Hii ndio hatari na tishio linalotokana na changamoto ya upumuaji

Hii ndio hatari na tishio linalotokana na changamoto ya upumuaji

Takwimu zingesaidia sana watu kuona ukubwa na uzito wa tatizo. Hakika mtu aliyezuia upimaji na utoaji wa takwimu ni muuji kama corona yenyewe.
Umsema kweli. Mimi nilikuwa nasema hata mwaka jana ule mlipuko wa kwanza walifariki watu wengi kabisa lakini kuna watu walikuwa wanabisha hapa. Huenda hata wengien wamekuja kupoteza watu wao kwa ubishi wao wa kijinga.

Tungekuwa tumekubali ukweli wa pigo la mwaka jana basi mwaka huu tungekuwa tumejifunza kitu. Badala yake mjinga mmoja akasema corona imeshaondoka kwa maombi.
 
Najitambua sana kiongozi,nipo against nyungu kwa sababu haina scientific evidence kuwa inatibu.Hakuna formula yoyote ya nyungu inayofahamika/documented anywhere in the world.Napinga unywaji wa pilipili kichaa,limao,tangawizi na vinginevyo vingi maana hakuna data za uhakiki wa ufanisi wake popote.
Watanzania tusiposema hapana kwa propaganda za kisiasa na kushika maelekezo ya WHO tunamalizika.
Hao wanasema vinatibu ni wajinga tu. Hivi vitu kama pilipili kichaa, limau na tangawizi mbona ni viungo vya kawaida vya vyakukla vinavyotumiwa kila siku na mataifa kama ya Asia!
 
Mimi nadhani ni vizuri zaidi kama watu wakajikita katika kutoa elimu ya jinsi ya kujikinga na gonjwa hili kuliko kutangaza vifo vya watu wa familia zingine,sijasema kutangaza vifo vya familia zingine haifai au inafaa ila elimu ya kujikinga na gonjwa hili ni muhimu zaidi,

Kama inawezekaza basi Mods wangeweka thd ya namna hiyo kama sticky thd.
Mkuu watu wanakufa mno.
Halafu mijinga iliyookotwa majalalani inalamba mafangasi ya jiwe na kusema ugonjwa watu hawafi.

A profesor anaongea utumbo.

Siyo swala la elimu tu, mkuu wa nchi atoke hadharani atoe tamko kua corona ipo Tanzania, inaua na watu walazimishwe kuvaa barakoa, kunawa, na kwenye mabasi level seat.
 
Hili watu hawalijui ,watu wakipata corona wanajikita kujifukiza na kutoangalia kupanda kwa sukari ambayo ni hatari zaidi ya korona.
Hivi mwenye tatizo la kisukari au presha akipata maambukizi ya korona na akafa na tukasema kilichomuua ni korona tutakuwa tumekosea?
 
Hivi wagonjwa wa Pressure na Kisukari zamani walikuwa wanakufaje? Hizi shida za kupumua zilikuwa haziwakumbi? Mbona tulikuwa hatusikii mialiko kama sasa hivi?
Pressure na kisukari vimeanza awamu ya tano. Nasema uongo ndugu zanguu
Hivi wagonjwa wa Pressure na Kisukari zamani walikuwa wanakufaje? Hizi shida za kupumua zilikuwa haziwakumbi? Mbona tulikuwa hatusikii mialiko kama sasa hivi?
 
Serikali ya Tz imepigwa baridi, jiwe anaogopa kusema ukweli kwa kuona aibu. Huyo jamaa yenu yuko tayari wote mfariki lakini kamwe hawezi kukiri kuwa corona ipo.
Ata akisema aitasaidia kitu zaidi ya kuzidisha HOFU
NB: akuna mbadala wa kukwepa kifo
 
Wewe unaendeleza yaleyale ya kuwaweka waTanzania gizani.
Kwa nini huhimizi watu wapimwe na pawe na takwimu kuhusu huu ugonjwa wa mlipuko, ikiwa kama sehemu ya kampeni ya kuelimisha na kujikinga!

Huko kuficha kunamsaidia nani, huyo aliyekana uwepo wa ugonjwa?
U.s.a wanapima wanatoa taharifa na wanachukua tahadhali zote imesaidia Nini.
 
Serikali inayokaa kimya watu wakiangamia inakosa utu. Kwa sasa baba anaweza kurudi nyumbani na ugonjwa akitokea safari ya mbali lakini kwa vile hakuna anayepima huyo naye anasambaza kwa familia nzima. Tukio la Profesa wa SUA mmeliona jinsi familia ilivyoteketea kwa Kutojua nani anao..
Mkuu nchi gani wamefanikiwa kupambana na Corona
 
Kuna ambao hata geti la Regency hawawezi kuingia maana hawatamudu hata Registration fee tu achilia mbali huduma.Huko tuendako hakutakuwa na SIRI tena!Hadi pale tutakapoipigia saluti COVID na kukubali miongozo ya kidunia badala ya kushabikia nyungu na malimao+pilipili+tangawizi etc.It's as if duniani kote hivyo vitu havipo.Vilevile kama hizo ni TIBA/kinga,kwa nini hatuithibitishii dunia ili nao wapone kama sisi?
Je,ni hiyo Ubinafsi,uchoyo na kukosa upendo dhidi ya binadamu wenzetu?
Tunaogopa chanjo ya CORONA ila pilipili kichaa tunakunywa tds,nani katuambia ni salama?Tujitafakari.
HOFU ni Jambo baya sana.
NB: akuna mbadala wa kukwepa kifo
 
Sasa hivi mataifa yote ambayo yana viongozi wenye akili na hekima, viongozi waliowekeza katika kutambua ukubwa wa tatizo, na kuweka jitihada katika kupambana, vifo vinazidi kupungua na maambukizi yanazidi kupungua. Lakini sisi tulio na uongozi usio na maono, maambukizi na vifo vinaongezeka.
Mkuu weka takwimu
 
Wagonjwa wa kisukari na presha huu ugonjwa ukikukaba masaa mawili ni mengi .....!!! Stay away
Ni kweli wagonjwa wa Sukari ugonjwa unawasumbua sana lakini sio kweli kuwa masaa mawili hawafiki , wanaweza kukaa hata wiki mbili na kupona. Muhimu kuwahi tiba mengine Mungu mwenyewe.
 
Wewe unaendeleza yaleyale ya kuwaweka waTanzania gizani.
Kwa nini huhimizi watu wapimwe na pawe na takwimu kuhusu huu ugonjwa wa mlipuko, ikiwa kama sehemu ya kampeni ya kuelimisha na kujikinga!

Huko kuficha kunamsaidia nani, huyo aliyekana uwepo wa ugonjwa?
Wapi nimeweka watu gizani? mimi nimehimiza elimu itolewe kutoka kwetu sisi member wa jf kupitia thd zetu,hayo ya kuhimiza watu wapimwe kwanini usihimize wewe? unataka kunipangia cha kuchangia humu?

JF is an open forums kila mtu anatoa maoni yake,ukiona una maoni tofauti ya mwenzako basi yaweke hapa hayo maoni/ushauri wako,

Hayo mambo ya kuambiana sijui kuweka watu gizani peleke huko kwenye vijiwe vyenu vya kahawa.
 
Back
Top Bottom