Hii ndio safari yangu ya Kigoma na niliyoyashuhudia

Hii ndio safari yangu ya Kigoma na niliyoyashuhudia

Safari yangu ilianzia Mwanza to Kigoma, then Kigoma to Dar...

Saa 12 asubuhi nilifika stand ya Nyegezi nikapanda gari moja maarufu linaitwa adventure, Mwanza kwenda Kigoma yapo magari maarufu kama Saratoga, adventure, yehova yille kati ya hayo hakuna gari lolote lile lenye unafuu magari ni 3 by 2, yaani upande mmoja watu watatu upande Mwingine wanakaa wawili, gari chache sana ni 2 by 2 na tajiri ndio anapanga lini likae barabarani...

Kwenye Ili gari picha inaanza hakuna customer care yoyote ile nilikata ticket ya mbele Kufika asubuhi nikaambiwa nikakae nyuma huko vurugu ikaanzia hapa ikabidi huyo mtu wampeleke huko nyuma.

Watu wachache walikosa seat wakasimama kuanzia Stand ya Nyegezi nakumbuka stand yoote tulipopita kuanzia Sengerema, Geita, Katoro nk watu walikua wanaingia na kusimama.

Humo ndani ya gari yalikua yanauzwa mahindi, mihogo, karanga vitumbua, mayai yaani tulikua tunapakia Muda wote non stop, story zinapigwa sana mtu wa seat ya mbele anapiga story na rafiki yake aliye seat ya nyuma, kweli waha ni kiboko.

Kufika Nyakanazi kundi kubwa la watu liingia yaani waliosimama ni wengi saana kuliko tuliokaa, nafasi hata ya kugeuka pembeni hupati mabegi yetu wengine tukawa tumebeba kichwani imagine hupo ndani ya gari Lakini begi lako umebeba kichwani..

Barabara ya lami inaishia Kakonko kwa mbele tukaanza kula vumbi mpaka Kibondo, wazee nimefika Kibondo pale mwili wote unauma Mwili mzima shingo haifanyi kazi tena, nikawauliza wenyeji wakanambia safari ya Mwanza to Kibondo ni karibu kuliko Jibondo tu Kigoma mjini, yaani Kibondo ni wilaya ambayo ni kubwa kuitembea ni mwendo wa masaa 4/5 Kufika Kasulu....

Raha ya kusema unasafiri usiitegemee kama unakuja Kigoma panda gari Ili ufike na sio u-enjoy nature, safari iliendelea tukafika mjini Kigoma saa 3 usiku.

NB: KIGOMA ni mji ambao una manispaa moja na town council inayoitwa Kasulu... Kigoma wanaishi watu kama watu wa mikoa mingine, Lakini Kigoma watu wa huku Kigoma Wana amini mno mambo ya kishirikina sio mdogo au mkubwa...

Kigoma Ujiji inapatikana Kigoma mjini. Huko ndio kwao Hashim Rungwe, Baruani Muhuza, Juma Kaseja huko ndio mji ulipoanzia, ni ngome ya kiislamu Watu wa huko ni masikini mno pia Kuna waganga wengi sana na mambo ya kichawi ni mengi mno, kukuta vyungu vimepasuliwa njia panda ni jambo la kawaida HAKUNA MTUMISHI YOYOTE WA SERIKALI ANAEKAA KIGOMA UJIJI, huko Hadi watoto wanajua uchawi ni nini kwenda kwa mganga ni jambo la kawaida.....huku Kigoma Ujiji harusi ni Kila siku huwezi pitisha siku hakuna harusi maisha magumu nyumba za udongo Lakini ni waswahili balaa, huko Ujiji maduka yanayokodisha mziki yanafika 40.

PALE KIGOMA MJINI.....ni center ndogo ya Kibiashara Lakini hakuna mzunguko wowote wa Hela Hapo wenyeji ni wengi na wengi wanauza kwa madawa usitegemee wa kuja ukafungua duka huku utapigwa zengwe mpaka uone moto.

Huu ni mji wa kinafiki, watu wanaishi kinafiki kinafiki saana, mvua zikinyesha unaomba Mungu radi zinapiga vibaya mno tena Kwa sauti kubwa sana.

Nilipapenda sana kigoma mjini hasa vyakula na beach,sema hapo kwenye safari ni majanga,ujiji ni uswahilini kumejaa masikini na wajinga.
 
Bukoba to kigoma ni mwendo wa masaa 13 Hadi 15...unatoa Bukoba saa 12 asubuhi unafika kigoma saa mbili usiku....

Kulinganisha Bukoba na kigoma ni mbingu na Ardhi..... Bukoba sasa wanachozidiwa na kigoma ni stendi ya mabasi ( japo naona siku hiz Bukoba nao wanajenga stendi yao) mambo mengine Bukoba ni superior kwa kigoma kuanzia makazi, Barabara, airport, elimu Hadi bandari bandari ya Bukoba inapanuliwa sana ikiwa ya pili kwa ukubwa Kanda ya ziwa

Kuna siku nilitoka bk to kgm,nmekuja kuingia kigoma sa4 usiku.
 
We bibi utakua na mtindio wa ubongo,waswahili ndio wamejaza ushenzi,magomeni,k.koo,temeke,ilala ndio kumejaza makahaba na mashoga.
Ukiwakuta watu wanafanya mambo ya kishenzi huko ujuwe hao washenzi wakuja tu, siyo Waswahili.

Kama ulivoenda wewe ukawakuta wenzako. Waswahili wenye asili yao ya Kiswahili utawakuta misikitini.
 
Back
Top Bottom