Kwanza nakupongeza mtoa mada kwa kujua kuwa utendaji Bora wa raisi unatakiwa upimwe kwa kigezo Cha utendaji waJPM, na hivyo haujamlinganisha mama na Marais wengine.
Nikukumbushe kuwa miezi mitatu ya mwanzo ya JPM, alikwisha ongeza makusanyo zaidi ya billion 500
Mama ni billion 40 za tozo
Billion 500 angepeleka kwenye ujenzi wa vituo vya afya angejenga vituo zaidi ya 1000 kila mwezi
Mapato hayo yalienda maeneo mbali mbali Kama elimu bure, posho za madaraka, ununuzi wa ndege, madawa hospitali, vifaa vya tiba vya mabilion ya fedha n.k
Kupanga ni kuchagua, billion 40 mama amepeleka kwenye ujenzi wa vituo vya afya
Miezi mitatu mama amepambania chanjo na diplomasia
Miezi mitatu baba alipambania uadilifu maofisini, kukata mirija ya unyonyaji, na mengineyo
Kuhusu kupanua wigo wa mapato tulimuona baba akifanya uboreshaji mkubwa wa bandari, ndege, reli, tanesko, bwawa la umeme, kuboresha mifumo ya ukusanyaji ya TRA, ambayo mama anavitegemea
Kuhusu kupanua wigo wa mapato tumemuona mama akiongeza tozo mbalimbali
Tutamsifu mama akifanya vizuri
Ila kumzidi JPM, bado saana
Viva JPM
Maendeleo hayana chama