Hayati Magufuli alifanikiwaje kuwafanya watu wa vipato vya chini kumuamini kiasi kile?

Hayati Magufuli alifanikiwaje kuwafanya watu wa vipato vya chini kumuamini kiasi kile?

Wewe ndiyo duni. Nenda Botswana uone madaktari wa kitanzania wanavyoaminika kwa ubora kuliko madaktari wa nchi nyingine.
Hao Madaktari ni zamani siku hizi nao wamesoma. Hiyo braindrain ya Madaktari ilikwenda Botswana kati ya 1985 na 2000. Baada ya hapo hakuna tena kwa kuwa hata working permits zikawa ngumu kutokana na fact kwamba WaTswana nao wakawa wameshasoma. Nina class mates wangu 4, ninajuwa hili
 
Hivi unadhani hatujui vitisho vinavyoendelea huko vijijini? Kinachokufanya ccm iogopwe au kujifanya inapendwa ni mifumo ya vitisho huko vijijini, na sababu hasa ni watu kujengewa hofu. Alipoingia Magu madarakani akashurutisha kueneza hofu hiyo nchi nzima. Hii ndio iliyopelekea mapenzi bandia kwake na chama chake.
Mara hao watu ni wajinga mara tena wanatishwa sasa nikuelewa lipi?
 
Njia ni rahisi tu.

Masikini wengi wana roho mbaya, wivu na akili ndogo hivyo:

Kwasababu huwa wana wivu na chuki kwa kila aliyenacho, wewe hakikisha unatukana kila siku mwenye nacho na kuwadhalilisha hadharani huku ukiwasifia wao masikini.

Tukana sana wazungu. Na hakikisha wakikupa pesa zao, hao masikini wasijue.

Dhibiti habari zote za mabaya yako, hakikisha unasifuwa na kutangazwa muda wote kwenye vyombo vya habari kwa mema tu.

Jifanye mcha mungu, na kila ukienda kwenye ibada hakikisha watu wanajua na picha zinatoka ukiwa mnyenyekevu.

Ukimsaidia ombaomba hata Jero hakikisha unachukua picha na video na zinaruka kila wakati kwenye TV ili kukuonesha ulivyo mwema .

Kila ukiongea na tajiri au mwenye cheo hakikisha unamfojea LIVE kwenye TV ili watu waone.
Halafu wanaojiona masikini huwa hayana information nimeupe sana kichwani kiasi cha kushindwa kureason na kutafuta uhusiano wa mambo kwa undani na uhalisia wake
 
Blaza usiandike propaganda za kitoto bila ushahidi.

Kama ni kuongeaonga tu hata mimi naweza kujisemea.

Kwa nini msiende kumkamata ili asaidie polisi maana sasa ni raia tu.

Acha majungu mitandaoni
Rudi kwenye akili zako, usijidhalilishe kuandika vitu ambavyo huna uwezo navyo. Makonda alitumwa na Magufuli kumshambulia Lissu.

Polisi unaotaka twende tukashtaki walikuwapo Dodoma na ndiyo waliohusika kutoa CCTV Cameras kwenye nyumba za mawaziri na wabunge pale Area D. Na hawakushika mtu hata mmoja kwa mashambulizi yale

Bado Serikali ni ya CCM iko madarakani ambayo Magufuli alikuwa ndiye Mwenyekiti wake na Rais na aliyetoa maagizo.

Ubalozi wa USA ulimsitishia Makonda kuingia nchini kwao kwa kuwa anatuhumiwa "kusitisha haki ya kuishi"ya Watanzania wengine.

Sasa kama huelewi mpaka hapa, sijui mitihani shuleni kwako ulipasi vipi?

