Hii sheria ya ardhi kuhusu wageni kumiliki ardhi isipokuwa makini mtakuja kulaumiana mbeleni

Hii sheria ya ardhi kuhusu wageni kumiliki ardhi isipokuwa makini mtakuja kulaumiana mbeleni

Sijui kama unafahamu Historia ya USA na alaska

hiyo histori naijua na sio hiyo tu, hata ile ya hongkong naijua vizuri
hizi zote znahusu nchi kutawala eneo fulani la nchi nyingine

hapa sisi tunajadili mtu au kampuni kununua ardhi sio nchi kununua ardhi
 
Minaona sheria haina mashiko na bora ifutwe then wageni wakodi ardhi na sio kununua.
Hivi hao wapitisha hiyo sheria mgeni anunue ardhi,wanawashwa nini kuacha vilevile alivyoweka Nyerere!?
 
Mmasai anatolewa Ngorongoro, Ngorongoro ni hifadhi ya dunia kwa sasa na si ya Tanzania. Na hapewi mgeni yeyote, wacha uongo.
Kama ni mali ya dunia mbona hata dunia imepiga kelele baada ya Wamasai kuondoshwa?
 
Hongera waziri wa ardhi Jerry Silaa nili kunukuu kuhusu swala la wageni mnafanya maboresho kuhusu wageni kumiliki ardhi.

Tatizo linaweza kutokea mbeleni kwenye sheria hii sababu wananchi wengi wako kwenye wimbi la umaskini ususani vijijini ambapo ndio maeneo yenye rasilimali kama madini,kilimo na biashara.

Wananchi hawa watajikuta wakiingia na tamaa za wageni kwa dau watakazopewa kuuza ardhi zao na mwisho wa siku ardhi ya tanzania itakuwa ardhi mataifa mengine yenye maeneo yao.

Kuna nchi zinazo zitolea macho tanzania ilivyo barikiwa na kila kitu

Naiona tanzania ikijitakia inachokitaka
Katiba mpya!
 
Sheria yenyewe iko wapi, mbona siioni?
Rasimu ya Sheria hiyo inapaswa iwekwe hadharani na kwenye mitandao ili Watu waione na ili Watu hao waweze kuitolea Maoni yao kabla Rasimu ya Sheria hiyo haijapitishwa na kuwa Sheria kamili.
 
Hongera waziri wa ardhi Jerry Silaa nili kunukuu kuhusu swala la wageni mnafanya maboresho kuhusu wageni kumiliki ardhi.

Tatizo linaweza kutokea mbeleni kwenye sheria hii sababu wananchi wengi wako kwenye wimbi la umaskini ususani vijijini ambapo ndio maeneo yenye rasilimali kama madini,kilimo na biashara.

Wananchi hawa watajikuta wakiingia na tamaa za wageni kwa dau watakazopewa kuuza ardhi zao na mwisho wa siku ardhi ya tanzania itakuwa ardhi mataifa mengine yenye maeneo yao.

Kuna nchi zinazo zitolea macho tanzania ilivyo barikiwa na kila kitu

Naiona tanzania ikijitakia inachokitaka
Hizi sheria zinatungwa kutimiza malengo ya tabaka fulani lenye nguvu ya pesa, mbaya zaidi wananchi hawashirikishwi kutoa maoni yao, mamlaka zinatumia nguvu kufanya maamuzi matokeo yake watu wanaporwa ardhi kimabavu kwakuwa hawajapewa elimu ya ardhi wala sheria za ardhi
 
Kama ni mali ya dunia mbona hata dunia imepiga kelele baada ya Wamasai kuondoshwa?
Hiyo labda dunia ya ndotoni mwako.

Hivi unafikiri nagorongoro Crater kufanywa urithi wa dunia ni kwa ajili ya wale wamasai wafanye makazi na maendeleo mule shimoni?

Waondoke mule haraka sana, wasibadili mazingira asilia ya wanyama, wasituharibie mbuga ile.
 
Tunarudishwa kwenye unyarubanja. Tutakuwa tunakodi ardhi kwa wageni ili kulima, ndani ya nchi yetu wenyewe. Tamaa mbele mauti nyuma.
 
