikiri hiyo akili ya kujua mantiki sijui nini kakupa nani? Kwanini mbuzi hawajui habari za mantiki?

Unakwepakwepa tu.

Utakuwa ulipitia magumu ndio maana unaona hakuna Mungu.
 
Walimdhahaki Mungu yupi.Mungu wa waislamu au wa wa wakiristo?
Wakristo wana trinith waisilami wana mungu mmoja. Waisla wanamdhihaki mingu yesu kila siku nao wakiristo wanamdhihaki mtume na mungu wake.
Hata JF watu wa dini tofauti wanadhihakiana kila siki.
Katika vitsbu vyote vys mungu sijawahi sikia Mungu akiahidi au kuonya kuwa atawadhuru wale wanaodhihaki bali mafikio yao yatakuwa jehanamu au moto wa milele huko mbinguni.
Tunafanyiana matuki mabaya kisha tunamsingizia mungu au shetani. Sisi binadamu ndio mashetani wakubwa, tunamatendo mabaya sana dhidi ya wengine na Mungu.
Kuna watu wanaunda sumu za kuua wengine lakini bado hatuwaoni kuwa ni wabaya.
 
Hawa walikufa mapema kaa sababu gani?
1.Steven Kanumba
2.Sharo Milionea
3.Bruce Lee
4.Tupac Shakur
5.Malcom X
6.Paul Walker
7.Bob Marley
8.Kobe Bryant
9.Michael Jackson
10.Princes Diana.
11.Whitney Houston
12...
13....
..
.
1. JOHN LENNON (MUIMBAJI)
Wakati alipokuwa akihojiwa na mwandishi wa habari wa gazeti la American alinukuliwa akisema hivi "Ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi kuwa na wasiwasi na hilo kwa kuwa nina uhakika nalo. Mafundisho ya Yesu yalikuwa sahihi na wala sipingi hilo ila mafundisho yale yalikuwa mepesi sana ambayo mtu yeyote anaweza kuyafundisha. Hebu angalia leo, tumekuwa maarufu hata zaidi yake (Hapo alilitaja kundi lake la The Bettle). Ilikuwa mwaka 1966. Wiki moja baada ya kutamba kwamba yeye na kundi lake lilikuwa maarufu hata zaidi ya Yesu, akapigwa risasi sita na kufariki.

2. TANCREDO NEVES (RAIS WA BRAZIL)
Alisema kwamba endapo angepata kura laki tano kutoka katika uchaguzi mkuu wa Brazil na kuwa rais, hata MUNGU asingeweza kumtoa katika urais huo. Akafanikiwa, akapata kura zaidi ya hizo, akashinda uchaguzi, siku moja kabla ya kuapishwa, akafariki dunia.

3. CAZUZA (MWANAMUZIKI WA BRAZIL)
Alipokuwa katika shoo yake ndani ya jiji la Rio De Janeiro, alichukua sigara, akaanza kuivuta, akachukua nyingine na kisha kuirusha juu na kusema "Mungu, hiyo yako, chukua nawe uvute" Alifariki akiwa na miaka 32 kwa ugonjwa wa kansa ya mapafu ambayo iliyaharibu sana mapafu yake kuliko mgonjwa yeyote yule.

4. MTENGENEZAJI WA MELI YA TITANIC
Baada ya kutengeneza meli ya Titanic, mwanahabari akamuuliza ni kwa kiasi gani ilikuwa salama nae akajibu "Ni salama sana, haiwezi kuzama na hata Mungu hawezi kuizamisha" Nafikiri unajua kilichotokea kuhusu Titanic.

5. BON SCOTT (MUIMBAJI)
Mwimbaji huyu ambaye alitamba miaka ya 70 alitoa wimbo wake mmoja mwaka 1979 wenye maneno haya "Don't stop me; I'm going down all the way, down the highway to hell'. Tarehe 19 February mwaka 1980, alikutwa amekufa baada ya kupaliwa na matapishi yake.

6.
Mwanamke mmoja alikuwa akihofia sana kuhusu ulevi wa marafiki wa mtoto wake.
Wakati wanataka kuondoka na gari, akamshika mtoto wake mkono garini na kumwambia "Binti yangu, Mungu awatangulie katika safari yenu" Yule binti akajibu "Gari imejaa mama, huyo Mungu labda akae kwenye boneti la gari". Baada ya masafa fulani ya safari yao, gari lile lilipata ajali kiasi ambacho hata polisi hawakujua ni aina gani ya gari lilikuwa. Lilikuwa limebondeka sana na watu wote walikutwa wamekufa. Kilichowashangaza polisi, trey la mayai wala halikuonekana kuguswa na hakuna hata yai moja lililokuwa limevunjika na wakati gari lilibondeka mpaka kutokutambulika.