All in All, Jinai haizeeki, iko siku au kutakuwa na Utawala wa Sheria au Chama cha upinzani kitaongoza Tanzania ndiyo utayaona mashtaka ya Makonda Mahakamani/Polisi
 
Jamaa alikuwa genius wa kufanya manipulation hatari, alaf anaongea kana kwamba ana uchungu kweli na kiukwel hamna alichowafanyia kikubwa.... Mwamba alikuwa mhuni Sana Yule
Huwa naikubali sana Spirit ya Mwamba.. wazungu wanasema it doesn't matter what you say.. but "How you say".. huyu Mwamba apa alipapatia sana.. simkubali sana ila apa alitushika.

Mwamba anakuambia.. "mimi ni mtumishi wenu, nimesacrifice maisha yangu kwa ajili ya watanzania masikini ".. HUwa nikiisikiliza hii nagundua JPM was a master mind.. a Conman na Mwamba mmoja mwenye ushawishi kwa kundi lililo kubwa.
 
Njia ni rahisi tu.

Masikini wengi wana roho mbaya, wivu na akili ndogo hivyo:

Kwasababu huwa wana wivu na chuki kwa kila aliyenacho, wewe hakikisha unatukana kila siku mwenye nacho na kuwadhalilisha hadharani huku ukiwasifia wao masikini.

Tukana sana wazungu. Na hakikisha wakikupa pesa zao, hao masikini wasijue.

Dhibiti habari zote za mabaya yako, hakikisha unasifuwa na kutangazwa muda wote kwenye vyombo vya habari kwa mema tu.

Jifanye mcha mungu, na kila ukienda kwenye ibada hakikisha watu wanajua na picha zinatoka ukiwa mnyenyekevu.

Ukimsaidia ombaomba hata Jero hakikisha unachukua picha na video na zinaruka kila wakati kwenye TV ili kukuonesha ulivyo mwema .

Kila ukiongea na tajiri au mwenye cheo hakikisha unamfojea LIVE kwenye TV ili watu waone.
Masikini wana Roho Mbaya sana.. Ndoto zao Tajiri afilisike waungane nae
 
Uliwaona wapi boss?
Ama kwa zile nguvu za yule mwovu?
Ni tajiri gani aliyewahi hata kuwekwa mahabusu kwasababu za kumyanyasa masikini?

Mimi nawajua masikini wengi waliofungwa, kutekwa, kuuawa, kufungwa kwenye viroba, na kutishiwa bastola.
 
Jana maeneo ya matumbi matraffic wakiwa wametanda kila kona, Dereva wa daladala alipowaona tu akasema " Baba yetu amefariki sasa wameanza kutusumbua".

Kauli kama hizi zimekuwa zikisikia kwa watu wa vipato vya chini kuona kama hayati alikiwa ndio kila kitu. Na sasa hivi kila rekebisho linalotokea na litakalotokea inaonekana ni kwa sababu mtetezi wao hayupo.

Hizo mbinu alizotumia kuteka mashabiki wengi kuliko wafuasi wa chama chake ni zipi na kwa nini wabunge, madiwani na serikali za mitaa walishindwa kututeka hivyo miaka yote?

Angalau Deo Filikunjombe na yeye alifanikiwa kwa kiasi flani.

Nawasilisha
Umenikumbusha Deo Flukonjombe
 
Jamaa alikuwa genius wa kufanya manipulation hatari, alaf anaongea kana kwamba ana uchungu kweli na kiukwel hamna alichowafanyia kikubwa.... Mwamba alikuwa mhuni Sana Yule
Hamtokaa mfanikiwe.
 
Alichokuwa anakifanya ni kupunguza gap kati ya walionacho na wasiokuwa nacho( jambo ambalo ni jema tu). Sasa changamoto ikawa kwamba wenye nacho ambao ni wachache wakahisi wanaonewa dhidi ya wanaoitwa wanyonge.
Ikitokea rais aliepo akajikita zaidi kwa walionacho basi itakuwa vice versa.
 