Tunarudishwa kwenye unyarubanja. Tutakuwa tunakodi ardhi kwa wageni ili kulima, ndani ya nchi yetu wenyewe. Tamaa mbele mauti nyuma.

Sasa kama ardhi haifanyiwi maendeleo na wazawa ni heri waje wenye kuhitaji wawekeze na itumike kuleta maendeleo ya uchumi na kijamii

Tanzania hadi leo ukitembea maeneo mengi ya nchi ni mapori yasiyokuwa na maana.
 
Wabongo waoga sana khs mabadiliko wanatamani wawe vile vile

tena ingewezekana uraia wa nchi mbili uwepo hapa tz, kwanza hao wageni watakuwa raia wa hapa na kuwa huru kununua ardhi

pili
wataongeza idadi ya wapiga kura wenye akili maana kwa sasa wenye akili wapo wachache

tatu
Tutapata fursa ya kuchanganya damu na watu weupe na kuzaa chotara
 
Mmeanza kuchokonia ardhi. Nashauri vijana wenzangu ukipata hela popote pale buy some piece of land. Hii nchi kuna uwezekano 10years land ikawa haikamatiki
 
Ardhi ya Tanzania kwa mujibu wa sheria ni mali ya Rais wa Jamhuri ya muungano na kila anayepewa kipande na kupewa hati anakuwa amepangishiwa kwa muda uliotajwa kwenye hati yake yani miaka 33, 66 au 99 zamani kulikuwa na 999 pia. So hamna mwenye ardhi hapo wote ni wapangaji na rais anaamua muda wowote ampangishie nani mwenye maslahi zaidi, na kwenda bungeni kubadilisha sheria ya upangishaji! Ufahamu tu...
 
Hii kauli mbiu ya twendeni na mama 2025, isipokuwa makini mtakuja kulaumiana mbeleni
 
Sasa kama ardhi haifanyiwi maendeleo na wazawa ni heri waje wenye kuhitaji wawekeze na itumike kuleta maendeleo ya uchumi na kijamii

Tanzania hadi leo ukitembea maeneo mengi ya nchi ni mapori yasiyokuwa na maana.
Hayo mapori ndiyo tunapata kuni na mkaa wa kupikia, miti ya kujengea, tunawinda kware na sungura, wasukuma na wamasai wanachungia ng'ombe na kufanya bei ya nyama iwe chini nk nk. Hakuna pori lililokaa bure.

Mkiwapa wageni mtachuma wapi watowo na masasati?
 
Magufuli alilijua hili na akasema wananchi wachukue maeneo wasajili ili wawekezaji wakija wawakodishie

Pamoja na yote ila alilijua hili
Muwekezaji anakuja na hela ili kuwekeza na atakutana na wenye tamaa huko ardhi
Sijui kwanini mswahili akiona mwenye hela anaziona kama za baba yake
Hapo atazungushwa hela zitamtoka ila atapewa ekari 1000
Lukuvi alisema tumiliki eka 50 tu sijui yeye ana ngapi leo
 
Hayo mapori ndiyo tunapata kuni na mkaa wa kupikia, miti ya kujengea, tunawinda kware na sungura, wasukuma na wamasai wanachungia ng'ombe na kufanya bei ya nyama iwe chini nk nk. Hakuna pori lililokaa bure.

Mkiwapa wageni mtachuma wapi watowo na masasati?

Yaan mawazo yako hayana tofauti na watu wa kijijini au watu duni wasio elewa maana ya maendeleo

kwanza matumiz ya kuni na mkaa yanapaswa kupigwa marufuku, nishati ya kupikia iwe gesi na umeme

pili
hao wamasai na wasukuma wanaharibu sana mazingira kwa ufugaji usio na tija wa kuhama hama, wanapaswa kufuga ng'ombe wachache wa kisasa wenye tija

tatu
baadhi ya maeneo ya kimkakati yatatengwa kwaajiri ya uoto wa asili, hifadhi ya wanyama na mimea ya asili au kwaajiri ya utalii
 
Back
Top Bottom