Sisemi mimi, uhalisia tunauona mtaani. Said kule Mwanza alimpiga risasi mkewe baada ya kutomkuta nyumbani. Alipompigia simu iliita bila kupokelewa.
Jose hapo goba akimkata mpenzi wake Penina na mapanga. Baada ya kuhisi kusalitiwa na kujibiwa hovyo alipohoji
Mikasa ya wanawake kufanyiwa ukatili baada kusomeshwa na mwanaume na kuamua kuvunja mahusiano baada ya kuhitimu au kupata kazi ndio ipo mingi sana.
Hizi ni story ambazo zinavuma mitandaoni lakini zipo nyingi sana haziwekwi kwenye spotlight.
Msingi wa haya yote ni uwekezaji wa kifedha ambao mwanaume anaufanya. Hao wanawake wangekataa kugharamiwa chochote wasingefika kwenye kuuana. Ndio maana nikasema mwanamke anapokubali provision kutoka kwa mwanaume lazima akubali kupoteza uhuru wake.