Hayati Magufuli alifanikiwaje kuwafanya watu wa vipato vya chini kumuamini kiasi kile?

Hayati Magufuli alifanikiwaje kuwafanya watu wa vipato vya chini kumuamini kiasi kile?

Aliyekupa Utajiri Wewe ndiyo huyo huyo aliyenipa Mimi Umasikini tatizo liko wapi na kwanini unateseka na hali yangu? Nimeshakuja Kukupigia Hodi Kwako kukuomba hata tu Makombo ya Ugali na Maharage yako?
Aliyenipa utajiri ni nani?
Mambo ya mtu kuwa supper ni kufanya kazi kwa bidii na kutumia akili. Sasa wewe (na wenzako) mnajiita wanyonge, masikini nk halafu mnatupa lawama kwa wengine?
Huyo mliyekuwa mnamwabudu kwa taarifa yako alikuwa mwizi hakuna mfano. Mwenye wivu, mshamba, kiburi nk. We baki na ulivyo
 
Jana maeneo ya matumbi matraffic wakiwa wametanda kila kona, Dereva wa daladala alipowaona tu akasema " Baba yetu amefariki sasa wameanza kutusumbua".

Kauli kama hizi zimekuwa zikisikia kwa watu wa vipato vya chini kuona kama hayati alikiwa ndio kila kitu. Na sasa hivi kila rekebisho linalotokea na litakalotokea inaonekana ni kwa sababu mtetezi wao hayupo.

Hizo mbinu alizotumia kuteka mashabiki wengi kuliko wafuasi wa chama chake ni zipi na kwa nini wabunge, madiwani na serikali za mitaa walishindwa kututeka hivyo miaka yote?

Angalau Deo Filikunjombe na yeye alifanikiwa kwa kiasi flani.

Nawasilisha
Kwa kutumia kikundi cha watu wasiojulikana na propaganda ya kuwapigania wanyonge
 
Usichanganye mambo, ukweli ni kuwa Magufuli alipendwa na wajinga na watu waliokuwa na maslahi binafsi na madaraka yake. Mara nyingi watu wajinga hawajiulizi mambo kwa kina, wao inatakiwa uwatangazie jambo lako bila kujali ukweli wa jambo hilo,na kulirudia mara kwa mara. Tangazo likijirudia mara kwa mara, mjinga hana uwezo wa kuling'amua.
Sasa mimi nimechanganya mambo gani? ni uongo kwamba watu huko vijijini wanaishi maisha ya ufukara ila bado wanaipenda ccm hadi leo? na hiyo kabla hata ya Magufuli.
 
Jana maeneo ya matumbi matraffic wakiwa wametanda kila kona, Dereva wa daladala alipowaona tu akasema " Baba yetu amefariki sasa wameanza kutusumbua".

Kauli kama hizi zimekuwa zikisikia kwa watu wa vipato vya chini kuona kama hayati alikiwa ndio kila kitu. Na sasa hivi kila rekebisho linalotokea na litakalotokea inaonekana ni kwa sababu mtetezi wao hayupo.

Hizo mbinu alizotumia kuteka mashabiki wengi kuliko wafuasi wa chama chake ni zipi na kwa nini wabunge, madiwani na serikali za mitaa walishindwa kututeka hivyo miaka yote?

Angalau Deo Filikunjombe na yeye alifanikiwa kwa kiasi flani.

Nawasilisha
Hata wakati Idi Amin anafukuza wahindi,maskini weusi walishangiria,kwa kuwa waliaminishwa Wahindi ndio wamesababisha wao wawe maskini.
Jiwe alikuwa ana makelele tu,anamuita Mkurugenzi,mwenye maisha yake bora,anaeishi masaki kwenye jumba la kifahari,anaendesha V8,harafu anamuuliza maswali ya kijinga mbele ya wananchi mafukara,jamaa akitumbuliwa,mafukara wanafurahi,wanaona huko aliko anafaidi,bora atumbuliwe aje chini,tupigike wote.
Waliokuwa wanafurahi ni kada ya chini sana,mama ntirie,bodaboda,machinga,watu wa middle class,wasingeweza kufurahia ujinga huo.
 
Watawala wote wajamaa waliopita waliamini hivyo kwamba kuwa masikini ndio uzalendo.Utajiri ni wizi ni ufisadi KILA aliyefanikiwa kaiba,thus awamu zao nadharia za uhujumu uchumi huwa wimbo wa taifa hali kiuhalisia ni athari za malezi yao ya dhiki utotoni yameathiri medula zao.
Ila ndio hao hao mnasema wanajilimbikizia mali kwamba mafisadi.
 
Nimetoka kuangalia taarifa ya habari Channel 10 wafanyabiashara wanyonge wa soko kuu kariakoo wanalalamika wanatolewa kwenye sehemu zao na kuwekwa wenye uwezo. Kweli ndio maana wengine umasikini hawautaki maana full kunyanyaswa.
 
Sasa mimi nimechanganya mambo gani? ni uongo kwamba watu huko vijijini wanaishi maisha ya ufukara ila bado wanaipenda ccm hadi leo? na hiyo kabla hata ya Magufuli.

Kupendwa na wajinga hakukupi sifa kuwa ulichokuwa unafanya ni kizuri ama sahihi, hasa wajinga hao wanapokuwa wanafanya hivyo kwa mazoea, upotoshwaji na hofu.
 
