Hitimisho langu: Ujinga ni tatizo kubwa sana kwa Watanzania

katiba mpya itapunguza mfumuko wa bei!!!!!!!!
 
Rais hawezi kuchangiwa na wadau halafu akawa na 'guts' za kuwadhibiti katika shughuli zao zozote iwe biashara kwenye utalii, biashara za bidhaa nk. Haikubaliki hata dakika moja kwa rais ambaye ni mali ya Watanzania na sio watu binafsi wenye ajenda zao binafsi halafu watanzania waache kulalamika kisa na wewe ni mnufaika.

Hao wadau watajwe kwa majina ili tujue uzalendo wao na kuwafuatilia zaidi maana Watanzania ndio watakaotoa ruksa kwa hiari yao sio kulazimishwa kwa mihemko ya mtu mmoja anayetaka kujijengea sifa binafsi isiyokuwa na tija.

Watalii wanakuja kutoka na taratibu za nchi zao kuruhusu kutoka baada ya wimbi la ugonjwa wa UVIKO-19. Nyalandu alishawahi kutangaza utalii kwa jinsi hiyo hiyo na hata alirekodi na kwaya moja nyimbo ambazo zilienda hadi za mbali zikionesha vivutio vingi vya utalii leo hii mnataka kuwadanganya Watanzania kwamba ninyi ndio mmebuni wakati hata hati miliki ya filamu yenyewe sio ya kwenu!!!
 
Naona umeamua kuwaangushia watz karibia mil.60 jumba bovu kwa kuwaita wajinga....ety kwa sababu wanakula ugali.
Ujinga uko huko juu maamuzi yanakotokea....

Kinachosababisha uwaite watanzania wajinga ni uvumilivu wao.....
Kumbuka ujinga uko huko juu ambako hamjui Sera na siasa za kimataifa zinavyokwenda mpaka pale tatizo linapotokea ndipo mnahaha kuja na matamko.

Ujinga ni pale utakapo sema Tanzania hatuchimbi mafuta na tuna gesi....

Ujinga ni pale unapowaambia watanzania kwamba bei imepanda kwenye soko LA dunia hata wakati hata wewe mwenyewe hujui hilo soko LA dunia lilipo.

Ujinga ni kudharau chakula chetu huku ukijua wote wana uwezo wa kununua pizza na Burger.

Ujinga ni kuitegemea movie kuwa italeta watalii na watalii tangiapo walikuwa wanakuja tatizo likaletwa na korona.

Wote tuna nia njema ya kuiona Tanzania inayopendeza isiyo na ubaguzi na dharau.

Mleta mada wewe ni mjinga.
 
Umasikini ndio unazaa ujinga. Ccm inawafanya watz wawe masikini kwa kuwatoza kodi kubwa Ili wasiinuke kiuchumi wazidi kuwa masikini, case study ushuru dhalimu wa uagizaji magari na bidhaa zalishi toka nje, utitiri wa kodi kwenye mafuta wizara 21 zote zinategemea kuchukua pesa ya Mtanzania masikini kupitia KILA lita ya mafuta.
Kwan kodi pekee ndo chanzo cha mapato ya kuendesha nchi, mbona mkoloni hakuendesha nchi kwa kodi na mambo yalienda na maendeleo makubwa yanaonekana.
 
True watu wamefadhili wamedhamini filamu means upo mifukoni mwao washakununua huna sauti nao tena,wametoa pesa zao ni lazima zirudi tena kwa faida,zitarudije sasa bila kuwaumiza watz.Kesho utaletewa vimemo na hao hao waliokupandisha ndege wanashida zao huwezi kataa.
 
Kuleni Dona a.k.a Donald Trump

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Umeongea vizuri kwenye swala la utalii hapo juu... Ila swala la 2 natofautiana kidogo na wewe..

Kwanza kweli vita lazima iathiri mafuta.. Kwa vyoyote mafuta yamepanda.. Ila kama serikali ili paswa itafute njia nzuri kupunguza garama za mafuta.. Mfano...

