Hayati Magufuli alijenga vituo vya afya 44 kwa miaka mitatu, Rais Samia anajenga 220 kwa miezi mitatu

Hayati Magufuli alijenga vituo vya afya 44 kwa miaka mitatu, Rais Samia anajenga 220 kwa miezi mitatu

Mama yupo very strategic kuliko anavyoonekana. Anawajua wabongo wengi wanaangalia kurasa ya juu kabisa sio wazuri kusoma kilichoandikwa kurasa za ndani.

Gwaji Boy oyeeeee
kabisa mkuu!
kwa alichokifanya jana nimemuelewa sana yaani! kumtumia gwajima kihekima vile ni jambo linalohitaji pongezi kwakweli........nimeanza kung'amua kitu kwa huyu mama, ngoja uone!!! yaani akishirikiana vema na wasaidizi wake huyu, tutasimulia!
 
Kwanza nakupongeza mtoa mada kwa kujua kuwa utendaji Bora wa raisi unatakiwa upimwe kwa kigezo Cha utendaji waJPM, na hivyo haujamlinganisha mama na Marais wengine.

Nikukumbushe kuwa miezi mitatu ya mwanzo ya JPM, alikwisha ongeza makusanyo zaidi ya billion 500

Mama ni billion 40 za tozo

Billion 500 angepeleka kwenye ujenzi wa vituo vya afya angejenga vituo zaidi ya 1000 kila mwezi

Mapato hayo yalienda maeneo mbali mbali Kama elimu bure, posho za madaraka, ununuzi wa ndege, madawa hospitali, vifaa vya tiba vya mabilion ya fedha n.k

Kupanga ni kuchagua, billion 40 mama amepeleka kwenye ujenzi wa vituo vya afya

Miezi mitatu mama amepambania chanjo na diplomasia

Miezi mitatu baba alipambania uadilifu maofisini, kukata mirija ya unyonyaji, na mengineyo

Kuhusu kupanua wigo wa mapato tulimuona baba akifanya uboreshaji mkubwa wa bandari, ndege, reli, tanesko, bwawa la umeme, kuboresha mifumo ya ukusanyaji ya TRA, ambayo mama anavitegemea

Kuhusu kupanua wigo wa mapato tumemuona mama akiongeza tozo mbalimbali

Tutamsifu mama akifanya vizuri
Ila kumzidi JPM, bado saana


Viva JPM
Maendeleo hayana chama
 
Kuna tofaut ya kukamilisha na kujenga, vingi vilianza kujengwa enzi zile
 
Sawa kwa kesi ya kulipa kwa fedha za nje pengine unaambiwa tuu acha na wanaacha
Vipi sasa kuhusu hiyo hasara?? Yaani kwa kila pesa iliyozidi rate ya makubaliano; unakuta inafika hta billion kadhaa kwa mwaka!!

Tuseme tu ukweli pesa zinaliwa kimtandao ndio maana wanalindana kuanzia hazina mpaka halmashauri ukizingatia hao hao pia wapo kwenye chama so inakua ngumu kuwashughulikia ila sijui Kusema CAG report sio conclusive ni kukimbia tu ukweli sote tunaoufahamu
 
Unapora hela za watu kuoitia tozo...afu nn
 
Rais kikwete hakunenga vituo vya afya, bali serikali ilijenga, Magufuli hakujenga, bali Serikali, Samia hatajenga, bali serikali ndio itayojenga. Hv why mnapenda kutajana majina hivi? Na mama naye kakubali kuandikwa hivi, kweli??
Bado tuna muda wa kujisahihisha. Acheni kusifia masuala ambaye hayana sababu.
 
Unasema Magufuli alijenga vituo 44 wakati kwenye Tv kulikua na matangazo ya vitu 1000+ na picha za vifaa vilivomo kwenye hivo vituo[emoji23][emoji23][emoji23] huyu naye akitoka tutakuja kusikia alijenga vituo 5 tuuu
 
Mkuu hawa maccm ni waongo sana. Kumbuka uongo wa dhalimu kwamba alijenga viwanda zaidi ya 4,000. Ukiwauliza vimejengwa wapi na vimeajiri Watanzania wangapi wanang’aa macho.
Hivyo vituo vimejengwa wapi na wapi?
 
