Hivi inakuwaje mtu anajua kusoma Quran ila lugha ya kiarabu haijui?

Ni aidha uandike kwa kiswahili au kiarabu kabisa tujue moja
 
Kiarabu kiko standard Arabic,ndio lugha inayotumika katika quran,na kuna kiarabu cha maandko na matamshi tofauti,inategemea gazeti limeandikwa kwa kiarabu kipi.Kumbuka Qur'an ni standard Arabic sio lugha ya kienyeji.Ni kama kiingereza kuna :
1.American English
2:British English
Halafu kuna English
1:Biblical English(ambayo pia inatumika kwenye vitabu vya dini kama Qur'an,Gita,Nk)
2:English ya sheria
3.English ya science
4.English ya mahesabu nk
 
So lugha iliyotumika kwenye kuandika Quran ni tofauti na kiarabu chenyewe?
Kiarabu cha Qur'an ni Standard Arabic, ni tofauti na kiarabu cha kuongea.Ndio maana hata muarabu,aliyezaliwa arabuni ni mpaka afundishwe Qur'an,na anaweza kufundishwa na mtu ambaye,hajazaliwa nchi za kiarabu,na hana asili ya kiarabu,iwe tu huyo mtu,amejifunza Qur'an na kuhitimu mafunzo yake.
 
Umeelezea vizuri
 
Umeeleezea vizuri sans.
 
Wewe ulijuaje kama kweli hilo gazeti limeandikwa kiarabu? Kumbuka Kuna lugha zinafanana na kiarabu Ila sio kiarab
 
Usipoelewa mifano hii basi una lengo tofauti na ulichoandika/kilichoandikwa

1.English, Kiswahili na Indonesia wanatumia herufi za aina moja... je ukipewa gazeti la Kiindonesia utasoma na kutafsiri?

2.Tamil na Hindu zote ni Lugha za Kihindi... je wanafanana?

3.Persian, Arabic na Urdu zote zinatumia herufi za kufanana... je huyo Mfursi ukimpa gazeti la Urdu au la Kiarabu atasoma na kutafsiri

Tuache huko twende kwenye swali lako jibu lake ni kwamba...

Kiarabu cha kwenye Quran ni tofauti kidogo na viarabu vingine kwani chenyewe kinatumia utaratibu wa irabu (fataha/kisira/dhuma/shadda/sakna/tanwin n. k) kitu ambacho lugha zingine za kiarabu hutakuta hizo mambo... hiyo ni moja

Mbili ni kwamba lugha moja inakuwa na lugha nyingine za kufanana nayo, japo mtu anaweza akaelewa/akasoma/akatafsiri/akaongea/akaandika lugha ya mwenzake wanaoendana itakuwa kwa taabu kidogo

Mfano tuchukulie hicho hicho Kiarabu kuna cha Misri, Saudia, Pakistan, na kadhalika
 
na wapo hao waarabu wanaokaa uarabuni wamezariwa uarabuni wanaojua kiarabu na kukisoma kiarabu pia na hata kukiandika

lakini hawawezi kusoma QURANI

JE UNAJUA HILO
Nimewahi kusoma mahali kuwa lugha ya kiarabu ndio iliamriwa kutumika katika Qurani sasa mbona unatutatiza tena
 
Mnasahau kama kiarabu kina irabu pia kina isimu ya lugha. QURANI imeandikwa na kupewa irabu, hata kama hujui isimu unasoma vizuri. Mataifa yote yanweza kusoma kurani Kwa sabab hiyo. MAGAZETI hayana irabu, yanataka uijue isimu kwanza ndo usome. Ni Sawa na kusema neno 'ktk Lng lng' yani mbongo atasoma 'katika lengo langu' lakini Kwa asiejua kiswahili vizur hili neno la 'Ktk' lnamsumbua. Hii lugha ambayo haina irabu ndio hiyo ambayo inatumika katika magazeti ya kiarabu
 
Hawataelew hili mkuu. Nimerudia tu wazo lako hapo juu
 
Kujua kusoma Lugha Fulani haikufanyi ujue kuiongea.

Kwenye lugha kuna Skills zifuatazo
1. Reading Skill
2. Listening skill
3. Writing Skill
4. Speaking Skill.

Kujua skills Zote hizo unaitwa Mahiri WA lugha Fulani.
Kwa mfano kuna Watanzania wanajua kuongea(speaking) Kiswahili na ukisikia(Listening) lakini hawajui kukiandika Wala kusoma.

Pia wapo Watanzania wengi kusoma kingereza wanajua na wanakisikia lakini kukiongea ni mtihani.


Hivyo sio ajabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…