Subiri ukishakuwa utaelewa
Ofcourse hajakaziwa lakini angalau yeye utajiri wake hauna makandokando, haibi kodi za wananchi anatoa pesa mfukoni mwake, ndio maana timu ikifanya vibaya hawezi kuacha kulalamika sababu anajua uchungu wake
Wote tunajua nchi hii bila ufisadi na utapeli ngumu kutoboa hasa kwa hao wafanyabiashara wakubwa, ndio maana wengi wanaamua kuwa machawa wa wanasiasa ili mambo yao yaende maana kwa akili ya kawaida tu watu kama kina gsm na rostam aziz tunasikia tu ni matajiri, ila hawaeleweki wanatoa wapi pesa zisizoendana na biashara zao maana net worth zao ni za kubumba tu hazipo hata kwenye vyanzo rasmi kama forbes kulinganisha na mo na bakhresa
Huyo manji naye walimkabia juu sababu utajiri wake ulikuwa na konakona yani matajiri wote walioyumba kipindi cha magufuli basi ujue walikuwa makanjanja, sababu matajiri wa ukweli mfano wa hao niliowataja wala hawakuyumba na ndio maana hao matajiri feki baada ya magufuli kufariki, baadhi wameibuka kwa kasi ya ajabu kwenye huu utawala wa kujilia kwa urefu wa kamba na wanatakatisha fedha kwenye mambo kama mpira na sanaa ili wasihojiwe sana sababu wanawapa furaha wananchi