Hitimisho langu: Ujinga ni tatizo kubwa sana kwa Watanzania

Njaa ndio inawatuma nyie wenyewe njaa tupu mnahamasi watu wale nini?🤣
 
Ni tatizo la kimfumo - huu mfumo huu wa SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA tangu uasisi wa Taifa letu ndiyo umetufikisha hapa.

Mfumo huu umetujengea hofu, kutojiamini, kujipendekeza mbaya zaidi bado unaambukiza hadi vijana wadogo kujikombakomba kisiasa. Mimi nafikiri baada ya kugundua mfumo huu umefeli Mwalimu angeuondoa na kutupatia Katiba Mpya mapema miaka ya 90, sasa hivi watawala sidhani wangekuwa wanatufanyia utani utani namna hii.

Sasa haya ndiyo matokeo yake kwamba badala ya wananchi kudai haki zao wao wanalilia vifuani huku wakiomba Mungu awasaidie.
 
Sasa royal tour itakuza utalii kivipi wakati mafuta yamepanda bei na wazungu wameteteleka kiuchumi kutokana na vita? Watalii hao hao ndo wanapigana sa sijui royal tour tunamtangazia nani aje? 😂
 
tangu lini ccm wakamjali mwananchi?
 
je na wale wanaofuja Mali za Umma nao Akili zao zimefubaa ?? Au ??
 
Ujinga na upumbavu ni kuwa chawa. Ukiwa chawa itakulazimu utetee uovu wa boss anayekulisha, kazi ambayo ni ngumu na fedheha sana.
 
karibuuu nagonga ugali wa asubuhi na Nyama kavu iliyopikwa kwa maziwa kabla sijaenda kuchunga ng'ombe. halafu hao unaowatetea wanaofanya juhudi na mikakati wao wanakula nini?
aisee ujingaa ni mzigo.
 
Kwa mujibu wa mawazo ya mtoa mada ni kwamba huu ujinga uliopo unatokana na chakula cha wanga specifically UGALI !! Na nafikiri huu Ugali unaleta matatizo mpaka kwa wasomi wetu , ndio maana utaona wengine wanakuwa wabadhirifu wa Mali za Umma bila kujua kwamba anaiumiza Nchi yake ambayo vizazi vyake vyote vitaishi humo !!!
 
karibuuu nagonga ugali wa asubuhi na Nyama kavu iliyopikwa kwa maziwa kabla sijaenda kuchunga ng'ombe. halafu hao unaowatetea wanaofanya juhudi na mikakati wao wanakula nini?
aisee ujingaa ni mzigo.
Hilo nalo neno !!
 
Wewe ndo Mjinga no Moja, tena wa Kwanza.

Utalii sio necessity, kwamba lazima watu watalii, Ila Chakula ni necessity hadi Somali wanahitaji Chakula ila Somalia hawahitaji kutalii.

Hizi nguvu zingeelekezwa kuzalisha Chakula kwa wingi mno tungeingiza pesa nyingi sana kuliko za Utalii. Wakayo wa Covid, Watu hawakutalii lakini walikula.

So weee ni Mjinga mkubwa sana
 
Mtoa mada wewe na ccm ndo wajinga kwa sababu unazozitoa zimeletwa na ccm hii hii. Na unafanya makusudi ili iendlee kutawala. Ccm ndo Ina uwezo wa kuondoa huo ujinga unaouongelea. Lkn ndo inayoundeleza.

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Swali. Je serikali hii ya ccm Ina uwezo wa kufanya hayo unayoyasema? Na pale Kuna mtu na uchungu na kuumia kwa wananchi. Juzi tu nape alikua anatumia chopa. Je hayo ya kupunguza matumiz inawezekana

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Kutojua kuandika vizuri ni dalili kamili ya ujinga Kama nilivyoona kwenye bandiko lako hili,
 
Lishe bora inatakiwa kuanzia utotoni, ubongo wa mtoto huwa unakuwa na kuwekewa msingi katika kipindi cha miaka mitano ya mwanzo, ukiharibu hapo huko mbeleni hata ukila balance diet haina maana sana.
Sasa wale waliokulia vijijini na hawakuwa na muda na haya Mambo still uwezo wa kuchakata taarifa Ni mkubwa unawaweka wapi.
Dunia Haina mjinga ila speed/ uwezo wa kuelewa huwa tunazidiana.
 
Ugali mazee mnausingizia tu

Huko west na Israeli na uarabuni tuseme pote tu wanakula ngano, sasa ngano na ugali si yaleyale tu.

Tena ungejua jinsi gluten inavyosemwa [ipo kwenye ngano] unaweza hata kusema ugali ni mzuri zaidi.

Ukisingizia maprotini sasa bado huchomoki tuna maharage, samaki, maziwa mbuzi n'gombe dagaa! Tena heeeh ugali na dagaa mazee acha tu.!

Ujinga wetu unaanzia kwenye kusingizia vitu vya nje yetu kama chanzo cha maamuzi yetu hayo ya kijinga, chochote utachoamua kusingizia iwe shetani, ugali, ccm etc kinakomaza ule ujinga halisi. Tabia za ubinafsi na uongo tusipozidhibiti zitaendelea kutugharimu.

Kile unachokitukuza huwa kina mtindo wa kutamalaki. Hivi ni lini tutakubali kwamba ni maamuzi yetu ndiyo yanapelekea hizi fujo? Bado natafuta jibu la kuongeza uwajibikaji, nikilipata ntawaambiaga. Ila kindoto ndoto kama tukianza kutukuza vitu vya maana na kuvipa airtime zaidi, nadhani tutatoboa. Tuige japan, urusi etc.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…