Hili la kuapisha Viongozi wa Serikali kibarazani nyumbani kwa Rais limekaaje?

Haya ni matusi makubwa kwa tuliomchagua Rais. Kuapisha kwenye makazi yake binasfi. J's Motel hoteli yake Rais.
Huyu mzalendo namba moja alijenga lini hii!? Ni baada ya kuukwaa Urais au hapo kabla?
 
Wewe dada utakufa na stress kwa sababu ya wivu. Rais kila alipo kuna ofisi yake kasome sheria inayoanzisha Ofisi ya Rais sasa wewe na ngumbalu yako unakuja na copy and paste ya Rwaitama fala yule!
 
MUNGU mbariki magufuli
Nchi hii toka enzi za mwalimu kila wilaya ina ikulu ndogo,anaebisha aje hapa
Hayo si makazi binafsi ni ikulu ndogo
Halafu katiba haimzui Rais,anaweza kumuapisha mtu hata mnadani,almuradi kanuni za kiapo husika zifuatwe
Mengine yote unaweza kuwa sahihi kwa ujinga wa Katiba yetu...
Lakini kwenye makazi unapotosha.... Hujui kuwa hujui!
 
Jinyonge la sivyo utakufa na stress dada!
 
Mengine yote unaweza kuwa sahihi kwa ujinga wa Katiba yetu...
Lakini kwenye makazi unapotosha.... Hujui kuwa hujui!
Anapotosha vipi Rais anatembea na ofisi popote alipo ndiyo kawaida. Ni pale tu anapokuwa nje ya nchi ndiyo huwa anaachiwa Makamo wa Rais
 
Mengine yote unaweza kuwa sahihi kwa ujinga wa Katiba yetu...
Lakini kwenye makazi unapotosha.... Hujui kuwa hujui!
Rais ana.bendera mbili,ya taifa na ya Rais
Anapokuwepo Rais lazima.bendera yake iwepo na.anahesabika.yupo ofisini
Mkapa.alimpandiaha cheo lt Generali Sarakikya kuwa General akiwa.uwanja.wa taifa,kwa nini hakusubiri afike ikulu
 
Mkuu mimi nilichokuwa nakosoa ni wewe kusema pale si makazi yake pale Chato bali ni Ikulu ndogo...

Anyway... You are setting new standards... Wengine watakapoyakataa makazi rasmi ya rais - Ikulu kwa sababu zozote zile mje mtetee hivi hivi mnavotetea leo...
 
Wewe dada utakufa na stress kwa sababu ya wivu. Rais kila alipo kuna ofisi yake kasome sheria inayoanzisha Ofisi ya Rais sasa wewe na ngumbalu yako unakuja na copy and paste ya Rwaitama fala yule!
Rwaitama ndo nani tena ?Ni mawazo yangu sijacopy popote. Ni analysis yangu mwenyewe baada ya kuona kituko hiki Rais alichofanya leo. J's hotel kuna office ya Rais ?
 
Magufuli is doing a very good job so far. I am impressed.
 
Kabla ya kuanza kulalamika, naomba kufahamu kisheria imekaaje? Ukitupia na vifungu kadhaa vya katiba itakuwa poa zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…