Na hapa Mimi natofautiana na wengi!
Samiah sio wa kuchukiwa hivyo!anatumikia mfumo uliomlea na alioukuta!!!
Alimuona Mzee mkapa akiwawaua Hadi watoto ambao walikua wanatoroshwa kwenda mombasa kama wakimbizi enzi zile wakazamishwa majini!
Mauaji ya mwembechai!!?
Kuna Rais ambaye hajaua watanzania wenzake kisa itikadi na sera!!?
Tulipoifanya siasa kama KAZI ya mapesa mengi kuliko usomi na ueledi ndipo tulipozalisha mauaji na umwagikaji damu muuonao Hadi leo!!
Mtu hawezi muua mwenzake ili apate masters degree au diploma au Ili awe Mwalimu!
Bali anaweza muua mtu kisa itikadi au tishio kwenye nafasi ya kisiasa aliyonayo!!
Amkeni,hata kama ungekua wewe na umepewa jukumu la kukivusha chama,huwezi kivusha bila kuua wanaharakati was kitikadi ndani na nje ya chama!!
Samia Suluhu Hassan binafsi nje ya taasisi ya urais ana haki zake zinazoathiriwa sana na hali hii.
Siasa mbaya, zilizojengeka muda mrefu, kwa sababu ya watu wengi waovu kushiriki zilifikia kilele (chaweza kuwa kidogo, bado vingine) wakati wake.
Kwa mtazamo mpana, lawama hazitakiwi kuelekezwa kwa Rais pekee, zianzie chini kwa mjumbe hadi taifa.
Wote wanaoshiriki kwa nafasi zao wajirekebishe kwa mustakabali mwema wa taifa.
Kila mmoja ana wajibu wa kufanya kuweka mambo sawa.
Ni vizuri kuanzia kwa kuwaweka watu wenye akili nzuri na utu kuanzia chini.
Uovu huanzia chini, kule juu ni matokeo tu.
Vyama vya siasa, mashirika ya siyo ya kiserikali, taasisi za dini, vikundi vya kijamii...vianze kampeni za kutambua watu wema na waendelezwe.
Wezi wa kura, wauaji na waovu wote wapo kwenye jamii na wanakaa viti vya mbele, kuheshimiwa makanisani na misikitini.
Watu waovu hawapo CCM pekee, wapo pia kwenye vyama vya upinzani (hawajapata madaraka), wapo kwenye utumishi wa Uma (wanaofanya na kufanikisha uovu), kwenye dini na jamii nzima.
Kazi iliyo mbele yetu ni kuchukua hatua za kupunguza uovu huo kwa faida ya taifa na vizazi vijavyo.
Kupambana na Rais kwa kuelelekeza fikra na nguvu zote ni chembe tu ya tatizo lenyewe.
Ukiwa na watu wote wazuri huwezi pata viongozi wabovu.