Hili ni kosa la kiufundi alilofanya Adolf Hitler

Fafanua kwenye biashara
ofcoz.

hata hivo jamaa katuachia somo kubwa sana kwenye maisha ya kawaida na biashara.

Mistake aloifanya hitler wanaifanya watu wengi sana kila siku iwe kwenye biashara au kwenye maisha ya kawaida.
 

naukubaliana na wewe lakin in addition one of major set back for germany during ww2 is inigma secret code kuwa bypassed ilikuwa cracked. inigma ilikuwa encription code ambayo ndio ulikuwa mfumo wa code za kimawasiliano. point no 2 ni uungwaji mkono waliofanya germany kwa japan kama germany isingeunga mkono japan, USA asingetoa msaada kwa allies kitu ambacho kiliwaongezea nguvu sana russia, and england japan. point no 3 hitler asingeingilia stratergic tactical decision za jeshi. to me nilipenda perfomance ya majenerali kadhaa ya wanazi 1.Hans guderian( the father of blitz) 2. erwin rommel ( desert fox) 3.paulis ( six army in stalin grade
 

Tuseme ukweli tu mchungu, aliyepambana zaidi na kusababisha Germany ika collapse ni USSR...
US alipambana zaidi na Japan kwa sababu alitaka ku control kil kitu kwenye Pacific Ocean...
but much respect to japan they fought more determined yaani ni kiume si kiume kiume hasa that was spirit okinawa and iwo jima was deadly battle
 
Sio kweli mkuu. Wayahudi kivyovyote number y 6million ni ndoto kwa miaka Ile. Unajua Leo iyo Israel baada ya kukusanyana kila kona na kuongeza 0 bado wapo wangapi???


Idadi ya watu wa Kiyahudi duniani inakadiriwa kuwa takriban milioni 15.7. Israel ina idadi kubwa zaidi ya Waisraeli wa Kiyahudi, ikiwa na watu takriban milioni 7.2, ikifuatiwa na Marekani yenye watu milioni 6.3. Hapa kuna muhtasari wa kina zaidi:
  • Israel: Milioni 7.2
  • Marekani: Milioni 6.3
  • Nchi zingine zenye idadi kubwa ya Waisraeli wa Kiyahudi:
    • Ufaransa: 440,000
    • Canada: 398,000
    • Uingereza: 312,000
    • Argentina: 171,000
    • Urusi: 132,000
    • Ujerumani: 125,000
    • Australia: 117,200
 
Kihistoria, Wajerumani hawakuwa wamezoea vita vya muda mrefu. Mikakati yao kuu ya kijeshi ilikuwa Blitzkrieg (Vita vya Radi), ambayo ilikuwa ni kushambulia adui kwa nguvu kubwa kwa kutumia vikosi vingi vya pamoja (Anga na Ardhi).
Mkakati huu ulifanya kazi Ufaransa, ambayo ilishindwa kwa muda wa mwezi mmoja na siku kumi. Haukufanya kazi katika Urusi, nchi kubwa yenye nguvu za viwanda.
Moja ya sababu kuu za uvamizi wa Umoja wa Sovieti ilikuwa ni kuteka maeneo ya mafuta ya Caucasus na rasilimali nyingine kama chuma na mpira, ambazo Ujerumani bado inategemea kutoka Urusi hadi leo.
Wakati wa uvamizi, Umoja wa Sovieti tayari ulikuwa umehamisha karibu viwanda 1500 vikubwa kutoka Ukraine, Leningrad na Stalingrad hadi Siberia ambapo Wajerumani hawakuweza kuvikaribia.
Hivyo, Warusi walilazimisha Wajerumani kupigana vita vikali vya uchovu, katika maeneo ambayo hayakuwa na umuhimu mkubwa. Wajerumani walikuwa na Divisheni 10 za Panzer, lakini mizinga yao ilishindwa kufanya kazi vizuri katika baridi kali ya Urusi. Wanajeshi wa Kijerumani walikufa kwa njaa, na hata tukio la ukatili wa kula wenzao liliripotiwa.
Kile ambacho nimejifunza kuhusu vita ni hiki: Teknolojia Bora ni muhimu katika vita, lakini Uwezo wa Viwanda ni muhimu zaidi. Wajerumani walikuwa na teknolojia bora, lakini Warusi walikuwa na uwezo kamili wa viwanda, ambao uliwapa uwezo wa kuzalisha zaidi kuliko Wana-Nazi na kujaza tena Jeshi la Redi wakati wa nyakati muhimu.

