Hii ndiyo treni yenye spidi ya kasi sawa na ndege, nilidhani uongo kumbe kweli

Good analysis that's written by the GT of JF.
Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
Wakati mwingine sio vibaya kuona progress tulizopiga kama Nchi badala ya kujaribu kushindana na wenye misuli kutuzidi.

Kuna Nchi tangu Mwaka 1940 ilishakuwa na MaProfesa zaidi ya 2,000 wakati sisi hadi Mwaka 1990 tulikuwa na MaProfesa hawazidi 20

Suala la maendeleo sio la Siku 1
 
Japan, India, South Korea nk. hawatumii kiingereza na wako mbali tu.
Hawatumii lakini ni second language yao na wanafundishwa shule, ndio maana utawakuta ni wakurugenzi wa tech giants huko kwa wanao ongea kingereza. Unashikaje position kama hiyo au kuwa effective kwneye nchi za watu bila kuwa fluent in language yao?
 
Mm nnakuelewa unachokisema,chuki binafsi kwa Magufuli ndizo hadi leo bado zinamtafuna akiwa kaburini,cjajua kwetu sisi watanzania maendeleo hadi yaletwe na namtu gani ndio tuaprreciate!
 
Mchina nouma.
 
Wachina hawaamjni Mungu, Yesu wala shetani . Hivyo wanatumia akili zao mda wote
Hizi kauli huwa zinatumika sana na wengi wetu pale tunapotaka kujifananisha na weupe kwa chochote kile lakini mimi naona hazina maana wala tija linapokuja suala la maendeleo,mweupe ni mweupe tu awe anaamini Mungu awe anaamini shetani awe haamini chochote hakuna rangi nyeusi wa kujifananisha nae yaani hayupo.

Kwani sisi Africa hatuna wasioamini habari za Mungu Yesu sijui shetani?atheist wapo chungu mbovu even humu wapo haya wamegundua nini cha maana?coz kama point inayofanya tushindwe kwenda kasi ni kuamini Mungu or whatever wale tunaosema hizo habari siyo za kweli tuamke tufanye chochote cha kujitofautisha na wanaoziamini lakini bado hatuwezi.
 
Sayansi China inafundishwa kwa mandarin.

Kuhusu lugha ya kiswahili hakuna tatizo lolote.
Lugha ya kufundishia inaendana na uchumi wenu. Ukitaka kujua hili, mfano rahisi upo kwenye magari tunayoyanunua toka Japan. Radio za magari hayo zitatutoaga jasho sana. Maana zipo kijapani, na tule tudada tunaongeaga kijapani. Sasa kama unataka ziwe za kiswahili maana yake utengeneze mwenyewe nchini bila kutegemea mtu mwingine nje ya nchi. Ukitaka utengenezee huko huko nje huku zikiwa zina lugha ya kiswahili, utalipa hela nyingi sana.
 
Hawatumii lakini ni second language yao na wanafundishwa shule, ndio maana utawakuta ni wakurugenzi wa tech giants huko kwa wanao ongea kingereza. Unashikaje position kama hiyo au kuwa effective kwneye nchi za watu bila kuwa fluent in language yao?
English na Kiswahili ni lugha mbili rasmi Tanzania

Angalau India kidogo kingereza wanafahamu lakini hao wengine kama hajazaliwa huko nje basi amekaa huko nje muda mrefu
 
China sio wagunduzi wa Train lakini mandarin haikuwazuia wao kuijua train kuiendesha na kuitengeneza na sasa kuwa moja ya mabingwa wa Train duniani hivyo hivyo kwa Japan

Wewe ndio moja ya wale watu wanaoamini lugha ya kiingereza ndio itatufanya tuendelee ?
 
Tatizo wa kusimamia hayo yawezekane ndiyo hatuna.

In short hatuna au kama wapo hawapewi nafasi kwenye uongozi,nchi hii ina matumizi makubwa sana yasiyokuwa na msingi siku akipatikana wa kukata mirija ya matumizi hayo tutaweza kusogea.
 
Wakuu mnajiaibisha!

maglev hazigusi reli,kwanini mchangia kitu msichokielewa?
Wewe ndiye huelewi. Air friction ipo pole pale kutokana na speed yake kubwa. Ndiyo maana Titunium na Tungsten hutumika kuunda aerospace vehicles. Na hiyo technology inaitwa magnetic tech, ipo hapa duniani kuanzia miaka ya 1984. Ila kwa wengi tumeanza kusikia kwenye bullet trains za Japan 'Shikansen'.
 
haya mimi sielewi.
 
Tatizo wa kusimamia hayo yawezekane ndiyo hatuna.

In short hatuna au kama wapo hawapewi nafasi kwenye uongozi,nchi hii ina matumizi makubwa sana yasiyokuwa na msingi siku akipatikana wa kukata mirija ya matumizi hayo tutaweza kusogea.
Kweli kabisa mkuu, akitokea mtu wa kupindua meza, nchi yetu bado ina potential kubwa sana ya kukua kiuchumi.
 
Hawatumii lakini ni second language yao na wanafundishwa shule, ndio maana utawakuta ni wakurugenzi wa tech giants huko kwa wanao ongea kingereza. Unashikaje position kama hiyo au kuwa effective kwneye nchi za watu bila kuwa fluent in language yao?
Mkuu, kuwa second language sio issue kabisa. Nakwambia wengi wao kiingereza chao bora hata cha kwetu. Wanazo kozi hizo unazozisema na zina watu wanaozisomea kwa lengo hilo la kwenda kufanya kazi huko. Kumbuka hata hao wachina wengi tu wanasoma huko ulaya na America, kama ilivyo kwa wahindi wa wakorea. Lakini asilimia kubwa ya hao watu wao wanaochangia huo ubunifu na maendeleo kwa kiasi kikubwa wanasoma kwa kutumia hizo lugha zao kuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…