Hivi huyu ni Kiongozi au tapeli? Kwanini Mamlaka zinamlea kiasi hiki?

Hivi huyu ni Kiongozi au tapeli? Kwanini Mamlaka zinamlea kiasi hiki?

Kama ilifikia mahali kiongozi anatoka eneo la himaya yake yake ya kazi anakwenda kuvamia maduka ya watu, kwanini kiongozi kama huyu asiitwe jambazi?

Huu unyang'anyi au uporaji wa mali za watu usiku unatumwa na nani? Halafu mpuuzi moja akitoka hapo anamtaja hadi Mungu.

Kwa mujibu wa gazeti andiko toka gazeti kiuchunguzi la Sauti huru hizi ni video zilizonaswa na CCTV zikionesha jinsi DC wa Hai alivyovamia maduka ya watu Usiku mjini Arusha akinyang'anya pesa za wafanyabiashara kwa nguvu.

Hawa ndio viongozi wa umma wa serikali ya mwendazake.

View attachment 1746084
View attachment 1746085
Kwa kweli bora Meko amefia mbali.
 
Huu upuuzi wa kurekodi video inayoplay kwa simu acheni! Si urushe video yenyewe kutoka kwenye NVR au DVR!

Wabongo hatuwezi kabisa kujihangaisha.
 
Sura ya sabaya live bila chenga, kasimama mikono mfukoni alafu jamaa mmoja akatoka kushoto kuja kumnong'oneza jambo.
 
Hii ni video fupi ambayo leo na jana imesambaa sana mitandaoni hasa twitter ikionyesha mkuu wa wilaya ya Hai ndugu Sabaya akikusanya kodi kwa mabavu yenye kiwango cha vita!
View attachment 1746415
Tofauti yake na ujambazi wa kawaida,ni kwamba ujambazi huu unafanywa na mwenyekiti kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya.ambaye ndiye anayetakiwa apelekewe malalamiko
 
Back
Top Bottom