 

Battle Of Stalingrad

Vasily Grigoryevich Zaytsev ( Machi 23, 1915 - Desemba 15, 1991) alikuwa mduguaji(sniper) mashuhuri wa Soviet wakati wa mpambano kati ya jeshi la Soviet lililojukikana kama Red Army na jeshi la ujerumani lililojulikana kama Wehrmacht huku likiongozwa na vikosi katili vilivyojulikana kama Schutzstaffel au kwa kifupi SS

Vasily Grigoryevich Zaytsev alijulikana sana hasa katika pilikapilika zake za udunguaji kati ya Novemba 10 na Disemba 17, 1942.
Hii ilikuwa wakati wa mpambano muhimu sana wa Stalingrad, ambapo aliweza kuuwa askari na maafisa wa adui 225.
Idadi hii ilijumuisha wadunguaji 11 wa adui. Kabla ya Novemba 10, tayari alikuwa amewaangusha wanajeshi 32 wa adui kwa kutumia bunduki ya kawaida ya
Mosin-Nagant Model 1891/30.
Kipindi hiki chote, Vasily aliweza kuuwa adui za bila yaku na darubini ya ulengaji kwenye bunduki yake.
Baada ya taarifa zake kufika kwa wakubwa wake jeshini, walimfanyia sherehe na kumpa medani, ambapo Vasily aliiomba kitu kimoja nacho ni darubini ya kufunga kwenye bundiki yake ili aendelee kuwawinda wanajeshi wa uerumani, sababu vita vya Stalingrad vilipiganwa katika ya mji ndani ya magorofa yaliyoteketezwa na ndege za jeshi la anga la ujerumani lilihulikana kama Luftwaffe, ambapo Vasily aliwahi kunukuliwa akisema ni mara kadhaa ilibidi aache kuwinda adui kwa udunguaji na kuamua kuweka singe kwenye bunduki na kuwasaka chumba hadi chumba.
Kati ya Oktoba 1942 na Januari 1943, Zaytsev alikuwa ameweza kuuwa wanajeshi wa ujerumani 242 yaliyothibitishwa. Baadhi ya watu wanaamini kwamba idadi halisi inaweza kuwa juu kama 400.
Umahiri wake ulimpatia sifa kama shujaa na kuwafanya waandaamizi wa chombo cha propaganda ndani ya jeshi la soviet kumtengenezea stori ya kusadikika(myth) iliyoelezea mpambano kati yake na mdunguaji mahiri wa jeshi la ujerumani aliyojulikana kama Major Erwin König, ambapo wataalamu wa historia walinasema haijawahi kuwepo na mdunguaji huyo kutoka jeshi la ujerumani.

 
Kilichomferisha Hitler ni hali ya hewa na USA kuingilia lakini alikuwa ashawamudu wote
 
Moja ya vitu ambavyo sio vya kawaida ni dem/mke wake hitler Eva Brown.Pale nilipata somo kubwa kwamba true love comes automatically.
 
Reader digest kitabu kilielezea vizuri.ina matukio na tarehe kwa picha.ni kweli vita ilikuwa kati ya mrusi na germany nakumbuka pia usa na japan naye ilikuwa mechi kali sana.
Hivi mkuu kama US asingekuw front, je mjapani angemsaidia mjeruman dhidi ya mrusi?.
Je, vikosi vya ujeruman vilivyokuwa upsnde wa magharibi visingstoa support huko east?
 
Yeah .. nilisahau na hiii . Nadhani iliitwa operation Torch kama sikosei.. na ilikuwa inasimamiwa na Erwin Rommel.

Umechanganya kidogo, Operation Torch ilikuwa ni uvamizi wa Allied Forces (Marekani na Uingereza) dhidi ya Afrika Kaskazini kwenye nchi zilizokuwa chini ya ukoloni wa Wafaransa. Lengo lilikuwa ni kuzuia Axis Powers (Germany na wenzie) wasikite udhibiti wao dhidi ya hizo nchi.
Kumbuka baada ya Ufaransa ku surrender Germany iliunda dola kibaraka kwa ajili ya Ufaransa (Vichy France), so Allied Forces waliivamia North Africa kuondoa udhibiti wa Vichy France kwa nchi hizo na kuondoa majeshi ya Axis Powers huko na kukata supply yao. Na pia kudhibiti routes za Mediterania kwa ajili ya usafirishaji na supplies zao Allies (akina Uingereza na wenzao).

Pia miongoni mwa malengo ya Operation Torch ilikuwa ni kuirahisishia Marekani katika combat kwenye Western front na kuipunguzia pressure Uingereza kule Misri (Misri ilivamiwa na Italy mwaka 1940 baada ya Italy kutangaza vita dhidi ya Uingereza, nchi za Jumuiya ya Madola na dhidi ya Ufaransa ("Free" France) na waliivamia Misri ili waikamate Suez Canal na baadae akina Rommel wakapelekwa kuongeza nguvu) na pia Allied Forces walitaka kuipunguzia pressure USSR kule East kwa kuilazimisha Ujerumani kupunguza attention na focus yake kule East.

Operation Torch ilikuwa ni Novemba mwaka 1942.
 
Yeah .. nilisahau na hiii . Nadhani iliitwa operation Torch kama sikosei.. na ilikuwa inasimamiwa na Erwin Rommel.
Rommel ("The Desert Fox") alipelekwa North Africa kumsaidia Italy, swahiba wa Germany, ambaye alikuwa anaelemewa. Alipelekwa mwaka 1941.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…