Hii nguvu si mchezo: Kitenge, Zembwela na Hando wapewa escort ya ving'ora Dubai

Hii nguvu si mchezo: Kitenge, Zembwela na Hando wapewa escort ya ving'ora Dubai

Kilichoifanya Dubai kuendelea kwa muda mfupi sii DP world Bali walifuta masheria ya kizamani ya Kodi na kujifanya FREE PORT.

Sisi bandari tunayo, maji yapo lakini kwa nini tusichukue maauzi magumu tuifanye BANDARI YETU FREE PORT?

Tusiwazi kuwa hayo ma Kodi ya kufanya bidhaa iwe mara mbili ndio yatakayoendeleza nchi. Ikiwa free port mizigo itakuja mingi, wageni watakuja wengi Tanzania kununua , mzunguko wa fedha utakuwa mkubwa, fedha zitakuwa nyingi serikalini na kwa wananchi, kampuni za kisasa za wazalendo za kupakua mizigo zitaibuka. Haya mengine ni mapropaganda ya kizamani kuamini kuwa hao Jamaa Wana ushawishi wowote kwa mtu mwenye akili timamu
 
Hao kina Kitenge, Zembwela, na Hando ni wasaliti wa Tanganyika yetu.

Usishangae hao jamaa wakijiachia, bahasha zimeshatembea kwao, kama zilivyotembea kwa wabunge.
 
Nani amefatilia Wasafi media leo asubuhi? Hawa watangazaji watatu tangu juzi wapo Dubai na wanajinasibu Kama ni wageni rasmi wa DP world kutoka Tanzania. Na wanapata escort ya ving'ora Kama wageni wa heshima.

Leo walikuwa wanawahoji watanzania ambao wanafanya kazi hapo bandari ya Dubai. Kiuhalisia wote waliohojiwa ni kutoka kwa ndugu zetu unguja na pemba (Zanzibar).

Mambo mengi mazuri Sana ya DP world yameongelewa,ikiwa pamoja na bandari kupokea meli 30 kwa wakati mmoja na kuhudumia meli sita zenye magari 3k kwa siku mbili tu. Mambo ni mengi.

Lakini Hawa jamaa ni wanajizima data au hawajui kilio Cha wanaowapinga hao DP world kuwa siyo ufanisi wao Bali ni MKATABA mbovu na wa kinyonyaji na wakivhief Mangungo baina yao na Tanzania?

Hata dada yetu wa Jf bi Faiza Fox nae aliandikw uzi wenye mtazamo huu huu wa kina Zembwela kuwa "DP world wapo hadi Uingereza iweje nyie walala hoi watanganyika mnawakataa". Akapigwa maswali haya haya,umeuona mkataba wa Uingereza? Au mkataba wa Uingereza na huu wa kwetu unafanana?

Alafu kingine; hivi ni nani amawafadhili Hawa jamaa watatu? Huko Dubai? Maana wanajimwayamwaya kama wafalme. Na Wana ego balaa,full kujisifu.

Hii nguvu ya DP world kwenye media za bongo siyo mchezo.

Lakini Hawajui kuwa ukimsisitiza Sana Mtu kuwa kitu chako ni ni kizuri ndivyo unavyomfanya astuke kwamba kwa nini jamaa ananilazimisha Sana nione hiki kitu chake kipo sawa? Jamaa wanafosi mpaka kila mtu Sasa anajua kwamba wanalazimisha!!

Hii tabia tunayo Sana sisi mawinga/ wazee wa kulenga hapa kariakoo. Nikiona hiki kiatu ni 'mdosho',nguvu ninayotumia kukuaminisha kwamba ni kiatu genuine ili uingie mkenge siyo ya nchi hii. Ukifungua wallet tu tukamalizana napita hivi,utajijua mbele ya safari. Ukikivaa ukapiga hatua zako 20,mguu unanyanyuka,soli inabaki chini.

Nikimwangalia Gerald Hando ni Kama Mtu mwenye kujistukia tofauti na wenzie. Hawa jamaa wawili wanaupepeta mdomo si mchezo. Hawana breki.
Huyu Mama angekuwa kwenye nchi ya watu wanaojielewa,angekuwa amerudi Zanzibar na Waziri wake.Serikali na Bunge wanadharau sana Wananchi!
 
Sijui ni nini kifanyike. Lakini Picha hii hapa. Hawa watu wameenda Dubai kula maisha na Wakarudi hapa kuja kupigia chapuo DP world. Hii ni hujuma zidi ya Watanzania.

1687507533275.jpeg
 
Huhitajika Uongo mwingi sana na nguvu kubwa sana kuhalalisha uovu.


Wao ngoja waipe promoooo tu , Watanzania sio wajinga, na Watanzania wa Sasa wameelimika.
Na ole wao waje tutawageuza nyama choma hao wauza watumwa, kuhusu hao sijui kitenge na wenzake hao achana nao maana tunawsjua ni makuwadi na madalali wa hao warabu.
 
Hawa viazi walienda sijui kufanya nini..kama kuna wengine wanahisiwa kuwa wanatumia mtandao pendwa sioni shida kujipeleka kwa Mwarabu..ile rangi ya madhiwa mbaya sana inakata akili zote mtu akikumwagia nyuma.View attachment 2666163
wivu unakusumbua. na hili taifa halitoendelea watanzania tuna wivu sana na kulogana.
 
Back
Top Bottom