Hii ni aibu leo Tabata. Polisi anatoa maelekezo kwa Wanajeshi aisee

Hawa sasa kuanzia leo wawe wanalipa nauli kwenye vyombo vyetu vya usafiri huwa wanapewa fair ,ila sasa hawastahili, alafu najiuliza jeshini hakuna majemedari na wazalendo wa kuweza kuwatulia viongonzi wa juu ambao wanaamua kulibagaza jeshi kisa siasa za ccm.

Mkuu wako akitoa order inatakiwa kuitii ila sio kila hata kama ni batili ,vinginevyo kwa umoja wenu mnatakiwa kumuadabisha pia
 
Kama CCM imeshindwa kutulinda na kundi la wahuni basi CCM D9 tutaitoa
 
Sasa maajabu yanatoka wapi hapo, mkuu 'Nightmare', kama siyo kutaka kuwalaumu tu hao kwenye picha.

Ubaya wa wetu waTanzania huwa hatwekei maanani maswala mengi; au tunashindwa tu kuunganisha 'dot' toka moja hadi nyingine!

Naomba nikukumbushe basi yaliyosemwa na Mkunda, unajuwa Jenerali Mkunda ni nani? Kumbuka aliyosema kabla ya Oktoba 29, na yote yaliyotokea baada ya hapo.

Ukikumbuka yote hayo na uwe na akili iliyo huru, huwezi kushangaa lolote unaloona kwenye hiyo picha..

Anyway, hizi ni mada tunazianzisha ili kupata muda wa kulalamika na kupoteza wakati. Sasa mada ishapanda, na tutaendelea kulilia hao watu wengine wafanye tunayotakiwa kufanya sisi wenyewe.
 
Umempa jibu la kueleweka; lakini nina mashaka sana kama bado atakuelewa.

Haijalishi matendo yao maovu kwa raia, lakini bado wanazo taratibu za kiutendaji.
Ni tofauti sana kama pangekuwepo na uasi huko ndani ya vyombo hivyo, hali ingekuwa ni tofauti sana..

Kuwa tu mwanajeshi, au kuvaa gwanda la kijeshi hakuondoi wajibu wa kufuata taratibu zinazoendesha taasisi hiyo. Kukiwa na maasi, hizo taratibu zinatupwa mbali, wanajifanyia wanavyojipangia waasi wenyewe.
 

Umenikumbusha jambo fulani. Ngoja nicheke kwanza af nisimulie😂😂😂😂

Miaka fulani, tukiwa jkt, siku moja afande (hawa jkt wakufunzi wenye V za kijani mabegani) alitupeleka kwenye fatiki eneo la mbali kidogo na kikosi.

Sasa tukiwa huko, sikumbuki chanzo kilikuwa ni nini, lakini ilifika muda tukawa tunagomea amri zake. Kila analosema tunagoma, kila anachoamrisha tunagoma. Tulikuwa ngorongoro tu (wanaume tu)

Basi akawa mpole, tukawa tunaendelea na fatiki vile tunataka sisi makuruta. Kumbe ameliweka moyoni.

Jioni baada ya chakula cha jioni, tulipofoleni kwenye kombania, oya tulipigwa doso la kikatili sana hadi serengeti (mademu kuruta wenzetu) wakajawa na huruma karibia wote wakaanz kulia. Wengine walipandisha mapepo😂😂😂😂

Ile show sitaisahau manina zake yule jkt mkufunzi
 
By that time pamoja kuwa kuruta hata kama badae kiliwaramba mlionesha ushirikiano ,sasa tiyri ni staff utofauti ni vyeo , na wapo zaidi laki 3, mnakubalije sasa mbagazwe aliye juu kwa mambo ambayo hayapo sawa
 
By that time pamoja kuwa kuruta hata kama badae kiliwaramba mlionesha ushirikiano ,sasa tiyri ni staff utofauti ni vyeo , na wapo zaidi laki 3, mnakubalije sasa mbagazwe aliye juu kwa mambo ambayo hayapo sawa

Mambo ya Jeshini Sio mepesi hivo.

Kwasababu ile Coup ifanikiwe, Ni lazima atleast kambi 5 ziwe ngangari upande mmoja lasivyo mapinduzi yanaweza kufeli au Ukatokea uasi.
 

Kwenye Hali kama hii TISS kwa kawaida wanavalishwa magwanda ya jeshi. Huenda huyo anayepewa maagizo ni afisa wa Tiss na anayetoa maagizo ni afisa wa Tiss vile vile! Hapo hakuna mjeshi Wala polisi.
 
Hivi siku hizi hawa mafisi wanalipa nauli kwenye daladala?
Maana zamani walikuwa wanarukwa, akidaiwa nauli walikuwa wananza kupiga makofi konda hadi dereva na safari inaiishia hapo
Pumbavu sana hawa
 
Sasa hapo mmejuaje anapewa maelekezo au sababu Maria kasema.... Mambo ya kawaida kabisa kwenye joint oparesheni haya mnayakuza kijinga tu..

Na msichijua lipokuja swala la kukontrol mitaa na wananchi POLISI WAKO MBALI MNOO.
 
Wamejitakia aacha waendelee kudharauliwa si mfo wanachotaka
Km wangefanya yao 29 ingekua heshima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…