Watoto waende likizo hakuna kazi isiyo na likizo tena kwa watoto wetu kupumzika ni muhimu sana. Mtoto akajifunze mambo mengine ya kimaisha mzazi mpeleke kijijini achunge,alime,apasue Kuni,salimie ndugu,ajifunze kilugha na milazao,acheze mitaani,akauze bidhaa sokoni nk.
Elimu yetu inakosa mpangilio mzuri wengine tulishauri mpangilio wa semister tatu mfumo uwe kamahivi;
3 Jan mpaka 31 machi - masoma(miezi 3).
1 April mpaka 30 April - likizo ya kwanza(mwezi 1).
1 may mpaka 31 July - masomo(miezi 3).
1 august mpaka 31 august - likizo ya pili(mwezi 1).
1 September mpaka 30 November - masomo(miezi 3).
1 December mpaka 2 January - likizo ya tatu(mwezi 1).
**Watoto watasoma jumla siku 180 (miezi 9 × 20 siku kwamwezi) ambazo zinatosha hazitofautiani na siku za masomo kwasasa!!
Darasa la saba wasome semister mbili tuu wafanye mtihani wa taifa Kisha Semister ya tatu (miezi mitatu) wanafunzi wa darasa la saba wafundishwe English na maths tuu kujiandaa kwenda sekondari, walimu wa sekondari wapelekwe primary wakati huo kusaidia ufundishaji maana sekondari kunakuwa hakuna mzigo mkubwa na walimu Huwa wengi sekondari nyingi kuzidi msingi!!
Serikali imekuwa nzito sana kufanya maamuzi katika elimu jambo linalozorotesha sana elimu yetu nakuongeza mdororo wa elimu kuwa na wahitimu wenye uwezo mdogo saaana hata katika kujieleza na kujisomea.