Baada ya Rais Mstaafu Kikwete kutoka Madarakani Matajiri walikuwa na Jeuri za kila aina mpaka Kuamua Uhai wa Watu Masikini na wasifanywe lolote lile kwani walimweka Mifukoni mwao.

Alipoingia Hayati Rais Dkt. Magufuli alitaka Kuwaheshimisha Masikini (GENTAMYCINE nikiwemo) kuwa hata Sisi pia ndani ya hii Ardhi ya Mama Tanzania pia tuna Thamani yetu hivyo akatupa (akatujaza) Jeuri mpaka Matajiri nao wakaanza Kutunyari (Kutuogopa)

Kwa hivi sasa ndani ya huu Utawala wa Rais Mama Samia Matajiri na Masikini bado tunamsikilizia (tunampima) Mama tuone Yeye atalia upande wowote ili tuanze Kumlaumu (Kumsiliba) japo ninavyomuona ni kama vile anataka kutuweka katika Mzani sawa kitu ambacho si kibaya pia na Mimi nakiunga mkono.

Kwani maskini nyie hamna mpango wa kupambana na kuwa matajiri kama hao matajiri?
 
wewe mjinga ni mnafiki sana.

ile kamptula yako nyingine unaitumia vibaya sana.
 
Kupendwa na wajinga hakukupi sifa kuwa ulichokuwa unafanya ni kizuri ama sahihi, hasa wajinga hao wanapokuwa wanafanya hivyo kwa mazoea, upotoshwaji na hofu.
Ndio nasema kwamba kabla ya Magufuli hao watu walikuwepo na hawakuwa wakitishwa wala nini pamoja na yote ila bado wanaipenda ccm.

Hao wajinga ni kwa sababu ya kuipenda ccm tu ila wajinga hao pamoja na ujinga wao wakishabikia mfano labda chadema hawaonekani tena wajinga.
 
Alikiuwa anawaambia wao ni wanyonge na kwamba wamechezewa sana? Halafu anamalizia na kumtumbua afisa mmoja wa karibu aliyepo hapo wananchi weweeeeeeee.[emoji2223][emoji2223][emoji2223][emoji2223][emoji2223]
Hapo kwenye kuchezewa naamini hata wewe mwenyewe upo kwenye kundi hilo ni vile tu ushabiki umekuganda kichwani....kufata mkumbo wa kumtusi hayati kwa wewe unaeshinda humu JF kutwa nzima unaama majukwaa ni ulimbukeni pia maana wenye bifu la kweli na Hayati hawana muda wa kupoteza kuchati chati humu zaidi zaidi wapo busy kuspare na kufix mianya yao ya kuludisha dili za mabilions of money....endelea kujitathmini mkuu.
 
Kwani maskini nyie hamna mpango wa kupambana na kuwa matajiri kama hao matajiri?
Sasa wote watakuwa matajiri? masikini lazima wawepo ili watumikishwe na hao matajiri waweze kutajirika zaidi.
 
Ni kweli watu wanaemchukia jpm wanaembeza na kumkashfu kwenye mitandao wako katika kundi hili Vyeti feki, watumishi hewa, wauza madawa ya kulevya, watakatishaji fedha, wanasiasa wafitini waliopoteza majimbo kutokana na kasi za maendeleo ya JPM, wakwepa kodi, wonyonyaji, majambazi, wala rushwa na mafisadi na wanajifanya wao ndio wananchi walioonewa na serikali ya JPM.
Tutake radhi kwanza mkuu,,,ila inawezekana na ww ni mnyonge wa mwenda zake alikunyonga mpaka akili fupi tyu zakufkilia
 
Jibu rahisi.Alijinasibu wazi kuwa yeye ni Rais wa wanyonge.

"Kazi hii ni ngumu"
"Tumechezewa sana nchi hii"
"Msiwasumbue mama ntilie na machinga, kitambulisho cha 20,000 kinatosha. Wafanye biashara kokote"
"We're in a right track"
"Niombeeni kwa Mungu"
"iiiiiiiiiii.....Ahaaaa"

Hizo ni baadhi ya kauli zake zilizomzolea mtaji wa watu wa hali ya chini.
Kumbe yy ndo anawachezea [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa alikuwa anawafanyia manipulation ya hatari, na kiukwel hamna alichowafanyia kikubwa.
Umasikini,unyonge Mara nyingi...huambvatana na roho lmbaya,chuki,husda nk!
Jiwe alitahidi na kufanikiwa kuwaamnisha hili kundi kuwa ..wanaonewa ,Kuna somebody somewhere ndio chanzo Cha umasikini na unyonge wao!
Hapo ndipo alipokuwa anawatumbua watu na akaonekana ni mkombozi!
 
Ndio nasema kwamba kabla ya Magufuli hao watu walikuwepo na hawakuwa wakitishwa wala nini pamoja na yote ila bado wanaipenda ccm.

Hao wajinga ni kwa sababu ya kuipenda ccm tu ila wajinga hao pamoja na ujinga wao wakishabikia mfano labda chadema hawaonekani tena wajinga.

Hivi unadhani hatujui vitisho vinavyoendelea huko vijijini? Kinachokufanya ccm iogopwe au kujifanya inapendwa ni mifumo ya vitisho huko vijijini, na sababu hasa ni watu kujengewa hofu. Alipoingia Magu madarakani akashurutisha kueneza hofu hiyo nchi nzima. Hii ndio iliyopelekea mapenzi bandia kwake na chama chake.
 
Back
Top Bottom