Hivi inakuaje mtu anachagua akifa achomwe (Cremation) mimi huwa naona kama ni Cult

Tatizo si ecosystem, tatizo ni tamaduni.

Unishasema hili ni kaburi langu asije kuzikwa mtu mwingine hapa, ushachukua nafasi kinyume na kanuni za ecosystem za kuachiana nafasi.
Mapori ni mengi sana mkuu ila binadamu tu ndiyo tumekuwa wabinafsi kupitiliza.

Kuna sababu gani watu warundike makaburi palipojaa mfano pale Kinondoni hadi wanafukua makaburi mengine ilimradi tu wazike hapo.
Wamasai ndivyo zilivyo mila zao na zimewapatia minofu fisi.

Je maiti inayochomwa moto imenufaisha vipi viumbe hai zaidi ya kuleta athari za uharibifu wa ozone layers tokana na moshi?

Ubinadamu ni kazi/the humanity is work.
 

Makabila yetu mengi yalikuwa yanazika kwa namna tofauti lakini still mwili unaenda ardhini. Dini zilileta utaratibu uliobora kutokana na tamaduni za huko sio mbaya kwa sababu still ni kwenye ardhi.

Sasa kama sio cult kama hata huko toka enzi wanazikana huu utaratibu wa kuchomana unatoka wapi?

Huyo Askofu Desmund Tutu pamoja na kuwa Askofu wa Anglikana bado anaweza kuwa kwenye Cult.

Wewe unaona ni sawa kuzikwa kwenye maji kweli yaani hata haiingi akilini.
 
pale tokyo ukisema watu wazike kwa kufukia , miili itatupwa barabarani
Wamelazimishwa kuishi papo hapo? Mapori yamejaa tele duniani kwanini walazimishe kubanana sehemu moja tu?

Tena uchumi wa Japan ni dunia ya kwanza, walivyo wabinafsi waliendekeza uzazi wa mpango na punyeto hatimaye wamebaki na rasilimali vitu tele na kuwa na uhaba wa rasilimali watu kusimamia na kuendesha rasilimali vitu.

"Failing to plan is planning to fail"

Ubinadamu ni kazi/the humanity is work.
 

Umeeleza kwa kina ila zote ni zakutisha na mimi naona zinaondoa utu wa binadamu na pia wanafanya hivyo inaweza kuwaathiri akili au pia ikaondolea kuthamini uhai. Hii ni cult sio normal. Mambo mengine sio ya kuiga.
 
Wewe una elimu ndogo ya dunia tu.

Hujui tamaduni za sehemu nyingi watu wanachoma?

Hujui hao wazungu waliokuleteeni Ukristo nao wanachoma?

Hujui kwamba tukianza kujadili cults hata hizo dini mnazoziamini nazo mimi nikitaka kuziita cults naweza?

Kinachotofautisha dini na cult ni nini zaidi ya namba ya watu na miaka tu?

Unajua kuwa hata hizo dini zenu zilivyoanza zilikuwa zinaitwa cults?

Unajua hizo tamaduni zako nazo kuna watu wanaziona cults tu?

Sasa unapojiona uko beyond cults, wewe mwenyewe unajuaje haupo katika cult uliyoikubali tu kuwa ni dini yako au utamaduni wako?

Unaelewa kwa nini neno la utamaduni kwa Kiingereza, "culture", linaanza na "cult"?

Unajua kwa nini kwenye Kiswahili neno "ustaarabu" linataja "arabu"?
 
Asante sana mkuu umeeleza vema
Upo vizuri.

Ndio maana wanajikuta wanakubali kuchomwa na ilihali wanajua ndugu zao hapendi na ni kinyume na tamaduni yao.
 
mkuu unaweza kupeleka watu wangapi kwa mwezi marekani na canada ? vijana wanauwezo mkubwa sana wa kufyeka mapori
Ishu si kufyeka bali ni kujaza maeneo yaliyo wazi kimakazi na wawepo watu wanaoendana na rasilimali vitu si kurundika rasilimali vitu pasipokuwa na balansi ya watu kusimamia na kuendesha.

Ubinadamu ni kazi/the humanity is work.
 
You are not your body or mind.

So nakubali kuchomwa itafaa zaidi maana unakuwa umesoeed up kusambaratishwa kwa mwili na pia kumtunza mazingira na space
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…