Hii video haina Maadili, Huwezi kupiga picha na Rais ili umringishie ex wako

Hii video haina Maadili, Huwezi kupiga picha na Rais ili umringishie ex wako

Sijajua kilitokea nini Hadi wahusika wakakubali kitu cha ajabu namna hii kikatokea. Hili lililotokea halikua sehemu ya uchekeshaji.... Huwezi kuomba kupiga picha na Rais WA Nchi (Mwanamke) eti ili umkomoe Ex wako. This is bulshit na Kwa kweli tuzuie huu ujinga usiendelee.

View attachment 3246880
Acha kucomplicate maisha isee acha watu waturahi huyo ni binadamu pia kama wewe na mimi anafurahi pia kufurahishwa.
 
Sio kesi saana, ukizingatia ilikuwa ni show ya comedy, kwa hili simlaumu mama.

Ila uchawa ndio too much, kila kitu mama, moaka KOMEDI ni ya mama, tunapoelekea itakuwa tukizagamuana, mrembo akinogewa na utamu apige kelele mama mi5 tena..
🤣 🤣 🤣 🔊
 
Sijaona Tatizo.
Walikuwa wansherehekea Siku ya wajinga na tuzo za Ujinga na wajinga so YES ni jambo zuri.

Wenzetu Commedians wana Taaluma za kueleweka huku kwetu kila ambaye akili hazimtoshi anakuwa celebrity.

Anyway Hii ni Tanzania
 
Sijajua kilitokea nini Hadi wahusika wakakubali kitu cha ajabu namna hii kikatokea. Hili lililotokea halikua sehemu ya uchekeshaji.... Huwezi kuomba kupiga picha na Rais WA Nchi (Mwanamke) eti ili umkomoe Ex wako. This is bulshit na Kwa kweli tuzuie huu ujinga usiendelee.

View attachment 3246880
Nyie watu mko serious sana na maisha.

Comedy hiyo . Ndio maana watu wanacheka.
 
Nami nimeona haya maajabu, yaani rais mwanamke.
Ndiko tulikofika, hivi mkapa kuna mjinga angeweza kumsogelea apige picha ya kumringishia X kweli?

Mkuu una uhakika hakuna wanawake waliopiga picha na kuwaringishia wapenzi wao.

Unakuuza mambo nje ya muktadha, wivu tu unakusumbua, yawezekana ukawa ndiwe ex wa huyo msanii!!!
 
Kwahiyo mkuu unasema jamaa angesema Mh. Rais naomba nikushike kiuno ili nimkomeshe mke wangu ananikataza kushika kiuno chake wewe kwako ungechukulia poa tu.

Kwenye comedy wewe unapimaje dhamira ya mzungumzaji kama analengo lingine tofauti na kuchekesha? Kila kitu kina limit regardless ya sehemu.

Mkuu take it easy, Rais ni binadamu, mazingira na hadhira ilikuwa inaruhusu. Punguza imagination potofu!!
 
Back
Top Bottom