Hili suala la wanafunzi kubaki shule lina umuhimu mkubwa kwa maisha ya baadaye ya mtoto wako

Sijakataa likizo wasiende bali vidato vya mitihani wabaki.
Wakati unasoma wewe ulienda likizo kwa vidato vya mitihani?? Kma ni ndio basi tunaanza kujenga taifa la vilaza
Likizo ni muhimu mkuu hawa watoto wanayakujifunza mengi huko nyumbani ikiwemo utu.

Embu fikiria wakati mtoto yupo shule alifiwa na ndugu huko mkoani let say baba mdogo, bibi, shangazi nk. na hakupata wasaa wakuhururia, kipindi cha likizo ndio hukitumia kwenda kuona hata mahali walipolala wapendwa wao. Tusiharibu tamaduni zetu jamani tukitumia ratiba na usimamizi mzuri watoto watafaulu tu. Pia tukae tukijua kuwa elimu ni pyramid in shape sasa hofu ya nini?
 
Ndio maana ikaitwa likizo, mtoto arudi nyumbani kupumzisha akili, kusaidia wazazi, kujisomea akiwa nyumbani, wazazi wafahamu tabia za mtoto.

Elimu ya darasani sio kila kitu katika makuzi!!
Kijijini atakwenda shambani, mjini atazurura mitaani na mimba zitaongezeka
 
Ulifaulu level gani? Wakati wako siyo sawa na wakati tuliopo
 
Mkuu sisi enzi zetu ikifika lilizo tulikuwa tunaruhusiwa kwenda nyumbani lakini tulifaulu masomo vizuri. Walimu hakikisheni mnakwenda na syllubus vizuri na kwa wakati! Lakini kwa habari ya Afya watoto waruhusiwe kupumuzika.
Wameenda tunawasubiri July break ya kwanza ni kuwapima mimba hapo Kila mmoja atabeba mzigo wake
 
Wewe unamlea mwanao na kusimamia maadili ya mwanao Kama mhindi??

Au unataka ucopy sehem tuu ya maisha ya wahindi na sio ful?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kijijini atakwenda shambani, mjini atazurura mitaani na mimba zitaongezeka
Kama mzazi unashindwa kumsimamia mtoto kipindi kifupi cha mwezi mmoja tu unafaa kuitwa mzazi kweli? Ulizaa ili nani abebe majukumu yako kama likizo ya mwezi mmoja tu inakushinda kukaana mtoto.
 
Mazingira yanatofautiana. Watoto kubakizwa shule ni makubaliano ya mzazi na mwl na hata watoto wenyewe na mwl. Mazingira ya mijini siyo sawa na ya vijijini. Watoto wengine ni wasahailifu sana, akikaa wiki moja hajaahika daftari, akija kufungua mwl unaanza nae upya hakuna anachokikumbuka.
 
Kama mzazi unashindwa kumsimamia mtoto kipindi kifupi cha mwezi mmoja tu unafaa kuitwa mzazi kweli? Ulizaa ili nani abebe majukumu yako kama likizo ya mwezi mmoja tu inakushinda kukaana mtoto.
Kumbe hujui malezi ya watoto wengi wa Sasa? Nenda hapo unga Ltd watoto wengi zaidi ya 90% wanalelewa na single parent na wengine ni bibi au Babu zao hakuna Cha wazazi
 
walimu fanyeni kazi bila kuchoka mtalipwa na Mungu yani hakuna watu watata kama wazazi wa sasa tena wanavijihela eti ukimchapa mtoto wao wamempigia mkurugenzi mara DO mara Afisa Elimu yani shida tupu sasa matokeo yanazidi kuwa mabaya hasa kwa sisi wa kata wenzetu (st francis na kemebos) hawana shida nimekaa pale nayasubiri matokeo ya Fuoni, changarawe, Temeke na Urafiki
 
Mzazi unalilia Mtoto wa Form four au form six arudi likizo???? Ndo zile familia za dady and mammii kichwani wazazi wanadhani kumpeti peti mtoto ndo kumpendaa...wazazi wa ovyooo sanaaaa kwani mwanao akimaliza Mtihani hutamuona??? Kaa nae hapo nyumbani bhasi asiende shule kabisaa ili uwee unamuonaa kila sikuuu.. shwain kabisa
 
Unadhani wakibaki Likizi mojaa bila kwenda Nyumbani kuna kitu gani kikubw watapungukiwaa??? Kubaki shule ni kupata muda mzuri wa kujiandaa na mitihani na hata waalimu huwa hawafundishi mostly ni nyie kujisomeaaa huku mmerelax... Sasa huo ujinga sijui kamiss ndugu mara apumzishe akiliii ni ovyoo sanaa.
 
TATE unaupiga mwingi hadi naogopa.
 
Kumbe hujui malezi ya watoto wengi wa Sasa? Nenda hapo unga Ltd watoto wengi zaidi ya 90% wanalelewa na single parent na wengine ni bibi au Babu zao hakuna Cha wazazi
Kwa hiyo single parent yeye hana uwezo wa kulea mtoto wake, yeye abaki tu shuleni kisa mama/baba yake hawezi kukaa nae mwezi mmoja wa likizo.

Acheni excuses za ajabu wakuu, walioweka vipindi vya mapumziko walijua ubongo unahitaji nini ili ukue. Unataka mtoto ajifunze Ax² + Bx + C = 0 mwaka mzima asifundishwe mambo mengine ya kimaisha? Usipoishi na mwanao utamfundishaje tabia njema, utatengeneza lini bond kati yenu?
 
Acheni kutetea ujinga na upimbi ,inawezekanaje mtoto wa miaka kumi na moja anapigishwa kwata ya kusoma kuanzia saa kumi na mbili asubui hadi saa tatu usikua kwa siku saba na bado unataka watoto husika wasipewe likizo ?
 
Anakaa nae saangapi wakati yupo samunge anauza mchicha apate mahitaji ya mtoto au mjukuu? Sasa yeye akiwa samunge, mtoto yupo vibanda vya movie. Je vibanda vya movie na shuleni wapi Bora?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…