Magufuli alikuwa kipenzi cha wengi.
Hili swala hawa mabwanyenye wenye pesa za kulipa watu kumtukana mitandaoni hawataki kuliamiani, JPM alipendwa sana na hayupo ataetokea, tunajua wanaogopa mama akipita mlemle na kutuaminisha kweli ni pro JPM mission yao itakuwa imefail, wako busy kumtikisa.
 
Tulibakia hatua chache tu kuelekea kwenye Civil Unrest,

Magufuli was a perfect solution at the time.

Hii ligi hata huko kwa mabeberu ipo

Na fimbo inayotumika ni punguzo la kodi.

Kikiingia chama flani kinawajali wanyonge (democrats/america)

Kikiingia kingine kinawajali mabeberu halisi (republican/america).

Ni ligi endelevu.
 
Hapo kwenye kuchezewa naamini hata wewe mwenyewe upo kwenye kundi hilo ni vile tu ushabiki umekuganda kichwani....kufata mkumbo wa kumtusi hayati kwa wewe unaeshinda humu JF kutwa nzima unaama majukwaa ni ulimbukeni pia maana wenye bifu la kweli na Hayati hawana muda wa kupoteza kuchati chati humu zaidi zaidi wapo busy kuspare na kufix mianya yao ya kuludisha dili za mabilions of money....endelea kujitathmini mkuu.
We lofa kweli mbona unataka kujifanya kama unanijuwa sana? Chukua time hata nishinde 24/7 hapa JF huwezi nipangia chakufanya .sawa?
 
Jana maeneo ya matumbi matraffic wakiwa wametanda kila kona, Dereva wa daladala alipowaona tu akasema " Baba yetu amefariki sasa wameanza kutusumbua".

Kauli kama hizi zimekuwa zikisikia kwa watu wa vipato vya chini kuona kama hayati alikiwa ndio kila kitu. Na sasa hivi kila rekebisho linalotokea na litakalotokea inaonekana ni kwa sababu mtetezi wao hayupo.

Hizo mbinu alizotumia kuteka mashabiki wengi kuliko wafuasi wa chama chake ni zipi na kwa nini wabunge, madiwani na serikali za mitaa walishindwa kututeka hivyo miaka yote?

Angalau Deo Filikunjombe na yeye alifanikiwa kwa kiasi flani.

Nawasilisha
Ushawahi kuona wale ndondocha wa kwenye maduka ya wahindi, uwa wako royal sana kwa maboss wao wakati hakuna wanachopata wala hawawezi kuwa na maisha ya maana.
Ukitaka mtu awe royal sana kwake, mfanye awe maskini zaidi, mfanye asijue haki zake, mtengenezee propaganda kuwa flani ndiye adui yake. Mfano umaskini wake umesababishwa na mabeberu wakati ni chama tawala kilichipo madarakan toka uhuru lakini limeshindwa kymanage resources.
Chagua mmoja kati yao piga naye picha mpe laki moja, maskini watakuona wewe mtu wa maana sana hadi unapiga nao picha
 
Jana maeneo ya matumbi matraffic wakiwa wametanda kila kona, Dereva wa daladala alipowaona tu akasema " Baba yetu amefariki sasa wameanza kutusumbua".

Kauli kama hizi zimekuwa zikisikia kwa watu wa vipato vya chini kuona kama hayati alikiwa ndio kila kitu. Na sasa hivi kila rekebisho linalotokea na litakalotokea inaonekana ni kwa sababu mtetezi wao hayupo.

Hizo mbinu alizotumia kuteka mashabiki wengi kuliko wafuasi wa chama chake ni zipi na kwa nini wabunge, madiwani na serikali za mitaa walishindwa kututeka hivyo miaka yote?

Angalau Deo Filikunjombe na yeye alifanikiwa kwa kiasi flani.

Nawasilisha
Aliwaaminisha kuwa amesakrifaisi maisha yake kwa ajili yao...such a stunt
 
Back
Top Bottom