7. CHRISTINA HEWITT (MWANDISHI WA HABARI)
Huyu alikaririwa akisema hivi "Nimesoma vitabu vyote duniani, ila hakuna kitabu kibaya...kibaya na kibaya kama Biblia" Siku chache baada ya kusema maneno hayo, mwili wake ulikutwa umeunguzwa na moto ambao haikujulikana mpaka leo ule moto ulisababishwa na nini.

8. MARILYN MONROE (MUIGIZAJI)
Huyu alifuatwa na Bill Graham na kumwambia kwamba alitumwa na Roho wa Mungu kwa ajili ya kumhubiria. Alimkaribisha ndani, akamsikiliza kwa makini, alipomaliza akasema "Simuhitaji Yesu wako, unaweza kuondoka nae". Wiki moja baadae, alikutwa amekufa katika makazi yake. Polisi walijaribu kuchunguza kipi kilimuua, mpaka leo hawajapata jibu
hakuna kama Mungu.

Follow me on twiiter as LegalGentleman
 
Thibitisha
Kiimani watu wenye imani ya juu zaidi ndiyo hupewa mitihani mizito zaidi na Mola kuliko ambao hawana imani. Ndiyo maana wewe leo unamkana lakini anakupa rizki na mfano wake na wapo ambao waliishi bila kuumwa kwa miaka na mikaka wakachupa mipaka na kudai uingu na kumkana Mola.

Na kadhalika Mola huwaadhibu watu waovu kwa njia hizo hizo.
 
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kuumba ulimwengu ambao viumbe wake anaowapenda wanakufa, wakati wao wanapenda kuishi, ni contradiction.

Unaelewa hilo?

Unaelewa contradiction ni nini?

Kilanga hizo sifa za Mungu ni za kweli kabisa na hakuna kufa bali kilichopo ni kuhama ulimwengu wa kimwili kurudi ulimwengu wa kiroho kama ilivyo kua awali kabla hujaja. Hiyo safari ya kuhama ina maajabu yake Wakati anapo hama mmoja wetu kutoka ulimwengu wa kiroho kuja ulimwengu wa kimwili walio tangulia humpokea kwa furaha na vigerere mno
Anaporudi ulimwengu wa kiroho waliobaki husikitika na vilio vingi.
Kwa hiyo Kilanga bear in ur mind there is no death as a death u think so but reality is a shifting from point A to point B that so.
 
Nadhani hoja ya mtoa mada ni kufanya kufuru kwakutokubali uwepo wa Mungu na hukumu ya haraka sana baada ya kukufuru.
Hoja sio kifo bali nikifo cha haraka sana baada ya kuona kwamba hakuna ukuu wa Mungu na mamlaka yake
Hawa walikufa mapema kwa sababu gani?

1.Steven Kanumba
2.Sharo Milionea
3.Bruce Lee
4.Tupac Shakur
5.Malcom X
6.Paul Walker
7.Bob Marley
8.Kobe Bryant
9.Michael Jackson
10.Princes Diana.
11.Whitney Houston
12...
13....
..
.
 
Upo sahihi japo watu wanakupinga ni wafinyu wa fikra
Kuna wengine Hawa hapa Stephen Hawking mwanasayansi nguri yeye baada kubukua vitabu akasema hakuna Mungu aliishia kuumwa gonjwa la ajabu Sana ,na gadafi wakati yupo Uganda aliwahi kusema Biblia ni makaratasi siyo maneno Mungu akakitupa chini na kukanyaga kilichobaki watu wake aliowalisha asali na maziwa wakamtoa uhai
NB Mungu anatokea kwa namna ambayo binadamu hawezi kutambua

Stephen Hawking
mach_hawking_thumb.jpg
 
Upo sahihi japo watu wanakupinga ni wafinyu wa fikra
Kuna wengine Hawa hapa Stephen Hawking mwanasayansi nguri yeye baada kubukua vitabu akasema hakuna Mungu aliishia kuumwa gonjwa la ajabu Sana ,na gadafi wakati yupo Uganda aliwahi kusema Biblia ni makaratasi siyo maneno Mungu akakitupa chini na kukanyaga kilichobaki watu wake aliowalisha asali na maziwa wakamtoa uhai
NB Mungu anatokea kwa namna ambayo binadamu hawezi kutambua

Stephen Hawking
View attachment 2053040
wewe jamaa ni mwongo mwongo sana Eti
Stephen Hawking alimkana huyo Mungu ndio akapata ugonjwa wa ajabu hivi hizi stori hua manazipata wapi?
Hebu Rudi kasome historia ya maisha ya huyo nguli ndio urudi hapa utupige Kamba zako!
 
Nachozungumzia ni kuwa matatizo humkuta yeyote hiyo ni nature wala haitegemeani na jinsi unavyo mcha sana Mungu kwamba utakua upo salama.

Kwa hiyo hata kwa hao uliowataja ifahamike kiujumla kua walipata matatizo ya kawaida tu bila kuhusisha element za laana.

