Hitimisho langu: Ujinga ni tatizo kubwa sana kwa Watanzania

Tumeomba Kodi zipunguzwe ili hiki kipindi kigumu kipite kwanza.

Halafu ukija kuzalisha mazao yako ukose pakuuza maana tarura watakuwa hawajamaliza hizo barabara kijijini kwa sababu kodi zimepunguzwa
 
Hujanielewa nimesema kipindi cha dharura.
 
Nakubaliana na wewe kwa upande fulani! Ujamaa nao umechangia sana udumavu wa akili za Watanzania
Ni tatizo la kimfumo - huu mfumo huu wa SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA tangu uasisi wa Taifa letu ndiyo umetufikisha hapa.

Mfumo huu umetujengea hofu, kutojiamini, kujipendekeza mbaya zaidi bado unaambukiza hadi vijana wadogo kujikombakomba kisiasa. Mimi nafikiri baada ya kugundua mfumo huu umefeli Mwalimu angeuondoa na kutupatia Katiba Mpya mapema miaka ya 90, sasa hivi watawala sidhani wangekuwa wanatufanyia utani utani namna hii.

Sasa haya ndiyo matokeo yake kwamba badala ya wananchi kudai haki zao wao wanalilia vifuani huku wakiomba Mungu awasaidie.
 
Amani iwe nanyi!

Kama kichwa cha mada kinavyosema, kwa muda mrefu sasa nimegundua kwa nini mwalimu nyerere alitamka kuwa moja wa maadui wakubwa wa Tanzania ni ujinga! Nasikitika kusema pia, kuwa hatujaweza kumuondoa huyu adui ujinga!

Mwana jf samurai katika uzi unaoelezea Mhe Rais kufanya kikao usiku kujadili bei ya mafuta ameelezea shida ya Watanzania kuwa na tatizo la kufikiri huku akitaja Lishe kama tatizo linalopelekea jambo hilo!

Ingawa naungana na samurai kwa upande fulani kwa sababu hata tafiti zilizowai kufanywa zinadai chakula kinachotokana na mahindi kinadumaza akili na kufanya mtu asifikiri vizuri! Hivyo chanzo cha ujinga wetu kinaweza kuwa kinasababishwa kwa kiasi kikubwa na ulaji wa ugali!

Mwaka 2020 Mgombea uraisi Hashimu Rungwe Spunda alikuja na hoja ya lishe kwenye kampeni yake! Ingawa wengi tilimdharau ila huyu mtu alikuwa na hoja ya maana sana!

Napenda leo nielezee kwa ufupi mifano michache tu ya kwa nini nasema ujinga ni Tatizo kubwa kwa Watanzania?

Royal Tour
Kwa miaka yote ukiondoa kipindi cha covid , sekta ya Utalii ndo imekuwa ikichangia kwa sehemu kubwa zaidi kwenye pato la taifa. Hii inamaanisha mapato mengi ya serikali yanachangiwa kwa sehemu kubwa zaidi na sekta ya utalii!

Kutokana na kutoelewa hii dhana kwa Watanzania wengi, hawajui kuwa fedha zinazolipa mikopo tunayokopa, zinazolipa mishahara ya watumishi wetu , zinazojenga barabara, zinazonunua madawa hospitalini, zinazojenga miradi ya maji kwa miaka mingi na karibu yote fedha hizi kwa sehemu kubwa zinatokana na mapato yanayotokana na utalii.

Hivyo ukiona Rais anafanya jitihada kubwa kuinyanyua sekta hiyo! Tena kwa ubunifu wa kutumia fedha za wadau na sio za serikali, alafu kuna watu wanakebehi, basi ujue shida sio Rais bali shida ni upeo wa watu husika au kwa lugha rahisi ni ujinga wa watu husika.

