Hili la vibali vya kazi Rais ashauriwe zaidi

Hivi wewe unaweza kukubali uwekeze pesa yako halafu uchaguliwe watu wa kuisimamia? Mwekezaji akija anataka zile key posts kama mkurugenzi mkuu, mkurugenzi wa fedha, mkurugenzi wa production na head wa technical service aweke watu wake. Hapo kuna ubaya gani wakati nafasi zilizobakia wanafanya wazawa.

Pili ujio wa wafanyakazi wa kigeni unazalisha nafasi za kazi indirectly kwa sababu hao wafanyakazi wa kigeni wataajiri mahouse boy na mahouse girls, walinzi na mashambaboi huko nyumbani kwao, hivyo kuzalisha ajira zaidi kuliko kama nafasi zao zingeshikwa na wazawa.
 
Tukisema tuwasikilize WAWEKEZAJI siku watakuja kuomba PASSPORT kwa kisingizio cha kutaka kulinda rasilimali zao.
 
Kama muwekezaji amefungua mradi au ana kampuni yenye watu 700 kuna tatizo gani hata 100 wakiwa ni kutoka nje??
 
Mbona kaeleweka vizuri tu. Kuna baadhi ya nafasi lazima u compromise kwa interest ya mwekezaji. Haina maana kuajili wageni bila ukomo. Maana hata hao wanaoruhusiwa kisheria, ku renew work permit imekuwa ni urasimu mkubwa.
 
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] msiba huu, kwahiyo waajiriwa wa vyuo watapata kazi za house boy na kufua sidiria za wageni
 
Amesema pia tuangalie mfumo wetu wa elimu tuweze kupata watu wenye ujuzi wa kufanya kazi vyema.
Mimi sipingi kauli
Natamani iwepo clarification..
Je wageni waajiriwe bila kujali idadi?
Au usimamizi uwepo kama enzi za JK..
 
Nchi iko na tatizo kubwa la ajira kwa sababu uwekezaji ni mdogo na viwanda ni vichache. Hilo suala la watu kutoka nje kuja kuchukua nafasi za wenyeji ni tone tu katika bahari ya matatizo ya ajira yatokanayo na uchumi usio na viwanda.
 
Kuna wazelendo uchwara wengi sana nchi hii
Mbona wageni hawakuwepo na ajira kwa watanzania hazikuwepo? Sheria ya vibali vya kazi ilibana lakini ajira zenyewe hata kwa watanzania hazikuwepo (hazipo).
 
Nchi iko na tatizo kubwa la ajira kwa sababu uwekezaji ni mdogo na viwanda ni vichache. Hilo suala la watu kutoka nje kuja kuchukua nafasi za wenyeji ni tone tu katika bahari ya matatizo ya ajira yatokanayo na uchumi usio na viwanda.
Sasa kama una degree ya atomic science nani atakupa ajira? Walimu haooo wanalamba ajira zao.
 
Ukiona mchina anakuja na wafagizi wake ni kwa sababu mliwaambia wao ni marafiki zenu wa karibu na hamukuwapa mipaka kama "mabeberu" ya kizungu ambayo wao huwa hawaji na wafagizi wao. Turejeshe uhusiano mzuri na wa faida na mabeberu ya kizungu pia ila tuwe na uwanja mpana kwani Wachina wako mbioni kuifanya Africa koloni lao baada ya kujua wao ndio wamebaki kimbilio la madikteta.
 
Naona hamjamuelewa Mh Rais. Yeye kasema kuna maeneo yanahitaji busara ili kulinda interest za mtaji wa mwekezaji. Haiwezekani mwekezaji alalamike vibali vya secretary, wahudumu, madereva, HR Officers n.k. Lazima watakuwa wanaongelea nafasi nyeti kulingana na aina ya uwekezaji. Mfano Director of Operations, Finance Manager n.k ambapo kwa complexity ya project unaweza kukuta watano ni wachache. Utakuwa ni ujinga wa hali ya juu kudhani eti Waziri mwenye dhamana ya uwekezaji naye ameelewa kama ninyi hapo.
 
Bado nchi inaongozwa na matamko na hotuba. Kila nchi duniani wamelipa kipaumbele suala la uhamiaji.

Miaka ya nyuma mambo yaliendeshwa kiholela mpaka raia wa kigeni walimiliki pasi za Tanzania.
Kweli kabisa, ni hatari sana kutaka walegeze kamba. Kauli ya Rais ni amri, inabidi achuje maagizo yake maana nina uhakika from Monday vibali vitaanza kutoka kama njugu. Mambo ya uhamiaji na vibali ni sensitive asisikilize kila kilio atawatoa kwenye reli watumishi.

Mambo kama TRA kuvuka mipaka inajulikana sababu ikiwemo task force ya kuvunjilia mbali lakini asipochunga tone yake kwenye maelekezo nyeti tutarudi nyuma hata kwenye mazuri aliyofanya JPM.

Nyakati hizi lazima kuna watu wana set agendas makusudi kwa malengo yao na watu wasio waaminifu wamchomekee mama. Usishangae tukarudi hadi kwenye kununua umeme wa IPTL. Twende taratibu na kwa utafiti wa kina, tusitibue maji yote kufurahisha watu tu.
 
Tuboreshe uhusiano wetu na mabeberu wa kizungu tuache kutegemea Wachina ambao hupenda kuja na vibarua wao katika miradi yao.Inasemekana hawa vibarua wao wanaokuja huku Africa wengine ni wafungwa huko kwao.
 
JPM kwenye maswala ya uchumi kaboronga tu mkuu ,hatuwezi kuja kuelewa mbele kabisa ,yaani uandae task force ya kina biswalo,bashite na dotto kwa ajili ya kupora wafanyabiashara mali zao ndio tuje kumkumbuka? Akumbukwe kwani amekuwa MTOTO WA DANDU?
Ile ilikuwa wrong wrong! Ila kuna vitu vya msingi vibadilishwe kwa tafiti na watu waadilifu. Ukiona unapendwa tu kila unachosema hilo ni tatizo. Huko mbele mzito utamuelemea wanaoshangilia sasa ndio watakuwa wa kwanza kumsulubu.
 
Mtu aliyewahi kuishi nje kauli ya mama ni nzuri sana ila kwa Mtanzania ambaye hajawahi kuishi nje anaweza kupingana na mama.

Muingiliano wa watu kutoka mataifa tofauti huchochea uchumi.
Bonge la point mkuu
 
Mimi nilimuelewa kuwa anapinga ucheleweshaji
 
Kwa nini shule binafsi na hoteli zinapenda kuajiri walimu na wafanyakazi kutoka nje wakati wangeweza kuwaajiri wa hapa nchini na wasiingie gharama za kulipia vibali vya kazi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…