Ukiniruhusu nitumie mfano wako wa huyo mmiliki wa meli ya titanic na kwa namna ulivyoeleza kua Mungu alizamisha meli kwasababu ya maneno ya dhihaka aliyoyatoa huyo mmiliki basi mwishoni hata mimi nitakosa busara ya uvumilivu hata mimi pia nitamdhihaki Mungu huyo

Kwasababu ile meli ilivyozama haikumuua mmiliki pekee, iliua watu wengi wakiwemo watoto wadogo wasio na hatia.

Kwanini Mungu anakua mpumbavu na kukosa huruma kwa watoto wadogo kuwaangamiza kwenye dhambi ambayo hawajahusika?

Watoto walichangia vipi kwenye hiyo dhihaka?
Kufa sio hatia kufa ni wajibu kwa kila mtu iwe wenye hatia na wasio na hatia wote tutakufa tukio linaweza kuwa moja lakini likiwa ni muunganiko wa matukio mengine pengine hata huyo mtu asingesema hayo maneno ajali ingetokea na watoto wangekufa vilevile. Mleta mada kachukua tukio kwa kuangalia katika angle fulani kwa sababu kila angle inajaribu kutoa funzo.
Jichukulie wewe ndo mmiliki wa hicho chombo/meli na ukasema maneno hayo ya kujiamini na kujiaminisha alafu mwisho wa siku chombo chako kikazama unafikiri baada ya hilo tukio ungekuwa na mtazamo gani?
 
Mimi nakuuliza dhana inayopita lugha, wewe unajibu neno la lugha moja.

Hiyo ndiyo tofauti yangu na wewe.

Ni kama tofauti ya guluguja na mtu mwenye aliyekamilika.
Hii tabia ya kukwepa maswali utaiacha lini ? Nilipo toa maana ya tamko Imani niliishia kwenye asili pekee au nikaarifisha tamko husika ? Ungekuwa umejikita humo unapo dai usingeingia katika mlango ambao huwezi kutoka. Ukajitia ujuaji ukaacha maana ukajadili asili ya neno hui ndiyo ujinga wako ulipo,na ulipo kuja kwenye asili ukashindwa kujitetea.

Maana niliyo kupa imekusanya zama zote juu ya tamko hilo.

Sasa jibu swali nililo kuuliza thibitisha ya kuwa tamko Imani si lenye asili ya Kiarabu.
 
Umeelewa nini?
Nimemuelewa kwamba licha ya wengine kufa pia pasipo kumdhihaki Mungu lkn mifano aliyotoa ya vifo vilivyotokea baada ya watu hao kumdhihaki Mungu ni tofauti kwa kuwa kwanza vimetokea ghafla mara baada ya kumdhihaki Mungu.Mfano ni hayo mayai yaliyosalimika wakati gari lilipinduka na kuua watu wote,huoni huo ni muujiza? Lkn huyo mwingine aliyeungua kiajabuajabu!! Na huyo rais aliyekufa bila kuapishwa huoni ukuu wa Mungu?
 
Una point sana, ila shida ni kuwa ume base sana kwenye "kudhihaki" kuwa ndio chanzo cha shida ilihali maisha ya hapa duniani, whether you are doing bad or good shida ni ngumu kuziepuka..
 
Mtoa post unaonekana kabisa wewe ni mdini lakini hata dini yenyewe huna ujuzi nayo, katika hao wote uliowaorodhesha hapo juu hakuna aliyehukumiwa na huyo mungu kwasababu ya kumdhihaki.

Labda nikukumbeshe kitu kimoja, kifo sio adhabu kwa maana huyo mungu mwenyewe kupitia maandiko yake kasema kuwa kila mtu kapangiwa siku yake ya kufa.

Sasa ikitokea leo mimi namdhihaki alafu anihukumu kwa kifo hapo ataonesha wazi kuwa hana msimamo, pia fuatilia alichokisema mkuu SCARS kwenye comment ya #3.

Sio ukristo tu hata uislamu utakufa, kadri siku zinavyokwenda watu wa dini wanaachana na hizi dini baada ya kugundua kuwa hizi dini ni za michongo.
 
Kilanga hizo sifa za Mungu ni za kweli kabisa na hakuna kufa bali kilichopo ni kuhama ulimwengu wa kimwili kurudi ulimwengu wa kiroho kama ilivyo kua awali kabla hujaja. Hiyo safari ya kuhama ina maajabu yake Wakati anapo hama mmoja wetu kutoka ulimwengu wa kiroho kuja ulimwengu wa kimwili walio tangulia humpokea kwa furaha na vigerere mno
Anaporudi ulimwengu wa kiroho waliobaki husikitika na vilio vingi.
Kwa hiyo Kilanga bear in ur mind there is no death as a death u think so but reality is a shifting from point A to point B that so.
Umejuaje haya yote, wakati hujawahi kufa?Yote haya uliyoandika ni mambo ya kusimuliwa tu.
 
Back
Top Bottom