Bei ya Mafuta
Hapa ndo utafurahi zaidi! Watanzania wengi wamejikuta kwenye mkumbo wa kushabikia vita kati ya Russia na Ukraine. wengi hata ukiwasoma humu kama yeriko Nyerere wameandika hadi mada humu kuunga mkono Russia kuvamia Ukraine. Ukifuatilia mfano mada za humu JF tu kipindi vita vinaanza kwa ujinga tu wengi walianza kuwalaaani West kana kwamba West ndo alianza vita dhidi ya Ukraine.

Kwa ujinga tu kwa sababu wengi hawajui, kila vita kubwa iliyowai piganwa duniani imewahi kuleta economic depression. Economic depression ina njia nyingi ikiwemo kupandisha bei ya bidhaa na hata kuleta uhaba wa bidhaa!

Urusi ndo mzalishaji wa pili wa mafuta na gesi ulimwenguni. Vita yake na Ukraine imekwenda kusababisha vikwazo kwake kwenye kuuza mafuta hasa ulaya. Hilo limesababisha demand kubwa ya gesi na mafuta Ulaya na duniani kwa ujumla hivyo bei kupanda.

Pamoja na Serikali yetu kuweka kodi kwenye mafuta ambayo ndo imekuwa ikishusha gharama ya umeme vijijini lakini kodi iyo imekuwa ikipelekwa kwenye miradi mingine ikiwemo barabaraza vijijini na kuunganisha umeme vijijni. Kuondoa kodi ghafla kwenye hili eneo inamaanisha moja kwa moja hii miradi inaenda kuathirika pakubwa na ndo mana serikali inakuwa makini sana kufanya maamuzi haya magumu. ila kwa ujinga wa Watanzania wengi hili nalo linaenda kwa lawama tu!

Napenda kuihasa serikali yangu, kufanyia kazi haswa tatizo la ujinga kwa kuanza kuhamasisha lishe mbadala kwa ugali! Nchi hii ujinga ni tatizo kubwa sana zaidi ya tunavyodhani!
Ndugu usishangae Sana ,kama jamii kubwa ya watu wanaamini ushirikina then unadhani kuna mtu wa kutumia akili hapo?

Takwimu hazidanganyi ,soma hii hapa 👇

Screenshot_20220506-163547.png

JamiiForums-2119221646.jpg

IMG_20220118_123054.jpg
 
Umeandika utoporo mtupu.
We naye ni sehemu ya hayo majinga unayoyasema.

Mfano, hayo mafuta Zambia ni bei ya chini kuliko Tanganyika; Zanzibar ni bei ya chini kuliko Tanganyika. Nchi zenye bei ndogo ya mafuta ziko mbinguni ambako hakuna vita ya Ukrain na Urusi?????

Royotua imetumia bilioni 7, kipindi hiki ni cha kutumia bilioni 7 kwa royotua???

Jinger kabisa wewe
 
Tupe takwimu za bei ya mafuta Zambia

Kwani kuna shida gani Royal Tour ikitumia bil 7 pesa ambazo hazijatoka mfuko wa hazina?
 
Mkuu
Sisi sio wajinga
Tunahoji masuala mazito Sana!
Lakini majibu tunayopewa ni ya hovyo na mepesi
Royal tour imekaa kisanii sana
Tanzania ina vivutio vingi vya kitalii halafu tuna wasanii pia kwanini na wao wasishirikishwe kwenye hiyo tour na iwe endelevu!!?
Mikataba ya uwekezaji ya madini unajua tunapata sh ngapi na kwanini!!?
Kuna vitu vinafichwa Ili kubariki upigaji fulani!!!
 
Mimi sifichi naweka wazi......ujinga wetu watanzania unatokana na kujitakia sisi wenyewe haswa kwa kuzishabikia hizi dini za kuletewa bila kujuwa ukweli wake. Wamekuja Waarab na wazungu na kutuambia kuabudu chini ya mti au jiwe ni ushetani wakati wao huko Israel na Uarabuni wanafanya hayo hayo kuabudu na kuzunguka jiwe (kaaba). Tunataabika waafrika sabbu tumekana mila na desturi zetu kufuata mila na desturi za wengine. Mwanamke anavaa magunia mwilini kuiga waarab na anaona sifa, kama huu si ujinga ni kitu gani?
Hahaha..mkuu wamasai wanafuata mila zao kikweli kweli hadi leo.
 
