Hitimisho langu: Ujinga ni tatizo kubwa sana kwa Watanzania

Mbaya zaidi hota ya msukuma eti tukope kupunguza bei ya mafuta ilipigiwa makofi bungeni
 
Mimi sifichi naweka wazi......ujinga wetu watanzania unatokana na kujitakia sisi wenyewe haswa kwa kuzishabikia hizi dini za kuletewa bila kujuwa ukweli wake. Wamekuja Waarab na wazungu na kutuambia kuabudu chini ya mti au jiwe ni ushetani wakati wao huko Israel na Uarabuni wanafanya hayo hayo kuabudu na kuzunguka jiwe (kaaba). Tunataabika waafrika sabbu tumekana mila na desturi zetu kufuata mila na desturi za wengine. Mwanamke anavaa magunia mwilini kuiga waarab na anaona sifa, kama huu si ujinga ni kitu gani?
 
Uzuri uliopo ni kwamba sote wakubwa kwa wadogo nchini tunakulaga UGALI !! itabidi tubadili hii menu kumbe ndio inayotuletea matatizo mengi !!
 
Tukiachana na kauli za mwalimu, sasahivi kilaa kitu kimepanda bei na sababu kubwa ni bei ya mafuta' na hii inaumiza raia wote'

Ukipiga hesabu zaidi ya nusu bei ya mafuta ni kodi. Na hii inaenda hata mpaka kwenye uagizaji wa magari na vitu vingine.

Sasa unaanzaje kuwa na wazo la kujenga kiwanda wakati mapato unayopata kwenye kodi ni makubwa kuliko ya kiwandani? Japo hayo mapato unayopata yanawatesa na kuacha familia ktk maisha magumu kiasi hata kumudu mlo kamili kwa siku ni shida!

Hayo yote yanasababisha umasikini, njaa na maradhi.

Ni sawa jenga barabara sambaza umeme jenga hospl mafly over na kila kitu kizuri lakini pakitokea majanga unaendeleaje na bajeti yako kama hakuna kilichotokea? Uliweka hela ya dharura/majanga au akiba? Kama mafuta ni muhimu ulihifadhi? Vp chakula umehifadhi?

Kwenye familia hata ng'ombe huuzwa pakitokea majanga na ni kwaajili ya kurudisha maisha ya familia ktk hali ya kawaida. Na huu ndo wajibu wa mwenye kaya.

Juzi nilimsikia moja anajibu swali bungeni, "serekali inazo hifadhi za mafuta lakini mafuta yaliopo kwenye hifadhi hizo sio mali ya serekali, ni ya wafanyabiashara"!

Huu ndo ujinga unaosababisha njaa umaskini na marafhi.

Kiufupi ni kama tunaongozwa na genge la mchwa wanaotamani na kula bila hata kuweka akiba, kila kitu watasingizia vita.
 
Najaribu kulink Ujinga na lishe Mana hata hao wanaokuka balanced diet ndio mstari wa mbele kwa ujinga.

Anaejua Ubongo unatumia aina gani ya chakula Kama fuel atueleze.
 
Mkuu umekomalia Sana hili swala .

Ni research paper ipi inayosapoti hii claim.
Research moja pekee inatosha inayoeleza kwamba Africa ndio bara masikini kuliko mabara yote Ulimwenguni !! Pamoja na Rasilimali zote ilizojaaliwa na Mungu bado ndiyo masikini kuliko mabara yote !! Mtoa mada Lord denning ameliona hili !! Kumbe sababu ni UGALI !
 
Umeongea mengi lakin kitendo cha kuusema ugali inadhihirisha hujui ni raha kiasi gan kula ugali na samaki wa kukaanga au nyama choma
Hajui!!

I am coming out! I am coming out!
Natoka! Natoka!
 
Ni sahihi kabisa, vyakula vya wanga ambavyo ndiyo vyakula mama kwa Afrika vinasababisha akili zetu kudumaa.
Tatizo kubwa sio vyakula wanga bali aina ya wanga. Sembe ni janga kubwa lakini zaidi kuna watu wanakula hiyo sembe na mchicha tu, Watu wanakunywa chai ya rangi na mihogo au vitumbua, watoto wanapewa uji mweupe wenye sukari tu n.k Kwa mtindo huu wa ulaji akili lazima zidumae.
 
Tatizo la nchi hii wala sio ugali unausingizia tu ugali..tatizo la nchi hii ni ccm na viongozi wake ambao wameshapoteza misingi ya uongozi wa wanancho na kugeukia matumbo na familia zao.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ni raha lakini ugali hasa wa sembe sio chakula sahihi kwa afya yako.
Umeongea mengi lakin kitendo cha kuusema ugali inadhihirisha hujui ni raha kiasi gan kula ugali na samaki wa kukaanga au nyama choma
 
Lishe bora inatakiwa kuanzia utotoni, ubongo wa mtoto huwa unakuwa na kuwekewa msingi katika kipindi cha miaka mitano ya mwanzo, ukiharibu hapo huko mbeleni hata ukila balance diet haina maana sana.
Najaribu kulink Ujinga na lishe Mana hata hao wanaokuka balanced diet ndio mstari wa mbele kwa ujinga.

Anaejua Ubongo unatumia aina gani ya chakula Kama fuel atueleze.
 
Mleta mada angetakiwa aongelee tatizo la lishe mbovu kwa ujumla, yeye amejikita kwenye ugali tu.
Uzuri uliopo ni kwamba sote wakubwa kwa wadogo nchini tunakulaga UGALI !! itabidi tubadili hii menu kumbe ndio inayotuletea matatizo mengi !!
 
rubbish,endelea kumtetea huyo kungwi wako,kashindwa uongozi wa nchi mapema sana
 
Nilikuwa sijui Kama na ww umo miongoni mwa wajinga wengi wa tanzania.
 
Kina his initials zaidi ni jinsi ambavyo nawe umeathiriwa na ulaji Wa ugali.Hayo ya kupambana na ujinga kumefanyika tangia tupate UHURU hadi leo,chini ya utawala Wa wanaopenda na kufurahia ujinga Wa watu wake ili waendelee kutawala.Sina kipimo cha ujinga na werevu Wa wananchi kama ulivyofanya mtoa mada ila ninapata shida sana kufahamu ujinga Wa wasomi unawezaje kuondolewa?
Ujinga ni tabia na kichaka cha watu wavivu kufikiri na waoga Wa kuthubutu.Ndiyo maana hata suala la Katiba Mpya linavyobishaniwa.
 

Uko sahihi kwenye hili suala la ujinga. Na kwa taarifa yako huo ujinga ndio unaosababisha hadi Leo ccm isalie madarakani. Hivyo kwa namna Moja au nyingine utawala huu ni matokeo ya ujinga huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…