Haya ni maajabu!! Rais anashinda ndani kama utumbo?!!

Samia Suluhu Hassan binafsi nje ya taasisi ya urais ana haki zake zinazoathiriwa sana na hali hii.
Siasa mbaya, zilizojengeka muda mrefu, kwa sababu ya watu wengi waovu kushiriki zilifikia kilele (chaweza kuwa kidogo, bado vingine) wakati wake.
Kwa mtazamo mpana, lawama hazitakiwi kuelekezwa kwa Rais pekee, zianzie chini kwa mjumbe hadi taifa.
Wote wanaoshiriki kwa nafasi zao wajirekebishe kwa mustakabali mwema wa taifa.
Kila mmoja ana wajibu wa kufanya kuweka mambo sawa.
Ni vizuri kuanzia kwa kuwaweka watu wenye akili nzuri na utu kuanzia chini.
Uovu huanzia chini, kule juu ni matokeo tu.
Vyama vya siasa, mashirika ya siyo ya kiserikali, taasisi za dini, vikundi vya kijamii...vianze kampeni za kutambua watu wema na waendelezwe.
Wezi wa kura, wauaji na waovu wote wapo kwenye jamii na wanakaa viti vya mbele, kuheshimiwa makanisani na misikitini.
Watu waovu hawapo CCM pekee, wapo pia kwenye vyama vya upinzani (hawajapata madaraka), wapo kwenye utumishi wa Uma (wanaofanya na kufanikisha uovu), kwenye dini na jamii nzima.
Kazi iliyo mbele yetu ni kuchukua hatua za kupunguza uovu huo kwa faida ya taifa na vizazi vijavyo.
Kupambana na Rais kwa kuelelekeza fikra na nguvu zote ni chembe tu ya tatizo lenyewe.
Ukiwa na watu wote wazuri huwezi pata viongozi wabovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…