Hayati Magufuli alipokuwa hai hakukuwa na uhaba wa mvua na ukame nchini kama sasa

Hayati Magufuli alipokuwa hai hakukuwa na uhaba wa mvua na ukame nchini kama sasa

Basi sawa mwanasayansi! Maana wewe ndo unajua sana! Dunia hii sio ya wanasayansi ni ya Mungu tena sio Mungu tu jina Mungu wa Ibrahim,Isaka,Yakobo na baba wa Bwana wetu Yesu kiristo!
Umeelewa,ubarikiwe sana.
 
Wanasema kila kitabu na zama zake. Lakini kweli utawala wa JPM ulikuwa na neema ya mvua. Sijui ni kwa mapenzi ya Mungu au alibebwa na majila.

Huyu mama sijajua Neema ya uongozi wake nini au ndiyo hili jua na joto!!
[emoji23][emoji23][emoji23]neema ya matetemeko ya ardhi kagera daah,kweli tunasahau mapema sana,HIZI CHANGAMOTO ZIPO KWENYE KILA AWAMU
 
Hali ya ukame (Dar kuna mgao wa maji) na joto tuihusishe na utawala wa sasa?

Je, utawala uliopo kwa sasa unatenda haki? Imeandikwa Mithali 29:2 Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua.
 
Mcha Mungu Magufuli alipokuwa hai hakukuwa na uhaba wa mvua na ukame nchini Kama sasa

Kuondoka tu mcha Mungu Magufuli nchi ukosefu wa mvua kila Kona ni ukame nchi nzima na tishio la njaa kila kona ya nchi hali ya hewa vipimo vyao vinaona ukame,ukosefu wa mvua na njaa tu inayokuja

Mwenyewe mcha Mungu angekuwepo haya yasingekuwepo

Serikali badala ya kuitisha maombi wanaenda kuhudhuria mkutano wa Mabadiliko ya Tabia nchi kuomba pesa kwa wazungu kwani pesa zaweza leta mvua msimu huu?

Magufuli angeshaitisha maombi ya kitaifa lakini kwa kuwa alikuwa mcha Mungu, Mungu alihakikisha kipindi chake mvua ipo ya kutosha ,ukame haupo na njaa haipo pamoja na yeye kutohudhuria mkutano wowote wa Mabadiliko ya Tabia nchi popote duniani.
kuna mikoa mvua bado inaendelea usikariri hata mwaka jana kuna mvua ilinyesha tarehe 13 october ambayo ilileta athari ya mafuriko na nyingine chache za mwezi april ambayo kiuhalisia hazikuwa mvua kama za miaka ya nyuma kama unakumbukumbu nzuri uhaba wa mvua umeanza tangu miaka ya 2013 na kama ni mkazi wa Dar siku nyingi utagundua miaka ya 90 ifikapo October kulikuwa hamna discussion mvua lazima zinyeshe ila kwa kuwa watu weusi hatunaga mambo ya Documentation ndo utasikia Magufuli kaondoka na Mvua

MVUA ZIMEANZA KUPUNGUA KITAMBO SANA NA WATAALAMU WA JIOGRAFIA wanajua sababu hasa ukiachana na Global Warming na pia achilia miji yenye joto kama Dubai, Dar es salaam ni mji mwingine utakaokuwa na sifa ya kijangwa hapo MBELENI.
 
Watu wengi wamepotea wewe,acha UZUZU! Zitto alitaja list ya watu 300 waliopetea kusini na pia Kigoma! Kuna wale waliokuwa wanatekwa Facebook,Twita na instagram na Kundi la kina DAB,Mwanaharakati huru hao nikna kanguye,gwanda,ben saa8 ,rwajabe ni wanajulikana kwenye jamii.

Ndugu za kuambiwa changanya na zako,sio kila kitu kinachosemwa na wanasiasa ni chakutilia manani vingine unaviacha vipite tu
 
Aisee watu mnasahau vibaya,
Hivi ushasahau tetemeko la Kagera mpaka ikaonekana kila la hovyo ni la wahaya.

Na mafuriko yale vp? Au ww shida kwako ni ukame tu.Hata hivyo haya ni majanga ya asili tu hayarelate na yeyote.
 
Baraka nazipokea ila nakwamnia neema ya mvua ni baraka kutoka kwa Mungu hata kama kutakuwa na mabadiliko ya tabianchi Mungu akiwa upande wetu tutakuwa na baraka tele ya vyakula!
Uko sahihi Wana wa Israel wakikula nyama choma jangwani kusiko na kware.Na mikate wakati Hakuna ngano kule jangwani Tabia nchi haikuwa na effect kwao
 
Magufuli asipokwenda motoni basi ujuwe hata huo moto wenyewe haupo wala Mungu hayupo.
 
Mabadiliko ya tabianchi (climate change) ni dunia nzima.Ndio maana UN ikaitisha mkutano wa kujadili kuhusu mabadiliko ya tabia nchi,na viongozi wa dunia nzima,wamekutana kwenye mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa COP26 ,karibia nchi 200 huko Glasgow,Scotland.
Achana na dunia Mungu alitupiganua barabara kipindi Cha Magufuli Hakuna ukame Wala njaa Wala ukosefu wa mvua kipindi chake .Kuna msemo kuwa ohh Tanzania ni nchi Maskini wakati Kuna mabilionea akina Bakhresa na akina Mo Dewji waliogoma kuwa sehemu ya hiyo sentensi ya kuwa Tanzania ni nchi Maskini

Kwenye swala la ukosefu mvua,ukame na njaa Tanzania tulijipambanua Kama peculiar kwenye huo ubwege wa global climate change hatukukosa mvua,hatukuwa na ukame Wala njaa kipindi chote Cha mcha Mungu Magufuli
 
Back
Top Bottom