Haya Mambo ya Viongozi wa Kisiasa Kwenda na Viti Vyao Kwenye Nyumba za Ibada Yasitishwe

Haya Mambo ya Viongozi wa Kisiasa Kwenda na Viti Vyao Kwenye Nyumba za Ibada Yasitishwe

Yale mabusati kule msikitini huwa hayaumizi,mbona hapelekewi kiti kule??
Alikuwa na busati lake.
Kijana mambo madogo una complicate,hata Mungu naamini hana tabu nayo.

Kwanza kwa mujibu wa dini yake hakutakiwa hata kuingia humo kanisani tunamtafutia au anajitafitia dhambi.

So akiwa na kiti cha Rais atleast anaweza hata kuhesabika ameenda kama Rais wa Tanzania na sio Samia Suluhu.

Hizi nchi ambazo ni secular(hazina dini) zina changamoto nyingi sana,ikiwemo hii ya kuhudhuria misa za dini mbalimbali, na hili linachangiwa na upumbavu wetu.

Rais hana ulazima wa kwenda katika misa au ibada yoyote kama sio imani yake, wakutane tu katika matukio ambayo sio ya ibada labda tafrija na chakula cha pamoja baada sherehe husika.

Huu UPUMBAVU unatufaa kwa kivuli cha UMOJA NA MSHIKAMANO. Kwa sababu bila kufanya hivyo mtapiga makelele mengi ya kuitana WABAGUZI bila kujali kuwa tunaingilia PRIVACY ya mtu.

Kwa sasa kwa kuwa WaTz wengi vichwa vyetu bado ni GB 32,Ram 2 inabidi twende taratibu tu.

Vipi watu wa imani nyingine ambao hajahudhuria ibada zao kama wahindu,wapentecoste,wasabato na huko Rais anatakiwa aende,au wao sio wengi na sio maarufu kama Waislamu na Wakatoliki(na wa kufanana nao kama KKKT,Anglican e.t.c)?

Lakini ujue kwa mujibu wa dini yake analazimika kuyavumilia haya yote HAKUTAKIWA kabisa kuwa humo,na hata katika nafasi aliyopo WAHAFIDHINA(Conservatives) wa kiislamu wanasononeka...HAIRUHUSIWI
 
Nafasi ya urais haipo Tanzania tu.Pichani juu ni rais wa Zambia na Rais wa Marekani wakiwa katika nyumba za ibada na wamekalia bench.Huyu wa kwetu anashindwa nini kukalia bench,kwamba utakatifu wake umezidi marais wengine ama vp?
Kwani huko Marekani na Zambia kuna ushirikina na unafiki kama ulivyo hapa kwetu?

Sijawahi kusikia Rais wa Marekani kaenda kanisani kutoa Rushwa; hapa kwetu ni kawaida sana.
Kiongozi akiwa Mkristo, ruhwa zake nyingi zinaelekzwa misikitini; sasa na huyu kafuata nyayo zile zile za kwenda kuwanunua viongozi wa kidini huko kanisani kwao.

Lakini cha ajabu, bado wanaogopa kurogwa huko huko kanisani; kwa hiyo inalazimu wabebe viti vya kukalia!
Nchi badala ya kupiga hatua kwenda mbele, sasa tunarudi kinyumenyume.

Hata Mwalimu Nyerere hakuwahi kwenda na kiti chake kanisani kwake aliko sali; na wala sikumbuki kama aliwahi kuingia msikitini au kwenye kanisa la madhebu aliyokuwa yeye.
Hata Mwinyi hakufanya maigizo ya aina hii ya leo.
 
Lakini ujue kwa mujibu wa dini yake analazimika kuyavumilia haya yote HAKUTAKIWA kabisa kuwa humo,na hata katika nafasi aliyopo WAHAFIDHINA(Conservatives) wa kiislamu wanasononeka...HAIRUHUSIWI
Kwani yote haya uliyosimulia kwenye andiko lako hili yameanza lini na kwa sababu zipi..., za UMOJAna MSHIKAMANO? Hatujawahi kuwa na umoja na mshikamano tokea uhuru, ila sasa ndipo imelazimu iwe hivi?

Watu wanao ona maigizo haya na kuyapa sifa ni kujiondoa akili tu.
 
Me nafkr tatizo siyo MH raisi,tatizo n wasaidizi wake ambao kazi Yao n ku arrange hyo siku na appearance ya Kila k2
 
Kwani shida ipo wapi hapo?.
Tatizo wabongo tunapenda ku- judge na kuhoji vitu visivyo na msingi. Hivi kuna madhara ama tatizo gani Kiongozi akiwekewa kiti Kanisani.
Kwa hiyo USA president angekuwa kawekewa kiti ndio ungeona sahihi kwako?.
Tusiwe watumwa wa kuiga vitu vya nje.
Kwani huyu ndiye rais wa kwanza Tanzania kuingia kanisani? Uliona wapi na hao wengine wakienda na viti vyao kanisani. Unajisemea tu mambo bila ya kuyafikiri kwanza?
 
Hii ni lini?
Tatizo na samia auanupenda UMUNGU MKE sana tena sana!
 
Mi Kuna kanisa jirani hapa la sabato na Kuna lingine la EAGT mbona naona waumini wanaendaga na viti vyao vya cello ....
Kama kanisa liko kwenye ujenzi bado, au halijajitosheleza kwa viti ni sawa waende na viti vyao. Lakini kama kuna viti vya kutosha, halafu wewe uende na kiti chako kwa kuona vile vya pale kanisani havina hadhi inayolingama na wewe, unamkufuru Mungu.
 
