Tunashukuru kwa historia nzuri hatukuwa tunaijua
Ila tamaduni nilizosema ni zile nzuri ndio tuziendeleze.
Jua kuna watu ambao ni Wahafidhina/ traditionalist na wengine ni Liberal kwa hiyo huo utaratibu wa kuchoma hata kama una manufaa bado kwenye jamii yetu hatuukubali.
Kutokubali mambo mapya hata kama hamkubali, ni muhimu kuangalia kama sababu zina mantiki.
Hutakiwi kukataa au kujubali jambo kwa sababu ni la zamani au jipya tu, unatakiwa kuangalia mantiki. Bila kujali jambo ni jipya au la zamani.
Kwa sababu mnaweza kutokubali kitu kipya kwa logical fallacy tu, ya "argument from tradition".
Mkakataa kusoma shule na kuchanganyika na wageni, kwa sababu katika utamaduni wenu kulikuwa hakuna kusoma shule wala wageni hao.
Kumbe dunia inayokuja kuwakabili ni dunia ya kusoma shule na kuchanganyika na watu mbalimbali.
Mkaachwa.
Jamii nyingi zilizoachwa ni zile ambazo zilikataa kubadilika.
Hata huo utamaduni unaousema nao unabadilika.
Sasa, uking'ang'ania kitu kimoja na kusema huu ndio utamaduni wetu, bila ya kuweza kubadilika, utapitwa na dunia.
Utabaki kwenye toroli la kuvutwa na mtu, farasi au ng'ombe ukikataa motorcar kwa sababu si utamaduni wako.
Sasa unapokataa kitu, una sababu za kimantiki?
Au unashikilia utamaduni tu?