Hili Taifa Vijana wangetumia ⅓ ya Akili zao leo hii tungekuwa Taifa kubwa kiuchumi zaidi ya Taifa la Marekani!

Hili Taifa Vijana wangetumia ⅓ ya Akili zao leo hii tungekuwa Taifa kubwa kiuchumi zaidi ya Taifa la Marekani!

Hili taifa Vijana wangejitambua wakasimamia Rasilimali Tulizonazo ingewezekana kabisa mkuu!
Vijana wangesimamia wapi wakati serikali ndiyo kila kitu?
Paypal vijana wamepiga kelele lkn yule bibi kaziba masikio. Vijana wafanyaje?
Nchi yoyote duniani imeendelea kwa uwepo wa ushirikiano mzuri kati ya serikali na vijana
 
Mkuu wewe enzi za ujana wako uliacha legacy gani mtaani ulipoishi?

Kama huna nauli niambie nikutumie uende hadi Tarime ukajionee mambo niliyo yafanya!

Nakutumia nauli ya Ndege (Air Tanzania au Precision ) unatua Mwanza then unapanda Zakaria au Kisire hadi Tarime kisha unaelekea Rebu ukajionee nilichofanya!
 
Tatizo lipo kwenye kumjua mjinga ni nani na mwerevu ni nani..

All in all, hii nchi haina generation ya kuicheka generation nyingine kwenye masuala ya kitaifa. Wote kuna namna imeonesha failure

Wazee wameirithisha nchi kwa vijana ikiwa imegawanyika bila system yoyote hivyo, sidhani kama walitegemea kupata matokeo tofauti na mfumo walioulea na kuukuza wenyewe.

Mkuu ulipata Divesheni ngapi Form 4 kwa Combination gani,nadhani hili ni muhimu sana!
 
Vijana wangesimamia wapi wakati serikali ndiyo kila kitu?
Paypal vijana wamepiga kelele lkn yule bibi kaziba masikio. Vijana wafanyaje?
Nchi yoyote duniani imeendelea kwa uwepo wa ushirikiano mzuri kati ya serikali na vijana

Serikali ni nani? Nani anayo ichagua?

Vijana acheni sababu za Kijinga wehu nyie!
 
Kijana umeamua kukimbia aibu!
Ndio mkuu nimeogopa kuaibishwa na wewe "genius". Level yako ya intelligence ni kubwa sana kunizidi kwa hiyo haina maana kuendelea na discussion yoyote ilhali kuna great thinkers wengi unaoweza jadili nao humu.
 
Form 4 nilipata division 2 ,combination ya PCB that's why najiamini sana mkuu!
 
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!

Ukiona viongozi wa Serikali wana wang'ang'ania wazee kwenye nafasi nyeti tambua ya kwamba vijana watakuwa na matatizo ya kiakili,Vijana wengi waliopewa nafasi ili waonyeshe uwezo wao wamekuwa wapumbavu kuliko hata wazee waliochokaa!.
Usipoteze muda wala nguvu zako ktk kufuatilia maisha ya vijana wa Tz, unaweza kufa kwa presha ya moyo au msongo wa mawazo. Achana nao, akili zao wanazijua wao wenyewe.

Jaribu kufikiria, kampuni moja inatoa tangazo la kazi kwa vijana mtandaoni, tangaxo hilo Lina muda wa miezi mitatu, lakini tangazo hilo limetazamwa na viewers wapatao 35 tu kwa muda wote huo wa miezi mitatu, walati huo huo kuna habari ya udaku kwamba "Wema Sepetu Apata Bwana Mwingine Mpya", na habari hii imewekwa mtandaoni yapata masaa matatu yaliyopita, lakini ukiangalia idadi ya watazaji wa hanari unaona wapo viewers laki tatu ambao wamesoma hanari hiyo. Hii ni ajabu sana, hizi ndio akili walizonazo vijana wa Tz.
 
Wa kulaumiwa ni vijana wa zamani ambao wengi wao ndo walitunga sheria za kishenzi na kuhusika kwenye ufisadi wa kutisha hali ambayo inamgharimu kijana wa leo. Viwanda vilivyokuwa vinatoa ajira viliuliwa na vijana walioenda kumpokea Harmonize? Sheria ngumu za mambo ya kodi na biashara zilitungwa na vijana wa mapokezi ya Harmonize? Wewe mzee mwombe sana mwenyezi Mungu hao vijana wasije kuamua kutaka kujua yaliyofanywa na vijana wa zamani ambao ndo wazee wengi wa sasa tunaowaita vigogo.
 
Mkuu mimi ni Kijana wa Kitanzania,haya uliyoandika yapo kwa kiasi fulani lakini sio ukweli kamil,Tanzania ni kubwa tena kubwa sana,na unapozungumzia vijana wote bila kutofautisha hata kidogo unakuwa unakosa adabu ya kufikiri vizuri,

Nafikiri huu sio wakati wa kulaumu bila kuja na suluhisho kwa jamii yetu na vijana wenzetu,,,

Nawajua vijana wengi tu wa Kitanzania ambao wanafanya vizuri katika maisha ya kazi na ujasiriamali pia,,

Labda nikuulize swali,,ni kipi umeshakifanya kuwasaidia vijana wenzako au taifa lako mpako sasa?maana tusiwe kama wapumbavu kwa kila siku kulalamika humu kumbe tunakaa kwa shemeji zetu na sisi wenyewe ni sehemu ya tatizo kwa kushinda humu kuandika andika ili tupate umaarufu,,

Binafsi nimetoa ajira kwa vijana wenzangu na pia nahamasisha vijana wenzangu kuingia katika sekta ya madini.
 
Mkuu achana na muda waliopoteza wao kwakuwa hawana cha kufanaya na wala cha kufikiria.

Swali nililojiuliza ni kwamba kutokana na mwendo wa yale maandamano kuwa na mwendo wa polepole je,serikali haijaona kama kumefanyika ucheleweshwaji wa shughuli za usafirishaji kwa watumiaji wengine wa barabara?

Mwisho wa siku unakuja kugundua kwamba serikali kuna namna inanufaika na mambo ya hovyo yanayowateka vijana kama haya ili washindwe kuhoji vitu vya msingi kama ajira,elimu,maji,umeme na huduma nyingine nyingi za muhimu kwa jamii.

Hii nchi tunapigwa sana hasa sisi vijana kwasababu hatujitambui.
 
Usipoteze muda wala nguvu zako ktk kufuatilia maisha ya vijana wa Tz, unaweza kufa kwa presha ya moyo au msongo wa mawazo. Achana nao, akili zao wanazijua wao wenyewe.
Jaribu kufikiria, kampuni moja inatoa tangazo la kazi kwa vijana mtandaoni, tangaxo hilo Lina muda wa miezi mitatu, lakini tangazo hilo limetazamwa na viewers wapatao 35 tu kwa muda wote huo wa miezi mitatu, walati huo huo kuna habari ya udaku kwamba "Wema Sepetu Apata Bwana Mwingine Mpya", na habari hii imewekwa mtandaoni yapata masaa matatu yaliyopita, lakini ukiangalia idadi ya watazaji wa hanari unaona wapo viewers laki tatu ambao wamesoma hanari hiyo. Hii ni ajabu sana, hizi ndio akili walizonazo vijana wa Tz.
Mkuu ni vyema ungeambatanisha picha au link ya hayo matangazo mawili( la kazi na la wema sepetu) isije ikawa habari yako ya kupikwa tu
 
Back
Top Bottom