Amewekewa msala wake wa kusalia !
Maana yake ni kwamba Rais ana ulinzi wa aina yake popote pale anapokuwepo !
Iwe ni Msikitini au Kanisani !
Na hata wale waumini watakaokaa karibu yake ni wale ambao wamekubalika na wanaosimamia ulinzi wa Rais ! Sio kila muumini ataruhusiwa kumsogelea Rais !

Watanzania tuna mahitaji muhimu sana kama Taifa,
Hii habari ya Viti au Misala ya kwenye nyumba za ibada tuwaachie walinzi wa Rais waamue wao atumie kiti au msala upi !
Sisi haituhusu hiyo maana sio kazi yetu !
Sisi tunataka Katiba mpya kwanza 🙏🙏🙏 !
 
Kuna uzi huko ulifunguliwa unataja kiti 👇 CC Walker Water


Nawasalimu wote wanajukwaa,leo nataka tujifunze silaha kuu tano zinazotumika katika ulimwengu wa kiroho.

Kama wengi tunavyojua kuwa katika ulimwengu wa kiroho kuna falme kuu mbili,falme ya kwanza ni ufalme wa nuru na falme ya pili ni ufalme wa giza.

Falme zote hizi zina muundo na uongozi na mamlaka kamili.Katika viumbe vyote binadamu ndiyo kiumbe pekee mwenye sifa ya kuweza kuishi katika ulimwengu wa kiroho na ulimwengu huu wa kimwili kwa wakati mmoja.Inawezekana umesoma vitabu vingi sana na kufanya jitihada nyingi sana ili ufanikiwe katika maisha yako lakini bado umeshindwa.

Nakushauri fuatilia darasa hili kwa umakini na siku ukimaliza Lazima ufanikiwe kwa kuwa manbo yote huanzia katika ulimwengu wa kiroho na ndicho utakachojifunza hapa.

Zifuatazo ni silaha kuu tano za ulimwengu wa kiroho.
1. Damu
2. Jina
3. Kiti
4. Maneno
5. Ardhi na Mbingu

Ukiweza kujifunza silaha hizi kwa umakini,utaweza kujua ulimwengu wa kiroho unavyofanya kazi,utapata nguvu za kuingia katika ulimwengu wa kiroho,utashinda vita vya kiroho na kimwili kwa urahisi na utafanikiwa kimwili na kiroho katika mambo yako.

Somo hiki litakuwa na jumla ya vipande kumi (10),yaana tutajadili silaha moja moja inavyotumika katika ulimwengu wa kiroho upande wa ufalme wa giza na moja moja inavyotumika katika ulimwengu wa kiroho upande wa ufalme wa nuru.

Naomba maoni yenu ya tuanze kuijadili silaha ipi, na tuanze na falme ipi kati ya falme ya nuru au ya giza au somo liishie hapa maana watu wengi hawaamini kama kuna ulimwengu wa kiriho.
 
Mama ni mtu humble sana; na naamini hili ni suala la timu yake ya usalama. Pengine waliona kuna tatizo akikalia mabenchi...

Isitoshe hata kwenye Biblia sidhani kama Wafalme waliingia mahekaluni na kwenye masinagogi na kukaa pamoja na commoners. Eti Mfalme Sulemani au babake Daudi wakalie mabenchi ya hekaluni. Aaaa wapi!

View attachment 2976290
Aaaa wapi !
Kwakweli 😅🙏
 
Sasa unatoa mfano wa marais wa marekani, kwanini hukutoa mfano wa marais wetu? JPM, Nyerere, Kikwete, Mkapa, Mwinyi walivyokuwa wanaenda makanisani walienda na viti vyao?

Sina uhakika na hao wengine. Lakini Mwalimu Nyerere na Mkapa sikuwahi kuona picha ikionesha wakiwa kanisani wamrkalia viti vilivyosombwa toka ikulu.
 
Kwahiyo kiroho unatakiwa kukalia benchi? Hebu acheni hekaya za kijima hizi.

Kiti cha rais au benchi la kanisani haviingiliani kwa vyovyote vile na mchakato wa maombi. Mtu anaweza hata akaja na godoro lake kanisani na wala hakuna shida. Msikariri.

Mleta mada yupo sahihi. Kanisani au msikitini ni mahali ambapo unajinyenyekesha mbele za Mungu, siyo mahali pa kwenda kuonesha kuwa wewe au mwingine yeyote ni zaidi ya wengine. Kujifanya bora zaidi kuliko wengine mbele za Mungu, iwe kwa kunena au kutenda, Mungu amelikataza. Kumbuka:

"Mtoza ushuru na mfarisayo walienda kuomba. Mfarisayo alitazama juu mbinguni, akasema, tazama, mimi si kama huyu mtoza ushuru. Mimi nasali, natoa sadaka, nafunga mara 3 kwa siku. Lakini mtoza ushuru alipiga magoti, hakunyanyua hata macho juu mbinguni, akajipigapiga kifua chake, akasema, mimi ni mwenye dhambi. Naomba unisamehe. Yesu akasema hakika huyu mtoza ushuru ndiye aliyesali"

Ibadani tunaenda kutafuta huruma ya Mungu, siyo kwenda kujionesha kuwa sisi ni tofauti au bora kuliko wengine. Tunamwachia Mungu, yeye ndiye ajuaye nani aliye bora zaidi katika ufalme wake.

Tukio alilolisema mleta mada, wa kulaumiwa ni hao watu wa protokali.
 
Back
Top Bottom