Research moja pekee inatosha inayoeleza kwamba Africa ndio bara masikini kuliko mabara yote Ulimwenguni !! Pamoja na Rasilimali zote ilizojaaliwa na Mungu bado ndiyo masikini kuliko mabara yote !! Mtoa mada Lord denning ameliona hili !! Kumbe sababu ni UGALI !
Wengine tunajua kuwa wanga husababisha maradhi mengi na kibaya vyakula vya wanga ndio vilivyo tawala si Tanzania au Afrika tu bali duniani, wazungu wenyewe washaandika sana vitabu kuelezea madhara ya wanga kwa afya. Sasa ajabu iwe kwamba wanga huo ndio usababishe kukosa akili kwa waafrika tu ila wazungu wale wanga ila wawe na akili?
 
Tatizo la nchi hii wala sio ugali unausingizia tu ugali..tatizo la nchi hii ni ccm na viongozi wake ambao wameshapoteza misingi ya uongozi wa wanancho na kugeukia matumbo na familia zao.

#MaendeleoHayanaChama
Labda jamaa atuambiwe hao viongozi wake wanakula nini?
 
Mtoa mada wewe na ccm ndo wajinga kwa sababu unazozitoa zimeletwa na ccm hii hii. Na unafanya makusudi ili iendlee kutawala. Ccm ndo Ina uwezo wa kuondoa huo ujinga unaouongelea. Lkn ndo inayoundeleza.

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
Kwa sababu yeye leo chawa wa Samia ndio anaona watanzania wajinga ila huko nyuma hakuona ujinga wa watanzania, yani sasa hivi hawataki kuona watu wakitoa maoni yasiyo mfurahisha Samia na ndio kuna chawa mwengine kafikia kusema hii mitandao ipigwe ban.
 
Wali una kiasi kidogo cha wanga kuliko ugali, wachina chakula chao kikuu ni wali ila kiwango cha kiribatumbo ni kidogo sana.
Ukizungumzia afya hata wali sio sahihi kwa afya.
 
Ndugu usishangae Sana ,kama jamii kubwa ya watu wanaamini ushirikina then unadhani kuna mtu wa kutumia akili hapo?

Takwimu hazidanganyi ,soma hii hapa 👇

View attachment 2218669

View attachment 2218670

View attachment 2218671
Wahindi wanaamini ushirikina tena kwenye biashara na bado wanafanya vizuri kwenye biashara huku kuamini ushirikina hata sio sababu kwa sababu hakuna ambaye hataki kufanya kazi kisa anaamini ushirikina. Hao vipngozi wako huko karibu wote wanaamini ushirikina ila wewe una waamini kuwa wataleta maendeleo.
 
Wali una kiasi kidogo cha wanga kuliko ugali, wachina chakula chao kikuu ni wali ila kiwango cha kiribatumbo ni kidogo sana.
Kuna kitu kinaitwa Glycemic index unakijua ni nini tunapoongelea haya masuala ya afya?
 
Wengine tunajua kuwa wanga husababisha maradhi mengi na kibaya vyakula vya wanga ndio vilivyo tawala si Tanzania au Afrika tu bali duniani, wazungu wenyewe washaandika sana vitabu kuelezea madhara ya wanga kwa afya. Sasa ajabu iwe kwamba wanga huo ndio usababishe kukosa akili kwa waafrika tu ila wazungu wale wanga ila wawe na akili?
Shangaa na wewe Tz mbongo !! Watu wamekalia uchawa tu ! Hawataki kuona wengine wanakosoa !! Nilimsikia mtaalamu wa lishe akisema wanga ndio chanzo kikuu cha nishati mwilini lakini mtoa mada anasema ndio chanzo cha ujinga Africa !!!
 
Back
Top Bottom