Weka jedwali kuonyesha mkoa, wilaya tarafa na kata kituo kilipo, pamoja na thamani yake. Usisahau kuweka tarehe ya kituo kuanza. Kinyume na hapo kadanganyeni waliolala usingizi mzito.
 
Bado unaamini kuna watu wanaamini hizo propaganda mfu?Kusanyeni hela kulipa madeni ya Magufuli.

1. Huduma za jamii zitaboreshwa
2. Ajira mpya serikalini zitaongezeka
3. Mzunguko wa fedha utarejeshwa kwa wananchi kupitia mishahara/ ujenzi wenyewe / ajira / vibarua na manunuzi.
4. Kutanuka kwa huduma za ziada usafirishaji / fedha (Banking / mobile money services)


Uzuri Tozo hizi hazipelekwi kujenga madarasa Sudani Kusini ni humuhumu nchini.
 
Mbona alichokisema mtoa mada na kilichopo ktk attachment yake ni vitu viwili tofauti?au mtoa mada hajui kusoma vzuri?

Ukurasa wa 24...8783-7014 = 1769 in total.

Ufanauzi Ukurasa wa 23...
Zahanati = 1198,
Vituo vya afya = 487
Hospitali za Wilaya = 71
Hospitali za Mikoa = 10
Hospitali za rufaa = 3
TOTAL = 1769

Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni
 
Mkuu hawa maccm ni waongo sana. Kumbuka uongo wa dhalimu kwamba alijenga viwanda zaidi ya 4,000. Ukiwauliza vimejengwa wapi na vimeajiri Watanzania wangapi wanang’aa macho.
Hapa kuna dalili za upikaji data maana wanajua watanzania wengi sio wafatiliaji
 
Huyu Mama anapingo sana, Kama atakuwa makini wasimpige basi huenda akawa Rais wa mfano duniani,

2025 tunakula kwa Lissu tunalala kwa Mama,
Na Hilo gaidi walipige mvua maisha ili awe rais wa mfano duniani.
 
Yaani waja hapa na ujinga wako kusema raisi Samia amejenga vituo vya afya 220 kwa miezi mitatu?

Huoni haya haya kuketi kitako kuleta hizi "cooked stuff"?

Hivyo ni vituo vya afya au vibanda vya afya?

Kwa sasa mmeng'amua kuwa watanzania wengi hawatilii maanani ufisadi wenu sasa mnatumia ujinga wao kama mtaji wa kuwaghiribu.

Au kwa kiingereza inasemwa "you are using your people ignorance so you can exploit them better".

Na huu ni uthibitisho wa mnachokifanya.

Shame on you.
 
Vipi sasa kuhusu hiyo hasara?? Yaani kwa kila pesa iliyozidi rate ya makubaliano; unakuta inafika hta billion kadhaa kwa mwaka!!

Tuseme tu ukweli pesa zinaliwa kimtandao ndio maana wanalindana kuanzia hazina mpaka halmashauri ukizingatia hao hao pia wapo kwenye chama so inakua ngumu kuwashughulikia ila sijui Kusema CAG report sio conclusive ni kukimbia tu ukweli sote tunaoufahamu
Technically mambo mengine huwa yanakuwa influenced na mambo ya chama ,unakuta hizo pesa zinapelekwa kusaidia chama kinyume na utaratibu ndio maana unakuta huwezi ku msite mtu mmja,ni kama ile ksmpuni ya kuweka pigment kwenye mafuta.

Nadhani CAG aendelee kuibua tuu
 
Mbona alichokisema mtoa mada na kilichopo ktk attachment yake ni vitu viwili tofauti?au mtoa mada hajui kusoma vzuri?

Ukurasa wa 24...8783-7014 = 1769 in total.

Ufanauzi Ukurasa wa 23...
Zahanati = 1198,
Vituo vya afya = 487
Hospitali za Wilaya = 71
Hospitali za Mikoa = 10
Hospitali za rufaa = 3
TOTAL = 1769

Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni
Sawa ila kwa mda gani? Kumbuka hospital zote hazijaanza na ushahidi ninao so Rais ana mzigo wa kuzimalizia na zianze huduma na kujenga mpya.

Kimsingi kwa sasa kila wilaya imepata hospital za Wilaya Kazi ya mama ni vituo vya afya na zahanati .
 
Back
Top Bottom