Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Amani iwe nanyi!
Kama kichwa cha mada kinavyosema, kwa muda mrefu sasa nimegundua kwa nini mwalimu nyerere alitamka kuwa moja wa maadui wakubwa wa Tanzania ni ujinga! Nasikitika kusema pia, kuwa hatujaweza kumuondoa huyu adui ujinga!
Mwana jf samurai katika uzi unaoelezea Mhe Rais kufanya kikao usiku kujadili bei ya mafuta ameelezea shida ya Watanzania kuwa na tatizo la kufikiri huku akitaja Lishe kama tatizo linalopelekea jambo hilo!
Ingawa naungana na samurai kwa upande fulani kwa sababu hata tafiti zilizowai kufanywa zinadai chakula kinachotokana na mahindi kinadumaza akili na kufanya mtu asifikiri vizuri! Hivyo chanzo cha ujinga wetu kinaweza kuwa kinasababishwa kwa kiasi kikubwa na ulaji wa ugali!
Mwaka 2020 Mgombea uraisi Hashimu Rungwe Spunda alikuja na hoja ya lishe kwenye kampeni yake! Ingawa wengi tilimdharau ila huyu mtu alikuwa na hoja ya maana sana!
Napenda leo nielezee kwa ufupi mifano michache tu ya kwa nini nasema ujinga ni Tatizo kubwa kwa Watanzania?
Royal Tour
Kwa miaka yote ukiondoa kipindi cha covid , sekta ya Utalii ndo imekuwa ikichangia kwa sehemu kubwa zaidi kwenye pato la taifa. Hii inamaanisha mapato mengi ya serikali yanachangiwa kwa sehemu kubwa zaidi na sekta ya utalii!
Kutokana na kutoelewa hii dhana kwa Watanzania wengi, hawajui kuwa fedha zinazolipa mikopo tunayokopa, zinazolipa mishahara ya watumishi wetu , zinazojenga barabara, zinazonunua madawa hospitalini, zinazojenga miradi ya maji kwa miaka mingi na karibu yote fedha hizi kwa sehemu kubwa zinatokana na mapato yanayotokana na utalii.
Hivyo ukiona Rais anafanya jitihada kubwa kuinyanyua sekta hiyo! Tena kwa ubunifu wa kutumia fedha za wadau na sio za serikali, alafu kuna watu wanakebehi, basi ujue shida sio Rais bali shida ni upeo wa watu husika au kwa lugha rahisi ni ujinga wa watu husika.
Bei ya Mafuta
Hapa ndo utafurahi zaidi! Watanzania wengi wamejikuta kwenye mkumbo wa kushabikia vita kati ya Russia na Ukraine. wengi hata ukiwasoma humu kama yeriko Nyerere wameandika hadi mada humu kuunga mkono Russia kuvamia Ukraine. Ukifuatilia mfano mada za humu JF tu kipindi vita vinaanza kwa ujinga tu wengi walianza kuwalaaani West kana kwamba West ndo alianza vita dhidi ya Ukraine.
Kwa ujinga tu kwa sababu wengi hawajui, kila vita kubwa iliyowai piganwa duniani imewahi kuleta economic depression. Economic depression ina njia nyingi ikiwemo kupandisha bei ya bidhaa na hata kuleta uhaba wa bidhaa!
Urusi ndo mzalishaji wa pili wa mafuta na gesi ulimwenguni. Vita yake na Ukraine imekwenda kusababisha vikwazo kwake kwenye kuuza mafuta hasa ulaya. Hilo limesababisha demand kubwa ya gesi na mafuta Ulaya na duniani kwa ujumla hivyo bei kupanda.
Pamoja na Serikali yetu kuweka kodi kwenye mafuta ambayo ndo imekuwa ikishusha gharama ya umeme vijijini lakini kodi iyo imekuwa ikipelekwa kwenye miradi mingine ikiwemo barabaraza vijijini na kuunganisha umeme vijijni. Kuondoa kodi ghafla kwenye hili eneo inamaanisha moja kwa moja hii miradi inaenda kuathirika pakubwa na ndo mana serikali inakuwa makini sana kufanya maamuzi haya magumu. ila kwa ujinga wa Watanzania wengi hili nalo linaenda kwa lawama tu!
Napenda kuihasa serikali yangu, kufanyia kazi haswa tatizo la ujinga kwa kuanza kuhamasisha lishe mbadala kwa ugali! Nchi hii ujinga ni tatizo kubwa sana zaidi ya tunavyodhani!