Kutokana na matatizo haya serikali ilibidi ifidie garama za mafuta...
Kwanza baadhi ya viongozi kama wabunge,wkuu wa wilaya na wakuu wa mikoa na wengine wkatwe 30%ya mishahara yao,kwa mafuta wanayotumia..

Kupunguza posho na safari zisizo na ulazima.... Then kuongeza kodi kwa vitu visivyo vya ulazima.. Kama vinywaji(pombe,juice)
 
Mkuu huyu jamaa ni team NAPE.wazee wa kulamba miguu.
Hapo alipo ashakunja zake hela za tour na covid ndio anakuja kutuita wajinga
 
Ukisoma maoni mengi ya whatsapp unagundua madhara ya ujinga kwamba yamejikita katika jamii yetu kwa kina.

Umejitahidi kufafanua hoja yako lakini ni tatizo linaloendelea kutusumbua. Tunapenda sana habari nyepesi za kina Wema na Diamond pamoja na kina Mwijaku, sababu ni ujinga huo huo.

Hatuna tamaduni za kusoma magazeti ya kiuchumi yenye kupanua uelewa wetu, tumejikita katika kuendekeza masikhara wakati zinapoletwa hoja za maana.

Tunajadili nani kalipia gharama za Greenburg kuja na kuandaa hiyo video tukisahau fursa nyingi sana zinazotangazwa na hiyo hiyo Royal Tour,, ni ujinga tu na sio sababu nyingine inayoyakwaza maendeleo yetu.
 
Sasa royal tour itakuza utalii kivipi wakati mafuta yamepanda bei na wazungu wameteteleka kiuchumi kutokana na vita? Watalii hao hao ndo wanapigana sa sijui royal tour tunamtangazia nani aje? 😂
Royal Tour ni tangazo la biashara, na siku zote hufanyika muda wote. Vita ina mwisho wake, na tangazo linakuwepo mtandaoni likizoeleka machoni mwa watu.
 
Umesema kweli kabisa! Ujinga unawafanya watu kutofuatilia habari za msingi na kuishia kufuatilia mambo ya ajabu. Hatimaye tunapata jamiiyq ajabu sana inayoendesha mijadala ya ajabu kabisa
 
Umesema kweli kabisa! Ujinga unawafanya watu kutofuatilia habari za msingi na kuishia kufuatilia mambo ya ajabu. Hatimaye tunapata jamiiyq ajabu sana inayoendesha mijadala ya ajabu kabisa
Samia aende mpaka USA na kufanya makubaliano ya kuitangaza Tanzania, hawezi kuwa mjinga kwa namna yoyote ile. Halafu hili ni wazo lililozaliwa huko huko Nje walipoona rais ni mwanamke wakaona ni wakati wa kutangaza nchi yake, ni aina fulani ya favor za kisiasa.

Nongwa zetu nyingi za mitandaoni ni kielelezo cha ujinga uliokomaa vichwani mwetu.
 
The most dangerous thing is an ignorant person in power.
 
Wali una kiasi kidogo cha wanga kuliko ugali, wachina chakula chao kikuu ni wali ila kiwango cha kiribatumbo ni kidogo sana.
Hapana, wali ndo una kiasi kingi cha wanga kuliko ugali.

Narudia ukilinganisha wali na ugali, wali ndio una kiwango kikubwa zaidi cha wanga.

Ugali unadumu zaidi mwilini kwa sababu tu mmen'genyo wake mwilini upo polepole una ustaarabu ukilinganisha na wali vuu vuuuu chap umeisha mwilini.
 
mtoa uzi pia naye ni mjinga hata ukiutafakari uzi wake pia ni wa kijinga sababu haujatoa suluhisho la kiuchumi wa namna ya kujinasua hapo tulipo bali anaishauri serikali iwe na mbadala wa ugali.ukiangalia mtoa uzi pia kwa kiasi kikubwa amelelewa mazingira ya kula ugali na pia watz wengi tumeishi kutokana na ugali na akili zao ziko vzr tu.wasomi wengi wametokana na familia duni ambao chakula chao mostly ni ugali sasa namshanga sana mtoa uzi kuongea ujinga huo.
 
Habari za burudani mkuu zipo kote hata huko kwa wenye akili na wanazifuatilia kweli kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…