Hii ndiyo treni yenye spidi ya kasi sawa na ndege, nilidhani uongo kumbe kweli

Hii kitu niliisomaga zamani kidogo , BBC wakiandika kua miaka ijayo huenda tukawa na treni inayopita kwenye ombwe kwa kasi..

China hana ajizi, katekeleza.

Sisi tuendelee kusema elimu haina umuhimu, bora vijana waache vyuo wawe machinga.
Je, Kuna mtu yeyote mwenye elimu ambaye amewahi kugundua kitu cha maana hapa Tanzania? Ishu ni akili sio elimu.
 
Maendeleo makubwa ya China yalipatikana baada ya kukamilisha mifumo ya usafiri ya kupunguza muda wa kuwa safarini kwa mizigo na abiria.

Hii ikiwemo kutoboa milima ili kupitisha barabara ndani yake na kuondoa safari za mzunguko mrefu za kukwepa milima. Pia, kutumia madaraja ya kuning'inia.

Kwa sasa China inategengeneza ndege zake yenyewe, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha usafirishaji wa anga. Huku reli ndefu zaidi duniani ikiwa nchi China.

Hili la reli ziendazo kazi limeipa China mafanikio makubwa sana kwenye sekta ya usafirishaji abiria na mizigo yao na kuunganisha miji iliyoemdelea na inayoendelea.

Katika kipindi cha sikukuu ya mwaka mpya wa China, njia za usafirishaji huweza kusafirisha abiria zaidi bilioni tatu, hii ikiwa ni karibia nusu ya watu walipo duniani.

Lakini, kubwa zaidi, miundo mbinu hii imejengwa na Wachina kwa mikono yao huku wakitumia zana zilizobuniwa na wao wenyewe. Ikiwa ni mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka 30 tu.

Na hii treni ya kusafiri kwa treni ya ndani ya bomba inazidi kuwaweka Wachina kuwa namba moja duniani kwa usafirishaji wa idadi kubwa ya watu ndani ya kipindi kifupi.

Ova
 
Hii bado sijaelewa mkuu, fafanua zaidi.
 
Marekani wana mradi wa ujenzi wa high speed railways California, kutoka L.A mpaka San Francisco tangu mwaka 2015, guess what?

Mpaka leo mradi umekua slow sana na gharama zinaongezeka kila mwaka

Zimejengwa km 190 tu mpaka sasa!

Wakati China tangu 2015 imeshajenga km 27,000 za high speed railways
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…